Jerusalem unaonekana post zako ni majibu ya Malaria sugu lakini Ukristo hauna mafunzo hayo ya kudhihaki dini nyingine yamkini utaishushia hadhi dini yako kwa yesu kristo.Kama kweli umeiva vema katika Ukristo utajaa moyo wa upendo kwa wale wasio wakristo wakiwemo watanzania wenzetu na ndugu zetu waislamu. Hoja za Malaria sugu sio za waislamu wote wanaipenda Tanzania na hoja zako Jerusalem sio za wakristo wote wanaoitakia mema nchi hii.
Kama ningekuwa nawafahamu (Malaria sugu na Jerusalem) nje ya mipaka ya jukwaa la jamiiforums, ningefanya kazi ya kuwasuluhisha ili kila mmoja wenu akabaki na dini yake na kisha mkatuachia Tanzania yetu salama salimini.