Zanzibar itaendelea kujitenga tu!

kajembe

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
878
500
Sisi wa Tanganyika tumelala bado usingizi wa pono hasa viongozi wetu, mambo haya yanamaudhi kweli ndiyo maana wazanzibar wamechoka na mambo yetu sasa wameamua kuwa kitu kimoja wote CUF na CCM na wanaonesha uzalendo wao wakupigania nchi yao,Sisi tulitegemea nini maelewano ya CCM na CUF visiwani!walikaa chini wakaona Kumbe Uzalendo kwanza sio vyama,vyama ugomvi tu na kugawa wananchi.

Ona sasa bara yameanza mambo ya ukanda,pwani wanasema ooh rais hatoki kaskazini,mara ooh udini tumekalia kulumbana mambo yasiyo ya maana huku wawekezaji kwenye madini actually wanyonyaji wanatuibia madini yetu kumbe kuna mpaka viwanja vya ndege kwenye mogodi du!

Wazinzibar waachwe waende zao wenzetu wamejanjaruka,sisi tumezubaa sana kama tunaibiwa hivyo madini unadhani wao watakuwa tayari kuendelea kuungana na sisi? mimi huwa najiuliza hivi ni jambo gani waliloongea Seif na Karume mara moja wakaelewana na kuamua kuwa wazarendo wa nchi yao! najipa jibu mwenyewe hawa watakuwa wameona mwenendo wetu ulivyo wakaona tunawapotezea muda maana hata rasimali zetu za huku bara hatujari tumekalia malumbano yasiyo na maana na uzalendo sifuri wakaona waunganishe nguvu dhidi yetu na sasa wanatuacha taratibu lakini kwa uhakika leo hii wanataka bodi yao ya mikopo ya elimu ya juu.

Narudia kusema kwani wao hawaoni uozo unafanywa bara? waache wamegundua tunadanganyana tu,mimi sio mzenj lakini naona sawa wanavyo fanya.Tunaibiwa madini tumekaa kimya,ufisadi mwingine tumesikia tena leo billion mia tatu na kitu wa zantel na airtel mpaka Mtu unajiuliza kwanini lakini jamani Watanzania,halafu wizara ya mali asili billion tisini du ajabu kweli, mara tunaambiwa hata wabunge wetu wa Africa Mashariki hawajui wanachofanya huko bungeni,hawajajipanga kama wenzao wa kenya tunategemea nini nchi ya namna hii jamani!

Haya angalia malumbano ya UVCCM, sasa Sumaye amejibu nae anawashangaa kwa maneno wanayo jiongelea tu bila kujua athari kwa nchi,sasa UVCCM kilimanjaro nao wamejibu wanawashangaa viongozi wa UVCCM taifa du, amakweli CCM imekufa jamani.

Wananchi sisi ndiyo tutakao amua mustakabali wa nchi hii na sio CCM. Chadema wameamua kuwaelimisha wananchi lakini wanaonekana wachochezi ajabu kabisa hii,kwani maisha hatuyaoni magumu! kwani sisi wajinga hatujui ugumu unachangiwa nini? Utapeli,ufisadi,wizi wa mali asili yetu ndiyo chanzo cha ugumu wa maisha yetu,hivi watanzania nani ametuloga?.

Mmambo yote haya yanasababishwa na kuwa na katiba mbovu ambayo watu wachache wamerundikiwa madaraka yote ya maamuzi na matokeo yake ndiyo haya, jamani tukatae haya mambo tuache ushabiki usio na tija, mambo ya udini, ukabila, ukanda hayatatatua matatizo yetu ya Njaa, elimu duni na kuchapika ila tu uongozi bora na katiba nzuri na tujue nchi hii yetu wote sio ya dola, tumeisikia amesema Sumaye kumbe ili uwe Rais vyombo vya DOLA vikukubali nashangaa sana kumbe tulipoteza muda wetu kusikiliza mikutano ya kampeni na hata kupiga kula,tumetumia billions of money kumbe ilikuwa changa la macho tu,kauli ya Sumaye ina nguvu maana alikuwa waziri mkuu na alikuwa jikoni na anajua anachokisema mimi mtu wa kawaida inaniingia kweli kauli kama hayo na nimeamini Dr slaa alikuwa ana haki ya kulalamika. Sasa maskini CCM mmeanza kulumbana wenyewe na ukweli wote tutaujua, mmeamua kumwaga ugali na wengine wanamwaga mboga sasa kumekucha.
 

Kamundu

JF-Expert Member
Nov 22, 2006
4,414
2,000
Kajembe unakiswahili kizuri sana!. Watu wa bara hatuna kiswahili kizuri hivyo ndugu yangu nakupongeza
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom