aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 835
- 1,215
Nasema Zanzibar pamoja na udogo wake wa uchache wa watu wake, Zanzibar ina jina kubwa duniani linalotokana na historia yake pamoja na makali ya historia yake, hatutakiwi kusahau historia hiyo.
Visiwa vya Unguja na Pemba vinayo sifa ya kuwa lango kuu la kuingilia Afrika Mashariki kwa wageni wote waliotoka Mashariki na Kaskazini mwa sayari yetu hii.
Kutokana na ukweli huo, Zanzibar imekuwa na sifa ya kuwa "Blenda" ya KUCHANGANYA Mataifa, makabila, rangi, imani, tanaduni, nitazamo na Jamala za kila aina za watu kutoka nchi Karibu zote za dunia hii.
Waarabu, Waajemi, Wachina, Wahindi, Wareno, Wanyakyusa, Wanyasa, na Wamanyema kila aina ya binadamu amechangia damu yake katika Visiwa hivi. Kwa watu wenye busara na wastaarabu, huu ni urithi mkubwa kwa jamii yeyote.
Mchanganyiko wa aina hii ni hazina kwani unarutubisha nchi, unaipa nguvu ya vipaji mchanganyiko, unaifanya iwe ni "Microcosm" ya dunia. Kwa namna tofauti ndivyo nguvu za nchi kama Cuba na Marekani zilivyojenga nguvu zake katika medani kadha.
Lakini jamii ya wajinga huona tofauti baina ya watu kama tangazo la vita na watu walio tafauti ni maaduwi. Watu wa kumalizwa kwa kila njia. Kutokana na itikadi hii ya kumuona mtu yeyote alietofauti kama tishio badala ya kuwa kivutio. Na haya ndio mawazo ya viongozi wetu wengi hapa visiwani Hivi Sasa Zanzibar imekuwa na jina kubwa katika anga za utalii duniani.
Watu wengi huja Zanzibar kuona jinsi makabila ya dunia na dini tofauti Zinavyoishi kwa pamoja kwa Amani, raha mustarehe.