Zanzibar kupata umeme Februari 20 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar kupata umeme Februari 20

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 8, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,587
  Likes Received: 5,773
  Trophy Points: 280
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetangaza kuwa huduma ya umeme wa gridi ya Taifa uliokosekana kisiwani humu tangu Desemba 10, mwaka jana, itarejea Februari 20, mwaka huu.

  Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi (MUNA), Mansoor Yussuf Himid amesema leo kuwa hali hiyo ni matokeo ya kuamuliwa kufanya matengenezo makubwa ya waya wa chini ya bahari kutoka Ras Kiromoni hadi Fumba Mjini Unguja.

  Himid amewaeleza waandishi wa habari kuwa, wataalam watabadilisha uendeshaji waya huo na kuufanya usiofanana na ule wa awali pamoja na vifaa vya uhifadhi wa mafuta na badala yake waya zitabaki zikiwa pekee.

  Amesema, ratiba hiyo inahusisha ununuzi wa vifaa, uunganishaji wa vipuri, matayarisho ya waya wenyewe viungio vyake kufanya majaribio ya waya pamoja na kuwasha Februari 20, mwaka huu.

  Alisema sehemu kubwa ya baadhi ya vifa vilivyoharibika kwenye waya huo matengenezo yake yanaendelea katika vituo vya Ras Kiromoni Dar es Salaam na Ras Fumba Zanzibar.

  Kwa mujibu wa Himid, baada matengenezo hayo majaribio ya kwanza katika 'cable' yanatarajiwa kufanyika kuanzia Febuari 18, mwaka huu na yatachukua siku mbili.

  Amesema, serikali imefanya mabadiliko ya mfumo mzima wa matumizi ya waya huo ikiwemo kubadili vifaa vyote vya kupokelea umeme katika vituo vya Fumba na Ras Kiromoni.

  Kiongozi huyo wa SMZ amesema, marekebisho hayo makubwa ni moja ya sehemu ambayo itasababisha kuchukua muda huo kutokana na wataalamu watayoifanya kazi hiyo kushauri kutumika siku 10 kwa kila hatua ya uwekaji wa kifaa kimoja.

  Waziri Himid alisema baadhi ya vifaa vitaanza kufikishwa nchini leo kutoka Afrika Kusini na kwamba, wataalamu wameanza kazi za kupima mafuta yaliomo katika waya wa Fumba.

  Himid amesema,wataalamu kutoka Kampuni ya Erickson ya Sweden ndio ndio watakaofanya kazi ya matengenezo makubwa ya waya huo wa chini ya bahari ambao ulitengenezwa miaka ya mwanzoni mwa 1980.

  Awali, wataalamu hao walipanga siku 15 kwa kila hatua kukamilisha kazi, lakini wameombwa kuangalia uwezekano na kurudisha siku na wakakubali kupunguza hadi kufikia siku 10 za kazi kwa hatua.

  Katika hatua nyingine, Waziri Himid alisema kwa kuwa wananchi hawapati huduma ya umeme, amefuta ada ya malipo ya huduma hiyo kwa wananchi hadi hapo hali ya umeme itakaporejea katika hali ya kawaida Zanzibar.
   
 2. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2010
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hivi hadi tatizo limekuwa kubwa hivi serikali ilikuwa wapi muda wote??? Je tathmini ya athari ya jambo hili kiuchumi likoje maana navyojua mimi umeme ni sehemu muhimu sana ya uchumi wa zanzibar hasa kutokana na uwepo wa biashara ya utalii.

  Walahi huu ni uzembe wa hali ya juu na waziri husika alipaswa awe ameshaachia ngazi kitambo.
   
 3. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  DUH!
  ni siku sita tu baada ya harusi yangu.ngoja niangalie honeymoon ifanyike wapi
   
Loading...