KAMATI YA MARIDHIANO SIX: MKUTANO WA CCM ULIOFANYIKA TAREHE 04/11/2012 (HIGHLIGHT 2) - YouTube
WWW-you tube.com/watch?v=_G6l9uJ8uoI&feature=player_embedded
Hakuna shaka kuwa hawa wahuni wanapata baraka zote kutoka kwa Mwenyekiti wa chama chao Rais Jakaya Mrisha Kikwete na Makamo Mwenyekiti na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mh Ali Mohammed Shein.
Kama kweli hawa watu nilio wataja na vyeo vyao vikubwa wangekuwa niwaungwana na viongozi wenye maadili na utamaduni mzuri na mila za Kizanzibar na Tanzania kwa ujumla basi wasingali subutu kuwaruhusu wahuni hawa wasiokuwa na Heshma na maledhi mazuri kutukana watu na kuwakashifu watu wenye hishima kubwa katika jamii yetu ya wazanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Katika Baradha Tukufu la Iddi Lililosaliwa Zanzibar hivi juzi na hutuba kali ya Rais wa Serekali ya Mapinduzi ya watu wa Zanzibar Alhaji Mohammed Shein, alikemea vikali kuhusu mtu yoyote atakae sababisha kuvunjika kwa hali ya amani na utulivu ulokuwepo hivi sasa chini ya serekali ya Umoja wa Kitaifa.
Mh Shein alisema hato mruhusu mtu yoyote au kikundi chochote chenye kusababicha fujo,juki na fitna ili hali ilokuwepo kutoweka, alisema amani na utulivu ulopo umeharimu samani kubwa ya Wazanzibar na Tanzania kwa ujumla, kwa hio atawachukulia hatuwa kali wale wenye kusababicha fujo na mwisho akamaliza kusema uvumilivu umekwisha.
a).Sasa tumulize Mh Rais hawa wanachokifanya kinaashiria nini katika Amani ya nchi yako?
b). Jee Mh Rais hawa wafuasi wa Chama chako ukiwa wewe ndio kiongozi chama chao na Rais wa nchi hii umewapa lesen ili watukane watu wenye hishima hazarani matusi ya laana ?
Nchi unaipeleka wapi cheni katika Style hii? au hujuwi kuwa mchunga ataulizwa kwa alicho kichunga? hujuwi kuwa una zima mbele ya Allah?.
Nchi unainakamiza Mh na wewe ndio kiongozi wa nchi na utasailiwa na M/mungu kutokana na uongozi wako na umekubali kuwa kiongozi basi usisahau kuwa umekuwa na hivi sasa zamana na zima ya wananchi wa Zanzibar iko katika mikono yako , uwe ccm ,uwe cuf ,uwe huna chama lakini madamu ni kiongozi wa nchi basi watu wote wenye vyama na wasio na vyama walio kuchaguwa na wasio ni watu wako na ilitakikana usi baguwe kutokana na itikadi za vyama.
Jee Mh Nchi unaipeleka wapi, jee hizi ni siasa au chuki na matukano ya vijana wako?
Umekemea Kuuliwa kwa askari koplo na kuchomwa moto kwa maskani Mama Kisonge, jee kwa nini hukufanya haki kwa raia wako walouliwa kwa kupigwa risasi na wafuasi wako wa Jeshi la Polisi akiwemo mtoto wa miaka 14 alokuwa anatamani kuvuta hewa na kupata fadhila kutoka kwa Mola wake Allah kama vile Allah anapo kupa fadhila zake za kuvuta punzi yake na kutowa pasipo hata kulipa Kodi ?.
Jee Shein Nchi unaipeleka wapi?
Mungu ibariki Zanzibar na watu wake na utulinde na wenye zamira mbaya katika nafsi zao.