Zanzibar kuwa na serikali ya mseto? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar kuwa na serikali ya mseto?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Vakwavwe, Sep 25, 2009.

 1. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2009
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  wana jamvi mimi ni mchanga kwenye siasa ila najaribu kufuatilia kwa karibu yanayojiri kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi....
  kwenye taarifa ya habari ya saa2 usiku TBC1 mzee Msekwa alikuwa akihojiwa kuhusu hali ya Zanzibar. katika majibu/maelezo yake amesema wao kama chama wanafikiria uwezekano wa kutawala kwa mseto Zanzibar kwa maana ya kuwashirikisha CUF. ameanzia uchaguzi wa 1995,2000 na hata 2005 kuwa mshindi alizidi kwa tofauti ndogo sana na kuwaacha nje ya serikali watu waliopata kuungwa mkono na wapiga kura wengi kiasi hiki sio haki sana though ndio utaratibu tulionao. kwa watu kama Msekwa kusema wanafikiria i guess ndo wanshaamua hivyo!!angekuwa mwanaCCM mwingine ningehisi kuwa ni mawazo binafsi lakini siyo kutoka kwa makamu mwenyekiti wa CCM.
  tetesi zingine nilizopata nje ya mahojiano ya Msekwa ni kwamba mkulu wa Zanzibar haafiki ktk hili ndo sababu hata mikutano kadhaa hajahudhuria akitoa visingizio kadhaa......
  Naamini kuna mengi watu wanayajua kuhusu hili naombeni mtupe kwa ukamili jamani....
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuhusu serikali ya mseto hiyo imeongelewa sana hata miaka ya nyuma lakini mpaka leo hakuna kitu kama hicho. So hi nayo inaweza ikawa paying lip service tu. Lakini hata wakiweka serikali ya mseto ni lazima ujiulize hao wengine watapewa nafasi zipi serikalini? Na ratio ya kila chama serikalini itakuaje?
   
 3. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280
  Serikali ya malaghai yenye uchu ya CCM hawawezi kukubali serikali ya umoja;wao wanataka watawale pekee yao milele!
   
 4. C

  Calipso JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 284
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hawa ccm waliwahi kusema mchele na kokoto haziendani kwa hiyo hakuna mseto wala nini.. lkn baada ya kupigwa bao na Cuf inaonekana wanajaribu njia za kuwashawishi Cuf warudi mezani.. mimi naona hakuna mseto hawa ni kuwaondoa tu kwa Mapinduzi kama wao wanavosema kuwa Serikali haitoki kwa karatasi.
   
 5. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Dear Nd.Vakwavwe,

  >na kuwaacha nje ya serikali watu waliopata kuungwa mkono na wapiga kura wengi kiasi hiki sio haki sana though ndio utaratibu tulionao.>


  I say, hapo umenifurahisha sana, kwani inaonesha kuwa wewe unaijua historia ya upigaji kura kule ZNZ. Hio kuwaacha nje wale walioungwa mkono na wapiga kura wengi ndio kweli utaratibu walionao ZNZ tokea zama za zama na sio utaratibu mzuri - hasa kwa sisi tunaopenda demokrasia ya kweli. Inaonesha Waznz wameirithi tabia hii kutoka kwa mababu na mabibi zao, kwani tokea huko nyuma kabla ya Mapinduzi mambo ndio yalikuwa hivyo hivyo.
  Kabla ya Mapinduzi ilikuwa siku zote wale waliokuwa wakiungwa mkono na wapiga kura wengi walikuwa wakiachwa nje ya serikali mpaka hapo tarehe 12 January, 1964 ilipofika ndio wakaamua kutumia misuli yao. Kama sio hivyo mpaka leo wangelikuwa nje ya serikali japokuwa wao walikuwa wakiungwa mkono na wapiga kura wengi!
  Jamani, ndugu zangu Waznz, tafadhalini acheni tabia hii mbaya mlioirithi toka siku za ukoloni wa kisultani!
  Acheni tabia hii ya mababu na mabibi zenu, kwani wakati sasa ni mwengine!
   
 6. Makalangilo

  Makalangilo Senior Member

  #6
  Sep 26, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali ya mseto haitawezekana Zanzibar kwa sababu utashi ndania ya Kamti Kuu ya CCM haupo.

  CCM ikikubali Serikali ya mseto itakuwa itakuwa inakubali ushauri,matakwa na maelekezo ya Hayati Mwalimu JK Nyerere.

  Mimi sitaona tofauti yoyote katika sual la Uchaguzi huko Zenji.Nasubiri kuona wananchi wanapata mkong'oto na magari ya deraya mitaani ilikusaidia CCM ifanye ufisadi wa kisiasa ili ku-sustain status quo.
   
 7. L

  Lampart Senior Member

  #7
  Sep 26, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hi Ngida,
  >Jamani, ndugu zangu Waznz, tafadhalini acheni tabia hii mbaya mlioirithi toka siku za ukoloni wa kisultani!
  Acheni tabia hii ya mababu na mabibi zenu, kwani wakati sasa ni mwengine!
  >
  Hii tabia wewe mwenyewe umeandika kuwa tokea kabla ya Mapinduzi ilikuwepo sasa leo na sisi tukiiendeleza kunaubaya gani wakati tumeirithi tokea huko nyuma?
  Au umesahau nani alipata kura nyingi katika chaguzi za 1961 na 1963 na nani alipewa serikali?
  Au mkuki kwa nguruwe kwa binaadamu mchungu?

  Ngida, what is good for the goose is good for the gander!Kwahivyo, tuachie tuendelee na tabia yetu hio tulioirithi kutoka kwa Sultani wetu na wakoloni wenziwe!
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  kiongozi upo?ulipotea sana au kwa sababu ya mfungo
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CUF haihitaji serikali ya mseto wala pure(mahindi na maharage) ,kinachohitajiwa ni uchaguzi wa haki tu, anachoongelea Msekwa ni ushindi wa wizi chini ya uchaguzi uliojaa mizengwe ,sasa ulingano wa serikali ya mchanganyiko inatokana na uchaguzi uliokwenda sawa kihaki katika sehemu zote tokea uandikishaji hadi upigaji kura ukifuatiwa na matangazo yaliosawia bila ya kubadilishwa ,sasa hapo ikiwa pana tofauti ya asilimia ya 0.1 ndio unaweza kuitisha huo mkorogo , lakini uchaguzi mzima ni wizi mtupu alafu mnajidai kutaka machanganyo ya serikali ,hivi hawa jamaa wana akili au ndio wameshaona kuwa CCM inazama na wanatafuta njia za kuwemo serikalini ?

  Wananchi ndio waachiwe kwa uhuru kabisa wachague Chama wakitakacho ,hapahitajiki polisi wala majeshi na maji ya washawasha kutafuta uongozi.
  Vyombo vya dola vikae pembeni na kuangalia kuwa haki inafuatwa na pande zote ,wasiwe wanatumika na kutumiliwa na CCM ,vyombo hivi vikae na kuona hakuna anaevunja sheria ,sio CCM wala vingine vinakuwa juu ya sheria ,halafu tuone nani ataibuka na uongozi wa nchi hii.
   
 10. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45

  Nd. Lampart,

  Sasa inamaana kabla ya Mapinduzi ASP walikuwa wakipata kura nyingi na still serikali wakipewa ZNP? Kutokana na hali hii unataka kwa sasa japokuwa CUF inapata kura nyingi lakini still serikali wapewe CCM?
  Nd. Lampart, what is this called? New wave of democracy in the Isles?
  Tafadhali tuwekee wazi, kwani in 1964 some of us were still in diapers!
   
 11. L

  Lampart Senior Member

  #11
  Sep 27, 2009
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngida,
  Naona umenipatapata japokuwa kwa pembeni.
  Lakini comparison yako naona haielekei, kwani japokuwa ASP ndio CCM, lakini ZNP sio CUF. Au nimekosea?
  >Nd. Lampart, what is this called?
  This is called HISTORY REPEATS ITSELF!
  ASP ikipata kura nyingi lakini haikuwa ikipewa serikali, na kwahivyo sasa waache CUF wapate kura nyingi lakini serikali wataiona paa tu!!!
  Our history just repeats itself over and over, again and again na CUF walie tu kama tulivyokuwa tukilia sisi siku zile za Sultani!!!
  It took us more than 200 years of slavery and sufferings to come up with the revolution, na kwahivyo CUF/ZNP watuachie tupoe kwanza na madaraka yetu tuliyoyapata tarehe 12 January, 1964!!!
   
 12. A

  Atanaye Senior Member

  #12
  Sep 27, 2009
  Joined: Oct 31, 2007
  Messages: 153
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ..sababu zipo wakuu
  ..kuna uwezekano wakufanya hili bila kuhudhuria katiba?

  ..halafu nasikia waZanzibari ni wataalam wa mseto(chakula)Wink!
   
 13. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  hiyo ni dhahiri kuwa ccm walikuwa wanaiba kura kwa upande wa zanzibar na 2010 naona hawataki tena dhambi hii ya wizi wanachofanya wanajiandaa kuweka utaratibu utakaowashirikisha kuunda serikali itakayoongozwa na upinzani
   
 14. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi wewe hujui CUF ndio wanaoiba kura huko Pemba. Angalia nini wanakifanya sasa huko Pemba. Mseto sio tatizo. Wa-zenj ni kweli wataalamu wa Mseto. Lakini mseto huo usiwe ni agenda ya kumrudisha Seif madarakani (hebu na akae chonjo apumzike-kwani CUF hawana wengine wanaofaa?). Kama ni hivyo abadan-asilan!!!!!
   
 15. H

  HAJI NYONJE New Member

  #15
  Sep 27, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo imezungumzwa sana lakini kimantiki ya kisiasa na historia yetu haijafanyika na sio leo tu tangu ezi hizo za waarabu mbona hawakuyafanya hayo. Usiseme wapizani kupewa madaraka ya chini hiyo ipo maana mawizarani mwetu wamo wa upande wa upizani na tunaenda nao pamoja na tuna wafahamu vizuri tu, ila hii ya mseto hiyo anasema kama yeye msekwa tu. Watafute yao
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wewe hufai hata kuwepo katika jamii ya binadamu ni RACIST ,halafu mna kitu mnakiogopa si bure ,ila mjue na kutambua mnachokiogopa kwa Seif kinaweza kutekelezwa na mtu yeyote yule ,na kitawaumiza vibaya sana pengine zaidi ya vile mnavyofikiria kutoka kwa Seif ,Seif aliitwa na Nyerere Butiama na Nyerere alitambua kuwa Seif ni kiongozi shujaa ,na Nyerere alimuomba Seif kitu ,hebu yatafute mazungumzo ya Seif na Nyerere ,uone baba yenu wa Taifa alivyomwamini Seif.
   
 17. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nipo mkuu. Si unajua Jamiiforums kubwa? Nilikuwa naexplore majukwa mengine kidogo.
   
 18. Bikirembwe

  Bikirembwe JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 250
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  "It took us more than 200 years of slavery and sufferings to come up with the revolution, na kwahivyo CUF/ZNP watuachie tupoe kwanza na madaraka yetu tuliyoyapata tarehe 12 January, 1964!!![/QUOTE]"

  Tutaendeleza chuki na visasi hadi lini? Nina wasiwasi kama muandishi anaitakia mema Zanzibar na TZ kwa jumla
   
  Last edited: Sep 28, 2009
 19. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  "

  Tutaendeleza chuki na visasi hadi lini? Nina wasiwasi kama muandishi anaitakia mema Zanzibar na TZ kwa jumla[/QUOTE]

  There were no slavery in Zanzibar but the slave market. Slaves were brought to Zanzibar from outside as merchandise for sell, even Zanzibaris themselves were allowed to purchase for their domestic use and cultivations of their cloves and coconut farms. If you don't know the history of Zanzibar please say so but do not distort The History.
   
 20. Freddy81

  Freddy81 Member

  #20
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 99
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ccm waongo tena muongo mkubwa huyo. Siku zote walikuwa hawalijui hilo?
   
Loading...