Zanzibar unawezadhani hakuna ubadhirifu ila laaa

Zanzibar unawezadhani hakuna ubadhirifu ila laaa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Zanzibar tuliaminishwa watu awapigi mpunga ila nimefuatilia madudu yanayoibuliwa na Rais aliyepo nikabaini binadamu hasa waliosoma wanatumia vyema taaluma zao kufanya ubadhirifu kuliko kuwatumikia wananchi. Baada ya tumbuatumbu kuwa kali wazee wameanza kumlalamikia Rais Mwinyi kwamba anafukua sana makaburi. Nikajiuliza wanapata wapi ujasiri wakusema Rais anafukua makaburi? Je ukiiba regime hii ndo ulindwe na regime unayofuata?

Lakini pia Kama eneo dogo Kama Zanzibar panaweza kuwa uchochoro wakuoba Mali za umma, vipi kuhusu bara?

Lakini pia Kama wazee wa CCM wanaweza kuhoji kwanini Rais anafukua makaburi kila watoto wao wamefutwa kazi au kushushwa vyeo kwanini spirit hii isiwaguse na masikini ambao wakituhumiwa tu jela?

Mhe. Rais ukiacha kufukua makaburi utakuwa umeacha kurejesha Mali za umma zilizoibwa na hivyo kukiuka kiapo chako. Wezi haki yao ni kushtakiwa,kufilisiwa na fedha kurejeshwa kwa umma bila kujali waliiba lini
 
Nani kakuaminisha kuwa Zanzibar watu hawapigi mpunga?
Huko kwenu bara kuna afadhali, mpunga watu wanapiga lakini unaweza kuona miundo mbinu inajengwa na kumalizwa. Zanzibar barabara ya kilomita moja nanusu inasubiriwa 2025 ndio imalizwe kutiwa lami. Traffic light zile bulb za LED zimewashinda kuzisimamia. Wakadai kufunga camera mji mkongwe watu wamepiga hela.

Yaani utawala Sheni na Balozi, imefanya kufuru katika kuiba mali za umma. Leo rais anasema hataki kufukua makaburi, kama hufukui makaburi na kuwawajibisha waliokula mali za umma, unategemea watu wajerekebishe vipi? Viongozi wa ZSSF wamepiga hela chafu, wakasimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Ishu imeisha kimya kimya, watu wameondoka zao na mabilioni hawana wasiwasi, kwanini? Rais hataki kufukua makaburi.

Kama hataki kufukua makaburi, anahangaika nini na kuwasimamisha watu kazi na kupisha uchunguzi? hakuna palipopigwa Mpunga bila kuwepo mkono wa kiumbe ambacho katiba inamlinda kushtakiwa kwaio Rais Mwinyi a chill tu naa aache kutaka kujua nini kimeibiwa mana hana uwezo wa kushuhulikia mwizi/wizi wakuu.

Hakuna mali ya umma iliorudi tangu hapo mwanzo, akifukua kaburi anakuta sura ya mshkaji mmoja ivi, anaanza kupata aibu na kukaushia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom