Zanzibar waanza kupewa gesi bure | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar waanza kupewa gesi bure

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 14, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  na Mauwa Mohammed, Zanzibar



  SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeanzisha mpango wa utoaji wa gesi ya kupikia bure kwa wananchi kama moja ya hatua za kudhibititi ukataji wa miti katika maeneo yote nchini hapa.
  Hayo yalielezwa na Waziri wa Kilimo na Maliasili, Mansoor Yussuf Himidi, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Darajani Mjini Zanzibar kuhusu maadhimisho ya siku ya upandaji miti.

  Alisema jukumu la usimamizi wa rasilimali za misitu ni la wananchi wenyewe hivyo amewataka kuendeleza tabia ya kuitunza.
  Mansoor alisema mwaka huu 2011 wizara hiyo imeandaa upandaji miti kitaifa katika eneo la Bumbwini Mafufuni, Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kusini Unguja.

  Alibainisha kuwa jumla ya hekta 959 hukatwa kwa mwaka lakini zinazopandwa ni hekta 450 kwa mwaka hivyo kuna kila sababu ya wananchi kufahamu juu ya umuhimu wa upandaji wa miti nchini. Alisema upandaji wa miti utafanyika Aprili 16 mwaka huu kwa upandaji wa mikoko na mikandaa ili kuimarisha ikolojia ya misitu nchini hapa. Mradi wa utoaji gesi bure uitwao Hifadhi ya Miti Asili Zanzibar (HIMA) unagharamiwa na serikali ya Norway hapa nchini na utatumia jumla ya sh milioni nne kwa muda wa miaka minne.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  embu wa fanye hivyo bara afu tuone
   
 3. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  naona wameamua kufanya kila kitu ili wawakere watu wa bara na kuhakikisha muungano unavunjwa
   
 4. babu M

  babu M JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 3,994
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  Hiyo figure ipo sawa?
   
Loading...