Zanzibar kuanza kuagiza mchanga kutoka Tanzania Bara

Serikali ya Zanzibar imetangaza mpango wa kuanza kununua mchanga kutoka Tanzania Bara kwa ajili ya kutumika katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa visiwani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar, Nadir Abdul Latif, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya siku 100 za uongozi wa Rais wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, katika kipindi cha pili cha uongozi wake.

Waziri Nadir amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na Zanzibar kukabiliwa na uhaba wa rasilimali ya mchanga unaoweza kukidhi mahitaji makubwa ya ujenzi, hasa katika kipindi hiki ambacho serikali inaendelea kutekeleza miradi mingi mikubwa ya maendeleo.

Amefafanua kuwa mchanga utakaoagizwa kutoka Tanzania Bara utatumika mahsusi katika miradi mikubwa ya ujenzi inayotekelezwa na serikali pamoja na ile inayohusisha uwekezaji mkubwa, ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo haukwami kutokana na changamoto ya upatikanaji wa mchanga.

“Tumegundua kuwa miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa Zanzibar kwa sasa inahitaji kiasi kikubwa sana cha mchanga. Kutokana na hali hiyo, serikali imefanya tathmini na kuona ni vyema kuanza kuagiza mchanga kutoka Tanzania Bara kwa ajili ya miradi hiyo mikubwa,” amesema.

Ameongeza kuwa hatua hiyo pia inalenga kulinda mazingira ya Zanzibar kwa kupunguza uchimbaji mkubwa wa mchanga ndani ya visiwa hivyo ambao unaweza kusababisha athari za kimazingira ikiwemo uharibifu wa ardhi, mmomonyoko wa udongo na kuathiri mifumo ya ikolojia.

Hata hivyo, Waziri huyo amesisitiza kuwa wananchi wa Zanzibar wanaohitaji mchanga kwa ajili ya shughuli ndogo za ujenzi kama ujenzi wa nyumba binafsi au utengenezaji wa matofali, hawatalazimika kununua mchanga kutoka Tanzania Bara.
chanzo ;Nipashe
Mbona ni muda sana mchanga na kokoto vinatoka Tanganyika miradi inayoendelea huko Zanzibar vitu hivyo vinatoka Tanganyika
 
Huu ni udwebedu mkubwa, wakati bahri imejaa nchanga tele!
 
Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar, Nadir Abdullatif Al-Wardy alisema hayo wakati akiwasilisha taarifa kuhusu mafanikio ya wizara hiyo katika siku 100 za Rais Dk Hussein Mwinyi madarakani jana.

Al-Wardy alisema mchanga huo utauzwa kwa wawekezaji wanaojenga hoteli kubwa na kutumika katika miradi ya serikali kama ujenzi wa viwanja vya ndege, viwanda madaraja na shule za serikali.

“Tumewapa kazi ya kuingiza mchanga na kokoto nyeusi kwa ajili ya miradi mikubwa, waweze kutuletea mchanga kwa njia ya meli,” alisema Al Wardy.

Alisema mchanga utakaotolewa Bara utakuwa na gharama kubwa kutokana na gharama za usafirishaji na vibali, hivyo si kwa ajili ya wananchi wa kawaida.

Alisema serikali haijapandisha bei za mchanga na kokoto, hivyo wauzaji wa bidhaa hiyo waweke bei za kistaarabu na wasiwakomoe wananchi.

“Wananchi wote wa Zanzibar ambao wapo chini ya uwezo wataendelea kupewa huduma na mchanga ueleule tunaoutoa Zanzibar na kwa bei ile ile na hatuna lengo la kuwapandishia, sisi tunataka wapate huduma bora,” alisema Al-Wardy
 
Ni mjinga tu ndiye atayeamini mchanga unapelekwa kwao na mchanga.

Tumerudi kulekule kwenye ufisadi, wizi wa dhahabu, maliasili nk..
 
Zanzibar kuna upungufu wa mchanga au wanamanisha nini
 
Mkuu, na Wazanzibari wanajua hivyo?
Au ndiyo ile kanuni ya "chao ni chao, ila chetu ni cha wote"?
Yes hiyo ndio kanuni yenyewe !, muungano ni kama ndoa, kuna mke na kuna mume, mume anawajibika kwa mkewe na kila kitu cha mume, pia ni cha mkewe, ila vile vitu vya mkewe ni vyake!
Mimi home kuna siku unarudi home unamkuta wife amevaa shati langu!, na mara kibao when we go out, anapulizia perfume yangu!, vipi mwenzangu utataka na wewe uvae gauni lake au kujipulizua perfume yake?

Tanzania ni nchi moja yenye uraia mmoja tuu wa Tanzania, Wanzanzibar wana haki zote za Utanzania na free access to mali na rasilimali zote za JMT ni za wote, ila vitu vya Zanzibar, ni mali ya Wanzanzibar wao pekee!.

P
 
Duh....!, yaani niandike makala kuhusu mchanga?!, Tanzania ni nchi moja, mchanga wote ni wetu sote, naomba kazi hii niwaachie waandishi wa mazingira, mimi naaendelea kuandika kuhusu issues, siandiki kuhusu vitu, wala kuhusu watu!.
P
Kama mchanga ni wetu sote Mtanganyika kanunue ardhi Zanzibar kama utaruhusiwa.

Nawaza kuwa tuendako Tanganyika itabomoka na kuharibiwa kabisa na Zanzibar kiuchumi, kiasi cha kwenda kukopa huko huko Zanzibar.
 
Back
Top Bottom