Zanzibar kupiga marufuku shisha na sigara za kielektroniki

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,114
1687441501304.png

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepanga kupiga marufuku uagizaji na utumiaji wa Shisha na E-sigara ikidai kuwa inatumika hovyo katika maeneo mbalimbali ya umma.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa Zanzibar, Masoud Ali Mohammed amesema serikali itatoa agizo maalum hivi karibuni.

“Sote ni mashahidi, unywaji wa Shisha na E-sigara umekuwa jambo la kawaida, na tutakuja na sheria maalum ya udhibiti ili kuwasimamia wale ambao watakuwa na vibali maalum vya kuagiza na kuuza shisha au sigara hizo,” amesema Masoud.

Aidha, Waziri Masoud amewataka waagizaji wa bidhaa hizo kusitisha kuagiza bidhaa kwani watalazimika kufuata sheria mpya ambayo serikali itatoa.

Kwa mujibu wa ripoti ya The Citizen, baadhi ya wafanyabiashara wa mahoteli Zanzibar wamedai shisha ni maarufu sana katika hoteli za kitalii na migahawa, hivyo kupigwa marufuku kwa bidhaa hiyo kunaweza kusababisha hasara kubwa katika upande wa mapato.

Pia soma:

Mkuu wa Wilaya Unguja avamia shuleni kusaka simu na shisha kwa wanafunzi

Marufuku nyingine Zanzibar soma:

Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika
 
walitakiwa kwanza wamalizane na wapiga kabari mitaani. CCM always wanashindwa ku focus na mambo muhimu.
 
Back
Top Bottom