Sr. Magdalena
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 803
- 472
Wakuu heshima mbele sana,
Kumekuwa na sintofahamu nyingi sana mara baada ya Serikali kwa bahati mbaya au makusudi kugawa fedha ya change ya Rada Tanzania bara pekee na Tanzania visiwani kutokupata hata centi moja, Wabunge wengi wa Zanzibar wameonekana kutokupendezwa na swala hili, Je ni sahihi kwa mgawo wa Rada kugawanywa bara pekee na si visiwani..?
Ni sahihi kwa kuwa rada haikuwa ya muungano.
Change ya Rada si suala la muungano.
Kaka Ngongo na Mangaline heshima zenu sana.
Naona umejibu kwa kifupi sana, unamaanisha nini unaposema Rada si suala la muungano, ninavyofahamu mimi ni kuwa ulinzi na usalama ni suala la muungano, correct me if im wrong.
Sr. Magdalena
Kumbu kumbu zangu kama hazijachoka zinaniambia rada ililetwa kwaajili kuimarisha usafiri wa anga [ndege za kiraia] ingawa ingeweza kutumiwa katika masuala ya ulinzi.Mawasiliano si miongoni mwa masuala ya muungano ndiyo maana unasikia Zanzibar wametoa kibali meli za mafuta za Iran kutumia bendera ya Tanzania.
Kaka Ngongo na Mangaline heshima zenu sana.
Naona umejibu kwa kifupi sana, unamaanisha nini unaposema Rada si suala la muungano, ninavyofahamu mimi ni kuwa ulinzi na usalama ni suala la muungano, correct me if im wrong.
Sr.Magdalena,
..Ulinzi ni suala la muungano, lakini kwa kawaida ZNZ huwa haichangii chochote ktk masuala ya muungano.
..kabla ya kulalamika, wabunge wa ZNZ wangeeleza wakati rada inanunuliwa ZNZ walitoa kiasi gani toka hazina yao. inajulikana kwamba makusanyo yote ya TRA Zanzibar hubakia hukohuko.
..mbona hatujasikia ZNZ wakililia kushirikishwa ktk kulipa madeni ya nje, kila siku ni kelele za kudai misaada na mgao??
..LET ZANZIBAR GO!!!

Zanzibar si nchi nje ya mipaka yetu. Hivyo wamarekani hawawezi kui-address barua yao kwa Shein (mkuu wa mkoa wa zanzibar), bali kwa rais wa Tanzania JKNimekuelewa kaka, nilidhani ilikuwa ni kwa ajili ya ulinzi na usalama, lakini kama iko Mawasiliano si muungano.
Hapa kwenye nyekundu naona umechomekea, wa amerikani na waingereza wamechukizwa sana na hii kitu, hope JK atawaelewesha na watamwelewa kuwa ile barua iliyokua addressed magogoni imekosewa inabidi wa TRY Zanziba kwa Mr. Shein.
JokaKuu, Hi!
Hapa ndipo watu wengi huchanganyikiwa, kwani mfuko mkuu wa serikali ya Jamhuri ya Muungano na mgawanyo wake wa fedha kwa serikali hizi mbili umekaaje?..na kuna uhusiano gani kati ya wizara ya fedha Bara na Visiwani, na Je wabunge kutoka Zanzibar wana maeneo maalumu ya kuchangia kwenye bunge la bajeti au wanachangia kila wizara?..