Zanzibar kumekucha ya 95 yajirejea watafika ?: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar kumekucha ya 95 yajirejea watafika ?:

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtu wa Pwani, Feb 22, 2009.

 1. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  KUMEKUCHA KARIBU UCHAGUZI WA 2010 UKO MLANGONI NA YALE YALIOZOELEKA KUTOKEA YAMEANZA

  SASA TUSEMEJE NA TUFANYEJE ?
  Nyumba 600 zabomolewa Zanzibar,Cuf yalaani Na Salim Said

  SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) jana iliendesha bomoabomoa inayodaiwa kuwa mbaya katika maeneo ya shehia(kata) za Tomondo na Kisauni ambapo zaidi ya nyumba 600 zilibomoloewa na kuharibu misingi 250 wilaya ya Magharibi .


  Watu walioshuhudia matukio hayo walisema yalifanyika kwa kushtukiza, bila notisi na kuendeshwa chini ya ulinzi wa Polisi wa kutuliza ghasia (FFU), Mkuu wa Mkoa huo, Mkuu wa Wilaya, Masheha na baadhi ya Maafisa wa usalama.


  Shuhuda na mwathirika Khamis Ramadhan Juma, ambaye kwa kushirikiana na wanakijiji wenzake waliendesha tathmini ya kuhesabu nyumba zilizobomolewa na kugundua kuwa nyumba 600 na fondesheni 250 zilikwishabomolewa hadi kufikia saa 10:00 jioni ya jana huku zoezi likiendelea. Sheha wa Shehia ya Tomondo jimbo la Dimani, Mohammed Ali Kidevu, alipoulizwa juu ya suala hilo jana , alisema kazi hiyo inafanyika kwa amri ya Mkuu wa mkoa na kwamba yeye asingeweza kuzungumza.


  “Sikusikii vizuri nipo kazini, unalisikia Burdoza (Tingatinga) hilo linafanya kazi na mimi natakiwa kusimamia, mpigie mkuu wa mkoa huyu ndiye mwenyewe” alisema Kidevu.


  Kwa mujibu wa baadhi ya waathirika, hatua hiyo inchukuliwa kwa madai kuwa walivamia maeneo yasiyoruhusiwa na serikali kujengwa yakiwemo ya viwanja vya shule.


  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi alisema, ana taarifa za kuendeshwa kwa zoezi hilo na kuthibitisha kuwa linasimamiwa na polisi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mjini magharibi .


  “Mimi sipo katika eneo la tukio ila mpigie mkuu wa mkoa amenipigia muda si mrefu akiwa katika eneo la tukio anasimamia zoezi hilo” alisema.


  Aidha alipogiwa simu Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi alijigamba kuwa ni kweli anasimamia lakini alikataa kueleza sababu za kubomoa bila ya kutoa notisi kwa wananchi.


  “Wewe panda ndege tu, uje uchukue habari, kila baada ya dakika 10 ndege zinatua pale uwanja wa ndege, mnakaa juu ya meza mnapiga simu kuandika uongo na kula fedha bure tu. Njoo huku kama unahitaji habari” alidai.


  Ali Ali Yussuf, ambaye ni muathirika wa tukio hilo, alisema SMZ imekusudia kuwadhalilisha kwa kuwa wao hawana nguvu ya kupambana.


  “Tuliwekewa X jana (juzi) jioni na sheha wa shehia yetu, na leo limekuja tingatinga

  kubomoa, lakini wamebomoa hata zilizokuwa hazijawekewa X” alilalamika Yussuf na kuongeza:

  “Tumeambiwa nyumba zingine zitawekewa X kesho (leo) na wanabomoa kama waliovuta bangi ,hawana huruma, wengi wamepoteza mali, lakini wepesi wameokoa baadhi ya mali”.


  Wakati huohuo Chama cha Wananchi (CUF) kimelaumu hatua ya SMZ kubomoa nyumba za wananchi eneo hilo.


  Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Mwasiliano na Umma wa CUF Salim Bimani, alisema ubomoaji huo umefanyika wakati shauri la suala hilo likiwa mahakama ya ardhi na bado halijatolewa uamuzi.


  “Sisi, Chama cha Wananchi (CUF), tunalichukulia suala hili kama ni uvunjaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala wa sheria ambao unahimiza kutokuchukuliwa hatua zozote za kisheria bila kupitia ngazi ya mahakama” alisema Bimani na kuongeza:


  “Pia tunatoa wito kwa SMZ, wanasheria na wananchi, kwamba SMZ isitishe mara moja bomoabomoa hiyo na ifidie hasara zilizopatikana kutokana na hatua hiyo.

  SOURCE MWANANCHI
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Feb 22, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh, ama kweli nchi inaongozwa kiholela!...
  kaazi kweli kweli!
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2009
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Eneo hilo wanakaa wapemba wengi na wengi wao ni wafuasi wa cuf huenda serikali ikawa iko right kuwa wamejenga kinyume na utaratibu lkn jee wakati ndio na hatua zilizochukuliwa ni sahihi ?
  Jee maeneo mengine ambayo waunguja na wafuasi wa ccm wanaishi hayapo na mbona hawachukui hatua kama hizi ?

  Jee huku ndio kujenga uvumilivu wa kisiasa ?
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magha'bi hana uwezo wa kisheria wa kuvunja nyumba za watu. Nawashauri hao waliovunjiwa nyumba zao pamoja na foundation waende mara moja Mahakamani na kufungua kesi ya madai dhidi ya Mkuu huyo wa mkoa.

  Ilipokuwepo JBA, ambacho kilikuwa ndio chombo pekee baada ya Mahakama chenye uwezo wa kuvunja na kuruhusu ujenzi na mwenyekiti wake akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini. Hata hivyo kuja kwa UDCA kumeondoa nafasi ya mkuu wa mkoa katika masuala yote ya ujenzi. Na mbaya zaidi hata hao UDCA hawana sheria ambayo inayowapa nguvu ya uvunjaji wa nyumba, kwani sheria za ujenzi katika Zanzibar zilikufa pamoja na JBA.
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  sasa kama watu wanavamia maeneo ya wazi ya kujenga shule...sasa SMZ ifanyeje?

  Hata Dar tumeyaona halafu eti watu wanamlilia Nyerere!
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hakuna kitu kinachoitwa kuvamia maeneo wazi katika Zanzibar... Ukujaribu kufuatilia utakuta sheha, diwani, mkuu wa wilaya na pengine mkuu wa mkoa kwa namna moja ama nyingine na katika nyakati tofauti walibariki ujenzi huo.
   
 7. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 8. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ah si ueleze ni yepi? Tupate hoja. Hivi mtu kutoka Kizimkazi kweli anataka kujenga kibanda Tomondo? Cha nini-Sema ukweli.
   
 9. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2009
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu wa Pwani,
  Huo mkasa wa kusikitisha sana hata kama waathiriwa walivamia hayo maeneo SMZ au Mkuu wa mkoa angetumia UBINADAMU angalau kwa kutoa NOTISI ya muda fulani kwa Wananchi. KAMA UPO UWEZEKANO TUPA PICHA za hiyo ZILZALA hapa jamvini.
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hao unaowabanangav walikwishasema Mambo ni kangaja......... Ubinaadamu unahitajika kwa wote hata hao Wapemba. Nafikiri tunasahau yaliyowakuta Waarabu hata wakapinduliwa kwa mawe . Tuache kutakabur, binaadamu si wa CUF wala CCM ni viumbe vya Mungu sasa kufurahia maafa ya mwenzio....
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Maneno yako yapo juu ya mstali... Kuna zaidi ya Idara nne zenye uwezo wa kutoa kibali cha ujenzi katika eneo lilivunjwa.

  Kwa mujibu wa master plan ya mwaka 1982, eneo la Tomondo lipo chini ya Manispaa ya Zanzibar na iwapo unahitaji kujenga katika eneo hilo lazima uwe na hati ya kumiliki ardhi toka katika Idara ya ardhi na eneo lazima liwe limepimwa.

  Chini ya Sheria ya Halmshauri ya Miji ya mwaka 1995, eneo hilohilo la Tomondo lipo ndani ya Halmshauri ya Magharibi. Hivyo Halmashauri hiyo inawajibika na maendelezo ya ardhi katika eneo hilo.

  Tomondo hiyo hiyo inawajibika kwa UDCA, inawajibika kwa Idara ya Ardhi, inawajibika kwa Idara ya Upimaji, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa, Katibu wa Halmshauri ya Wilaya Diwani wa Jimbo na Mwisho kabisa kwa Sheha wa Shehia ya Tomondo.

  Hao wote wanasimimia na kutoa ruhusa ya ujenzi katika eneo hilo, hivyo kuleta usumbufu mkubwa kama sio kukaribisha ujenzi holela. Mfumo wa Sheria na Taratibu za Ujenzi ulianza kwenda kombo baada ya SMZ kuvunja tawala za mikoa mwaka 1969, aidha kwa idara kadhaa kutoheshimu mipaka yao ya utendaji.

  Leo hii mtu una kila sababu ya kujiuliza iwapo Zanzibar kuna sheria za ujenzi
   
 12. K

  Kwaminchi Senior Member

  #12
  Feb 25, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Mimi si Muunguja wala si Mpemba. Lakini, kwa kuwa mimi ni binadamu, kinachomwathiri binadamu mwingine, kinanihusu.

  Wahenga walisema, sheria msumeno, unakata huku na huko. Ipo sheria inasema, alieiba ni mhalifu na anayeficha mali ya wizi, nae ni mhalifu pia ingawa hakushiriki kuiba.

  Kama wahusika walihalifu kwa kuvamia maeneo yasiyoruhusiwa kujengwa, nao wanaadhibiwa kwa kuvunjiwa majengo hayo, tena ghfla bila ya taarifa ya muda muafaka na bila kupitia vyombo vya sheria, kama vile mahakama, ni lazima tujiulize, walinda sheria walikuwa wapi na walikuwa wanafanya nini wakati wote huo ambao wavamizi walipata wasaa wa kujenga na kuishi huko? Je, wao si wahalifu pia? Na kama ndio, wao wanaadhibiwa vipi?

  Mimi naona, zoezi lote hili ni suala la "mnyonge kupata haki, ni mwenye nguvu kupenda." Hapa pana harufu ya unafiki. Hawa walinzi wa sheria, wanaposhika nyadhifa zao, hushika misahafu na biblia na kuapa kuwa watailinda katiba, ambayo ni sheria mama ya nchi. Moja ya madhumuni ya katiba ya nchi ni kumlinda mwananchi na mali yake. Ulinzi wenyewe ndio huu?

  Watazame unafiki wao, katika nyuso zao, wanapopita kwa raia kuomba kura. Sikiliza uongo wao, katika ahadi zao wanazotoa. Wanatoa ahadi hizo hizo, kwa maneno tofauti.
  Ahadi za kinafiki, zisizotekelezeka. Ujinga wa wapiga kura, ndio ngazi zao za kwendea madarakani. Wakisha kwea na kujikweza, sikiliza kauli zao, eti "panda ndege uje huku."

  Kinachoendelea hapo ni wizi wa kura. Watu wengi wanafikiri wizi wa kura hufanyika siku ya kupiga kura, kwa kupiga kura zaidi ya mara moja au kwa kuhesabu kura za kweli pamoja na zile za haramu peke yake. La hasha, zoezi la kura kuibwa huanza mapema sana
  kama hivyo.

  Wizi huendelea wakati wa zoezi la uandikishwaji wapiga kura, wakati wa mikutano ya kampeni, uwakilishi wa mawakala, rushwa na hongo kwa wapiga kura, ulaghai na mizengwe, vitisho vya kutandazwa askari na utembezwaji mikong'oto. Kabla watu hawajatanabahi, ushindi wa tsunami ushatangazwa. Na kabla ya tangazo rasmi halijatoka,
  washindi weshaapishwa vyumbani.

  Kinachobaki ni mazungumzo baada ya habari ya mwafaka feki.
   
Loading...