Zanzibar: Mhadhiri SUZA atiwa mbaroni

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Saleh Mohammed Saleh, anashikiliwa na polisi mjini Zanzibar kwa madai ya kuhusika kulipua nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame.

Mhadhiri huyo ambaye ni Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF)Zoni ya Magharibi A Unguja na aliyekuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Welezo, alikamatwa na saa nane za usiku wa kuamkia jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu,Habari na Uenezi, Pavu Juma Abdalla alisema polisi walivamia nyumbani kwa mhadhiri huyo na kuvunja mlango.

Alisema kiongozi mwingine aliyekamatwa ni Mwenyekiti wa chama hicho Zoni ya Mfenesini, Omar Hassan Issa.

Alisema kutokana na hali hiyo, jana kutwa nzima walizunguka vituo vingi ya polisi lakini hawakuwaona.

“Polisi walivamia nyumbani kwao saa nane usiku, wakavunja milango na kuwapiga na kuondoa nao.

“Tumewatafuta vituoni hatukuwaona,tumeambiwa ni miongoni mwa watu wanaoshutumiwa kwa kulipua nyumba ya Kamishna Hamdani,” alisema Pavu.

Alisema CUF wanaendelea na jitihada za kuwatafuta viongozi hao waweze kujua hatima yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alikiri kushikiliwa kwa viongozi hao.

Alisema hakuwa tayari kutaja majina ya watu wengine waliowakamatwa akisema wanaendelea na upelelezi.

“Bado tunaendelea na upelelezi, tukiwa tayari tutatoa kila kitu, kwa sasa hatuko tayari kuwataja majina yao,” alisema Kamanda Mkadam.

Alisema polisi wanaendelea na msako mkali dhidi ya watu wote wanaotuhumiwa kuhusika na ulipuaji wa nyumba hiyo.

“Kutokana na uchunguzi wetu tuliofanya, tunayo orodha ya washukiwa wote na tutaendelea kuwakamata na ikithibitika tutawachukulia hatua,” aliongeza.

Chanzo: Mtanzania
 
wewe polisi babayako anapuliza moto kwa mdomo huku kijijini babu yako pia hiyo petroli mliyowasha mtaweza kuizima?huyu babu na bibi yako mnafikiri wanaweza kukimbia ?je na huyu mchepuko wako
 
Kwahiyo mkuu waachwe tu hata kama ni kweli wanahusika kwasababu bibi yake hawezi kukimbia??
 
12049648_1152951574714977_5981441728498050725_n.jpg

MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) AKAMATWA NA POLISI AKIHUSISHWA NA ULIPUAJI NYUMBA YA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR.

MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), Saleh Mohammed Saleh, anashikiliwa na polisi mjini Zanzibar kwa madai ya kuhusika kulipua nyumba ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame.

Mhadhiri huyo ambaye ni Katibu wa Chama cha Wananchi (CUF)Zoni ya Magharibi A Unguja na aliyekuwa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Welezo, alikamatwa na... saa nane za usiku wa kumkia jana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu,Habari na Uenezi, Pavu Juma Abdalla alisema polisi walivamia nyumbani kwa mhadhiri huyo na kuvunja mlango.

Alisema kiongozi mwingine aliyekamatwa ni Mwenyekiti wa chama hicho Zoni ya Mfenesini, Omar Hassan Issa.

Alisema kutokana na hali hiyo, jana kutwa nzima walizunguka vituo vingi ya polisi lakini hawakuwaona.

“Polisi walivamia nyumbani kwao saa nane usiku, wakavunja milango na kuwapiga na kuondoa nao.

“Tumewatafuta vituoni hatukuwaona,tumeambiwa ni miongoni mwa watu wanaoshutumiwa kwa kulipua nyumba ya Kamishna Hamdani,” alisema Pavu.
Alisema CUF wanaendelea na jitihada za kuwatafuta viongozi hao waweze kujua hatima yao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alikiri kushikiliwa kwa viongozi hao.

Alisema hakuwa tayari kutaja majina ya watu wengine waliowakamatwa akisema wanaendelea na upelelezi.

“Bado tunaendelea na upelelezi, tukiwa tayari tutatoa kila kitu, kwa sasa hatuko tayari kuwataja majina yao,” alisema Kamanda Mkadam.

Alisema polisi wanaendelea na msako mkali dhidi ya watu wote wanaotuhumiwa kuhusika na ulipuaji wa nyumba hiyo.

“Kutokana na uchunguzi wetu tuliofanya, tunayo orodha ya washukiwa wote na tutaendelea kuwakamata na ikithibitika tutawachukulia hatua,” aliongeza.

Chanzo : Mtanzania
 
Dah! Tunaomba Ndugu zetu wazanzibar mtumie njia nzuri ili msijenge chuki na raia kwa kuona mnafanya uonevu, kama ni kweli mnawachukua kwa kuwapiga kama hii habari ilivyoeleza mtaonekana mnafanya uonevu au kukiuka haki za kibinadamu, kama ni kweli wamehusika basi wachukuliwe hatua ila hakikisheni hili zoezi halileti sura ya uonevu, ukizingatia juzi tu tumetoka kwenye uchaguzi na baadhi ya wanachi wameonyesha kutoridhishwa, Mungu ibariki Zanzibar, Tanganyika na Tanzania kwa Ujumla, Ameen.
 
Kwa maneno ya Kamanda, uchunguzi ushafanywa, ithibitike nini tena na uchunguzi mushafanya? Wapelekeni mahakamani muwashitaki tu, hao criminals
 
Kama ni kweli wamefanya hivyo kulipua nyumba washitakiwe na wanyongwe maana ni magaidi
 
CUF ni tawi la Al shabab...ikithibitika ni kweli basi wanyongwe tu maana hakuna namna sasa
 
Ikidhibitishwa na nani wakati wewe umesha kiri.. Kwanini usiende kutoa ushaidi
Viongozi wote wa Uamshio ni CUF...Na uamsho ni tawi la Alshababy..therefore CUF ni tawi la Alshababy..hiyo ndio logic..Ikithibitika kwamba huyo jamaa ni kweli anyongwe tu..
 
Polisi wa Zanzibar ni lipi walilolifanyia uchunguzi wakafanikiwa?
Si padri kuuwawa,mwengine kujeruhiwa na risasi,wasichana wazungu na Mashehe kumwagiwa tindikali,hakuna lolote la maana
kazi yao kutumika kisiasa
Marekani wanaitwa Keystone Cops yaani polisi ambao wapo wapo tuu
 
Back
Top Bottom