Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imerasimisha usafiri wa bajaji na bodaboda na kuweka kanuni na mashrati maalum katika biashara hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Usafiri na Leseni Zanzibar, Muhammed Simba Hassan, alisema serikali imechukua uamuzi huo kutokana na vijana kujiajiri katika usafiri huo.
Alisema usafiri huo utasajiliwa kwa ajili ya biashara ya kusafirisha abiria na kuwa na namba maalum za usajili.
Simba alisema madereva wa vyombo hivyo watapewa elimu ili kufuata sheria za usalama barabarani na kuepukana na ajali zisizo za lazima.
Kuhusu nauli katika usafiri huo, Simba, alisema itakua ni makubaliano kati na mtoa huduma lakini wakigundua kama kutakua na malalamiko kuhusu nauli itabidi waweke kiwango maalum.
Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Rahma Kassim Ali, alisema usafiri huo unaendelea kukua kwa kasi na kwa vijana ni sehemu yao ya ajira katika kujipatia kipato.
Alisema urasimishwaji huo umekuja kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 48 (4) cha Sheria ya Usafiri Barabarani Na. 7 ya Mwaka 2003.
Waziri huyo aliwataka wananchi wanaotaka kuingia katika biashara hiyo kufika katika mamlaka husika ili kupatiwa utaratibu wa kupata leseni ya biashara hiyo.
Pia aliwataka wananchi wanaotumia usafiri huo kuwa waangalifu na kuhakikisha wanapanda katika vyombo vilivyosajiliwa ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri na Usalama Barabarani, Haji Ali Zubeir, akizungumzia utambulisho wa bodaboda hiyo, alisema huduma hiyo itatofautiana na vyombo vinavyosafirisha abiria wa kawaida kwa kuwa vyombo hivyo vitakuwa na usajili maalum.
Pia alisema waendesha bodaboda na bajaji watakuwa na mavazi maalum yanayowatambulisha kuwa wanafanya biashara hiyo na watapangiwa vituo maalum kwa ajili ya kupakia abiria.
“Hadi tunatoa taarifa hii ya urasimishaji wa usafiri huyo tayari tumeshasajili vyombo 13,000 zikiwamo bajaji na bodaboda,” alisema.
Muhammed Mahmoud Hassan, Mtunza Hazina wa Jumuiya ya Bodaboda Zanzibar, ambaye pia ni dereva wa usafiri huo katika kituo cha Hospitali na Mnazi Mmoja, aliipongeza serikali kwa hatua hiyo kwa sababu ni kilio chao cha muda mrefu kutaka urasimishaji wa biashara hiyo.
“Tumefurahi sana kuwa biashara hii sasa ni rasmi, cha msingi kujielewa na kufuata masharti ili kuepuka kufanya makosa” alisema.
Alisema kurasimishwa kwa biashara hiyo na kuwekewa kanuni maalum, kutasaidia kupunguza malalamiko ya kuwa wafanyabiashara hao kujihusisha na matukio ya kihalifu ikiwamo udhalilishaji wa kijinsia na uporaji.
Madereva wanatakiwa kuelewa kuwa kazi hiyo ni kama kazi zingine na wananchi wahakikishe wanatumia usafiri huo kwa watu wanaowatambua ambao watakua na utambulisho maalum.
Yasir Nassor, dereva wa bodaboda katika kituo cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, alisema urasimishaji wa usafiri huo utapunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili na kuahidi kuendelea kufuata miongozo iliyowekwa.
Ippmedia