Zanzibar 2020 Zanzibar: Wafanyabiashara wailaumu Serikali kuvuruga shughuli zao kila Uchaguzi unapokaribia

Stone Town

Senior Member
May 28, 2007
114
26
Wakizungumza leo asubuhi, Wafanyabiashara wachache waliokutwa katika maeneo yao ya biashara, bila kufungua maduka ama vitalu (vibanza) vyao ndani ya soko kuu la Zanzibar, Marikiti, wafanyabiashara hao walisema kuwepo kwa idadi kubwa ya wanajeshi na askari polisi, kunafanya washindwe kupata pesa, hivyo maisha yao kuwa magumu.

Siku chache kabla ya kupiga kura na kabla ya kutangazwa matokeo, imekuwa ni kaaida kwa Zanzibar kufungwa kwa aeneo ya biashara kwa hofu ya kutokea rabsha baina ya makundi ya wanachama wa vyama vikuu vya siasa; Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa ACT-Wazalendo.

Jana majira ya saa 1.40 hadi saa 3.15 usiku, nilitembelea eneo maarufu la kuuza vyakula na vinywaji baridi jioni, Forodhani, na kukuta meza moja tu ya kuuza vyakula.

Katika meza hiyo iliyosheheni mishkaki ya samaki; nduaro, chaza, mihogo ya kukaangwa, mishkaki ya nyama ya ng'ombe na kuku, viazi vitamu vya kukaanga na mbatata, hakuna wateja walioshuhudiwa hadi naondoka eneo hilo.

Mfanyabiashara wa vyakula hivyo, Mwinyi Makame Khamis alilalamika kuwa pamoja na umuhimu wa uchaguzi, lakini kwa Wazanzibari imekuwa ni kero na chanzo cha kuwapa umasikini zaidi.

Amesema meza yake iliyokuwa na bidhaa za Sh.470,000, huenda akapata hasara kwa kuwa hakuna wateja, hivyo kuhofia kupoteza hata mtaji wake.

"Hapa naumia sana, najua nitapoteza mali zangu, lakini hii yote ni kwa ajili ya uchaguzi na tamaa ya madaraka ya watu wenye nafasi, sisi masikini tunapata shida sana, wao wenye mapesa wanataka nafasi za uongozi ili wapate zaidi, lakini kwa gharama ya umasikini wetu," amesema kwa hisia kali.

Juma Ismal, muuza samaki katika soko kuu akiongea asubuhi ya leo amesema kwamba hana uhakika kama anaweza kuuza samaki wake kwa kuwa watu wengi wana hofu ya kupigwa ikiwa watatoka majumbani mwao kwenda kununua vyakula na bidhaa nyingine kwa kuwa kuna wanajeshi.

Siku tano kabla ya uchaguzi leo, maeneo mengi ya Zanzibar yameshuhudiwa kuwa na askari Polisi na wanajeshi wengi wakiwa na silaha wakiranda katika mitaa na barabara za visiwa hivyo.

Jana sehemu mbalimbali za Zanzibar zilipigwa mabomu ya machozi na wana usalama hao, kila walipoona makundi ya watu, hasa vijana wakiwa barabarani au kukaa kwenye vijiwe, maarufu kwa jina la Maskani.
 
Watawaliwa huwa hawana hiyari hadi mtawala atake...
Labda gavana atawapa mitaji...
 
Back
Top Bottom