Siri ya sifuri
JF-Expert Member
- Sep 21, 2018
- 2,580
- 2,224
Habari wakuu?
Katika harakati zangu zakutafuta maisha bora nikatua zangu mjini Zanzibar nikitokea mkoani Tanga, wilaya ya Pangani Magharibi, Mtaa wa Kongowea. Kyle Zanzibar makazi yangu yakawa mtaa wa Shaurimoyo mkabala na shule ya msingi, Katika kutafuta marafiki ndio nikakutana na wakazi wengi wa mkoa wa Tanga kutoka wilaya tofauti, nanilichofaham baadae ni kwamba, wenyeji wengi wa mkoa wa Tanga wanaoishi Zanzibar ni mafundi ujenzi. kuna waliohamia kabisa na kuna wanaokwenda kufanyakazi na kurudi, niseme ni kambi.
Nilikua na kawaida ikitokea MTU wa Tanga amkuwa na shughuli kama harusi au msiba naenda kujumuika nae, kuna utaratibu ulionivutia kwenye harusi nao ni huu"Mkienda kuposa huwa mnaandaliwa CHAKULA cha wote ila bwana harusi anaandaliwa cha kwake peke yake, anawekewa samaki kwenye kisahani, wakati wote wa mlo huwa ndugu wa mke au baba mkwe wake kama yupo wanamfuatilia jinsi anavyomla yule Samaki, wajua kwanini!?
Hawataki amgeuze, wanachotaka wao kuona ukimaliza upande mmoja unaondoa mwiba ambao ndio uti wa mgongo wa samaki unaotenganisha upande mmoja na mwingine kisha ndio umalizie kula upande wa pili, ikitokea umemgeuza basi itakua ndio umejinyima mke wewe mwenyewe, wanasema huna maadili hufai hata kidogo kumuoa binti yao, eti utaenda kumgeuza" utamlakotekote"basi hata kama ulikuja kutoa mahari utarudi nayo, hawaipokei na ikitokea umeoa mke thamani zote ndani yanyumba ni Mali ya Mwanamke, siku mkiachana anabeba kila kitu anaacha nyumba nyeupe, kwa maana kwamba mwengine utakae kwenda kumuoa atakuja navyake, na ikitokea umekamatiwa na binti"msichana"basi kutawekwa mkataba mahakamani na hutaweza kumuacha chini yakipindi cha miaka 5 na ukikaidi unakamatwa na kufungwa.
Hiyo ndiyo Zanzibar bwana