Elections 2010 Zanzibar: Uchaguzi waahirishwa wadi nne (4)

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
31/10/2010

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema italazimika kurejea uchaguzi katika wadi nne za Mji Magharibi kutokana na hitilafu zilizotokea katika karatasi za kupigia kura.

Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kupokelea matokeo ya uchaguzi ndani ya ukumbi wa hoteli ya Bwawani Mjini Unguja, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Khatib Mwinyichande alisema kuakhirishwa kwa uchaguzi huo kunatokana na kasoro zilizojitokeza dakika za mwisho.


Akizitaja wadi hizo mbele ya waandishi wa habari na wangalizi wa chaguzi huo, Mkurugenzi wa ZEC, Salim Kassim Ali alisema, Wadi ya Mchangani ambayo ipo katika Jimbo la Mji Mkongwe, Wadi ya
Kwahani ambayo ipo katika Jimbo la Kwahani, Wadi ya Miembeni ambayo ipo katika jimbo la Kikwajuni na Wadi ya Nyerere ambayo ipo katika Jimbo la Magomeni.

"Wakati zoezi hili la usambazaji wa vifaa linaendelea tume imepokea taarifa kutoka katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wa wilaya mjini inayoonesha kuwa kumetokezea tatizo linalohusiana na uchapishaji wa karatasi za kupigia kura za wadi nne za uchaguzi" alisema Ali.


Alisema tatizo hilo linatokana na baadhi ya wagombea wa wadi hizo kuonekana katika wadi ambazo hawahusiki kupigiwa kuwa na pia baadhi ya wapiga kura wa shehia kulazimika kupiga kura kati ya wadi ambazo sio za kwao.


Hata hivyo Mkurugenzi huyo alisema kutokana na upungufu huo tume ya uchaguzi ilijadili na kuamua kuwa uchaguzi wa wadi hizo nne za mjini utafanywa wa marejeo siku ya Jumapili, Novemba 28 mwaka huu.


credit : Salma Said via mzalendo.net
 
hiyo ndiyo tume yetu, 'kasoro zimegundulika dakika za mwisho!' huu ni uharibifu tu.
Wanasheria wa nchi hii, Hivi hakuna jinsi kuwapeleka ktk kesi watendaji hawa? Mfumo wetu wa sheria ukoje?
 
Walivyokuwa mabingwa wa kasoro hata wakichakachua kasoro zitakuwa nje nje mpaka iwe aibu yao
 
Kama wangekuwa wawazi, wakashirikisha vyama kukagua vifaa hivi mapema, haya yasingetokea...
 
Back
Top Bottom