Zanzibar Tunamtaka Rais huyu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar Tunamtaka Rais huyu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vitendo, Jan 20, 2010.

 1. Vitendo

  Vitendo JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 597
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  NI miaka miwili sasa tangu nilipomsifia Balozi Ali Abeid Karume (Balozi Karume) kwa hatua yake ya kutangaza kugombea urais wa Zanzibar wakati utakapofika.

  Wakati akiwa nchini kwa kazi maalum ya kiserikali Januari 2008, Balozi Karume ambaye anawakilisha Tanzania nchini Italia, alitangaza rasmi kuwa atagombea urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa 2010.

  Katika tamko lake hilo, alisema wazi kuwa ameamua kutangaza mapema ili kuwapa wananchi muda wa kutosha kutafakari kwani anaamini ni haki yao kufanya uchambuzi kwa yeyote anayetaka kuwa kiongozi wao.

  Hakueleza hasa ni mambo gani atayapa kipaumbele iwapo chama chake cha CCM kitamuidhinisha kugombea nafasi hiyo na atakapochaguliwa na wananchi.

  Lakini alieleza kwamba jambo kubwa analoona halikwepeki kwa sasa akichaguliwa kuwa rais, ni kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Lengo ni pamoja na kuondoa siasa za chuki na kujumuisha kila mwananchi katika serikali ili iungwe mkono katika majukumu yake.

  Wapo watu waliomshangaa Balozi Karume kwa tamko lake la kutaka kugombea urais. Wana sababu zao. Lakini nilimuunga mkono na kumfanyia mahojiano maalum.

  Katika makala niliyoandika baada ya mahojiano naye yaliyofanyika mjini Dar es Salaam, nilisema alifanya jambo jema na kutangaza mapema nia yake ya kuja kuomba ridhaa ya wananchi wa Zanzibar.

  Nilihimiza ule ulikuwa ni wakati mzuri kwa kila Mzanzibari kujipima uwezo wake na iwapo anadhani ana hamu ya kuongoza serikali ajitangaze mapema.

  Faida ya mtu kujitokeza mapema na kutangaza nia yake ya kutafuta uongozi ambao unahitaji ridhaa ya wananchi ni moja kubwa: wananchi watamjadili kwa mapana na siku ya kuchagua watakuwa wameshafanya uamuzi.

  Nilihimiza na kuhamasisha watu kujitokeza kumfuata Balozi Karume kwa sababu uchaguzi ni hatua inayopaswa kufanyika kwa uwazi na kwa mujibu wa taratibu.

  Itakuwa uhuni mtu kukaa kimya kwa muda wote halafu akaja kujitokeza dakika za mwisho ambapo atakuwa amewanyima wananchi fursa ya haki ya kumchambua alivyo.

  Isitoshe, ni kitendo cha ushetani mtu aliyetia nia ya kuja kugombea wadhifa mkubwa kama wa urais au ubunge na uwakilishi akanyamaza kimya asijitangaze hadharani mapema nia yake hiyo; kumbe chinichini anafanya kampeni.

  Tunapoeleza mambo haya yanayohusu umma, huwa tumeshaangalia mbali kwa kuzingatia mazingira mbalimbali. Tunajua mienendo ya wanasiasa wa kileo na hasa hawa tuliowazoea.

  Kwanza, inasikitisha kuwa hadi naandika makala hii – miaka miwili kamili tangu wakati ule – ni Balozi Karume peke yake aliyeweka wazi dhamira yake ya kuwania urais.

  Pili, sijapata kusikia chama chochote cha siasa kilichopiga marufuku wanachama wake kujitangaza kwa yule anayetaka kugombea uongozi unaopiganiwa wakati wa uchaguzi mkuu wa taifa.

  Kama kipo basi viongoz iwake watakuwa hawajui maana ya kuwapa fursa wanachama kujitangaza kwa wananchi au wanajua lakini chama kinataka kuja kuvuruga wapiga kura dakika za mwisho kwa kuwashtukiza na kuwalazimisha wachague hata “jiwe.”

  Uzoefu unaonyesha vipo vyama vinavyonyonga wanachama wake dakika za mwisho kwa kuwakata pande na kuteua wengine kinyume na matakwa ya wapiga kura. Hii inadhoofisha demokrasia, ikiwemo ya kuridhia maoni ya watu.

  Bahati njema Balozi Karume anaishi nje ya Zanzibar na Tanzania. Ni mara chache anakuja nchini kwa shughuli za kikazi au kwa likizo. Hafaidi sana uwanja wa siasa wa nyumbani kama wanavyofaidi wanasiasa wenzake.

  Hivi kwa kujitangaza mapema si ameshajadiliwa na wapiga kura? Ametoa nafasi kwa wananchi kumchunguza tangu utotoni kwake hadi nafasi alipo sasa.

  Tayari wananchi wanajua uwezo wake. Wanajua uadilifu wake. Wanajua namna anavyoingiliana na watu wa nchini kwake na wa kimataifa. Watu wanamjua Balozi Karume kwa mbivu na mbichi kufikia sasa.

  Hivi yeye aliyejitangaza mapema na wale wana CCM kadhaa wanaotajwa tu katika vyombo vya habari kuwa watagombea urais, wakiwemo waliokana kutia nia hiyo wanapoulizwa na waandishi, yupi bora?

  Hiyo haitoshi. Balozi Karume anajulikana amekuwa kiongozi kwa muda mrefu sasa hivyo kuwa katika nafasi ya mtu kuweza kukadiria mapato yake.

  Sasa wale waliokaa kimya na wengine walioulizwa na kujibu kuwa “ingali mapema” lakini wamekuwa wakikusanya fedha hata nje ya nchi, nani ana afadhali hapa?

  Ukiacha Balozi Karume, orodha ya wenye shauku ya kutafuta urais kwa Zanzibar wanapata kumi. Wote hawajatangaza hadharani lakini harakati zao zinathibitisha wanaunyatia urais.

  Na ni hawa wanaofanya kampeni chafu zinazohusisha na mipango ovu ya kugawa wanachama wa CCM ili kutimiza dhamira zao za kutaka kiti cha Ikulu.

  Umma unashuhudia namna watu wenye shauku ya urais wanavyopita kwenye mikusanyiko na kugawa fedha bila ya kusema ni za nini.

  Zipo taarifa kwamba kuna makada wa CCM wamefika hadi Uarabuni kutembeza bakuli kwa wahisani wao ili kuja kuzitapanya kwa watu na kutumainia kuungwa mkono. Tayari wameanza kuzigawa kwa makada wenzao.

  Wapo baadhi ya makada wanaotafuta urais wanawatumia waandishi wa habari wenzangu kuwatajataja magazetini na katika televisheni ili kujikurubisha na wapiga kura.

  Makada walio mawaziri wanajiundia ziara kila siku za Pemba na wanalipa waandishi wa habari fedha mchezo tu kufuatana nao kwa ajili ya kuwapamba waonekane wanafanya kazi za wananchi.

  Ukweli ni kwamba makada wengi sasa wanazunguka nchi kujijenga kisiasa kwa ajili ya tamaa ya urais. Katika kujijenga huko wanadiriki kuchafua wenzao bila ya aibu.

  Kwa bahati mbaya sana, wanafanya hivyo kwa kutumia fedha za wananchi, magari ya serikali na muda waliopaswa kutumikia wananchi. Huku ni kutenda haramu, jambo lisilokubalika.

  Nilipomsikia Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha anasisitiza watu waache kufikiria urais, naye akigoma kutangaza kuwa anautaka urais, nilicheka. Lakini nilihuzunika kwa kuwa ninayoyasikia kumhusu yeye yanachefua.

  Makada wengi wa CCM wanaoutaka urais wanafanya kampeni za kibaguzi na kimajimbo na kupoteza raslimali za umma na hakuna anayegomba.

  Hata pale rais anapokemea mtindo huu hakuna anayejali. Wanaendelea huku wakisema, “Hana analo, anamaliza muda wake aondoke.”

  Makada wanaotajwa sana kuwania urais ni pamoja na Shamsi, mtangulizi wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Muhammed Seif Khatib, Haroun Ali Suleiman, Ali Juma Shamhuna na Dk. Hussein Mwinyi.

  Wananchi wawatie adabu makada wa aina hii. Wakatae kununuliwa kwa fedha au kwa kitu kingine chochote. Uadilifu wa kiongozi lazima utokane na historia yake ya utendaji na siyo uadilifu wa kutengeneza ukingoni kabla ya uchukuaji fomu za kuomba uteuzi kuanza.

  Zanzibar inahitaji kiongozi aliyetukuka. Awe mwema kwa maneno na vitendo. Atambuwe na kuthamini wajibu wake kwa atakaokuja kuwaongoza.

  Zanzibar inahitaji kiongozi mpenda nchi na watu wake; mwenye uchungu itokeapo shida; mshirika siyo mtenganishi; anayetoa uongozi unapotakiwa; anayefikiria maendeleo ya watu siyo ya familia yake na rafiki zake.

  Source :MWanahalisi by Jabir Idrisa.
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ali Karume ndie next prez visiwani, na ana sapoti kubwa toka CUF na CCM kwa ujumla... na haya maridhiano ndio yatampa kula kedekede!

  Kumbuka kuwa ndio mgombea pekee aliyesema kuwa yupo tayali kuunda serikali ya mseto iwapo atachaguliwa. Kauli ambayo iliungwa mkono na Maalim Seif!
   
 3. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mbona Aman Karume aliyepo anataka kuendelea? Huoni nia hiyo?
   
 4. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hili haupo sahihi kama ulimsikiliza wakati akitoa hotuba yake siku ya mapinduzi alisema awamu yake ya kuongoza Zanzibar iimekwisha. Sidhani kama kweli anataka kuendelea kuongoza Zanzibar otherwise avunje katiba. Na Wazanzibari hawamvumilia avunje katiba.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Wanataka aendelee, na ni kwa muda fulani pasipo kuwepo na uchaguzi... Nami nazungumzia rais atakaye kuja baada ya uchaguzi mkuu.
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mbona wewe unamtajataja Balozi Ali Karume gazetini ina maana unatumiwa na kada Ali Karume wewe leta sifa zake tuzijadili si kulaumu waandishi wenzako, unasema mnapoeleza huwa mmeangalia mbali na nani.........na huyo kada au....

  Halafu unasema bahati njema anaishi sana nje, mkuu.....sasa ni wakati gani huwa anaingiliana na wananchi wake au anapokuja mara chache chache, tujulishe.

  Mimi nafikiri kwa mgombea kiti cha urais kukaa nje sana siyo sifa wala bahati njema ni bahati mbaya kwa sababu muda mwingi hayuko karibu na wapiga kura wake.
   
 7. D

  Darwin JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  I guess hiki sio kiswahili cha Kizanzibari!!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,604
  Likes Received: 18,643
  Trophy Points: 280
  Ili balozi Karume aweze kugombea, na Wanzazibar wasione huu ni usultani wa familia ya kina Karume, itambidi Ali awanong'oneze Wazanzibari baadhi ya siri za nasaba ya Abed Amani Karume kwa kutumia DNA, ili aupate urais wa Zanzibar kwa sympathy vinginevyo hii ni zamu ya Seif.
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wewe wanena
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Tatizo lako ni nini?
   
 11. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2010
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 341
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35

  Yawezekana kibunango ni mzanzibara [​IMG]
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kuna sehemu nimesema ni mzenj?
   
 13. D

  Darwin JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  [​IMG] Kibunango[​IMG] [​IMG]
  Kibunango Mapinduzi Daima...!

  Wengi wa watanzania hapa ni HYPO!!!

  Usione kwamba kila mtu hana kumbukumbu, Ulikua unaizungumzia Zanzibar kama unatoka Michenzani vile kumbe unatoka Zanzibara.

  Nakushangaa sasa ukisema kwamba wewe sio mzenji.
  Wewe sio mmoja tu unayetembea na ngozi ya kondoo wakati wewe ni chui ili uwakamate kondoo.

  Yuko anayejiita Mwanakijiji ambaye mwaka 2005 alikua anampigia debe JK kule kwenye DHB kama nini.
  Nashangaa sasa yeye ndio yuko mstari wa mbele kumponda JK
   
 14. Ustaadh

  Ustaadh JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2010
  Joined: Oct 25, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pamoja na ukweli kuwa ana haki ya kugombea kama raia mwingine wa Zanzibar, tumechoka kusikia majina ya KARUME katika urais wa zanzibar. Vinginevyo inakuwa kama usultani hivi! Wengine nao wagombee isiwe kama ni cheo cha ukoo.
   
 15. MrFroasty

  MrFroasty JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 702
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Technically hiyo ni haki yake huyo Ali Karume kugombea urais wa Zanzibar au kupigana kikumbo na JK.

  Cha msingi mie huwa nasema demokrasia iachiwe ifanye kazi yake, wana CCM wakimtaka nawamueke tuu.Personally I have no problem as long as he is clean, which I doubt it on this case.

  Huyu bwana Ali Karume nasikia alishawahi kuwa na criminal charges za kumuuwa binti wa watu na kumtupa viwanjani maeneo ya Maisara.

  Sasa mtu akishakuwa na criminal charges, moja kwa moja hafai...sijuwi sheria kama zitaweza kussupport hii hoja au ndio zitapindishwa kwa ajili ni mtoto wa Karume :D
   
Loading...