Zanzibar hajawahi kutoa rais wa Muungano

Zanzibar hajawahi kutoa rais wa Muungano

mdukuzi

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
22,338
Reaction score
56,115
Miaka 50 ya muungano wa tanganyika na zanzibar ,zanzibar haijawahi kutoa rais wa muungano,rais wa kwanza nyerer kazaliwa butiama ,mwinyi kazaliwa kivule mkoa wa pwani ,mkapa mtwara na JK msoga na kuna dalili rais wa tano kutoka bara kwani majina yanayotajwa ni ya wabara tu
 
Kwan Zanzibar imeshawahi kuwa na raisi kutoka bara? Au hata waziri tu!

Zanzibar ni wajanja kuliko Tanganyika yaani Wao cha kwao ni cha kwao tu ,lakini cha Tanganyika ni cha Wote . Wabunge wa Zanzibar ni Mawaziri huku Tanganyika tena wengine ktk Wizara ambazo si za muungano , lakini hakuna mbunge wa Tanganyika amewahi Kuwa Waziri Zanzibar hata kunusa vikao vya Baraza la wakilishi tu imekuwa Vigumu.Wabunge wa Zanzibar wanakula posho Dodoma lakini Wabunge wa Bara marufuku Posho ya Baraza la wakilishi.inashangaza sana eti Kisiwa Kidogo chenye watu million 1.5 tu kinagawana mapato sawa na Nchi yenye watu million 44 ambayo wameiroga ilikatae jina lake la Asili na kung'ang'ania Kuvaa koti la Muungano Lenye Kunguni na Chawa.
 
Urais taasisi nyeti sana huwezi kuifanya ya kizamuzamu!
 
Miaka 50 ya muungano wa tanganyika na zanzibar ,zanzibar haijawahi kutoa rais wa muungano,rais wa kwanza nyerer kazaliwa butiama ,mwinyi kazaliwa kivule mkoa wa pwani ,mkapa mtwara na JK msoga na kuna dalili rais wa tano kutoka bara kwani majina yanayotajwa ni ya wabara tu
Pesa inayotoka Tanganyika kwa ajili ya kuubembeleza muungano ni Nyingi kuliko hata wangekuwa na Rais mpemba, wazanzibar wanafaidika sana na matunda ya muungano,Umeme bure,pesa za kulipa Mishahara ,posho na huduma za jamii zote zinatoka Tanganyika,Pesa Yao wananunulia Urojo na kununua Viwanja na Majumba ,kwa kweli Tanganyika amekuwa Dog mbele ya Chatu Hana Sauti mbele ya Zanzibar , ndio Maana wamevunja katiba na kujiita Nchi lakini Tanganyika ikaogopa kuwauliza kisa wanahofia Zanzibar watakasirika na kuomba Talaka kisha wafunge ndoa na Oman.
 
Iweje nchi nyingine itoe rais kuongoza nchi nyingine? Mbona hakuna waziri kiongozi wa smz aliyetoka bara?
 
Zanzibar pekee ndie iliotoa Rais Msaliti wa Muungano, mfungwa Aboud Jumbe, na wasaliti wa Jamhuri wengine Amani Karume, Salmin Amour ambao wote ni Marais wa Zanzibar ambao Koti linemewabana kwa kuvimbiwa pesa za Tanzania.
Pia kati ya hao Marais 4 wa Tanzania 3 wametoka mikoa ya Pwani.
 
Miaka 50 ya muungano wa tanganyika na zanzibar ,zanzibar haijawahi kutoa rais wa muungano,rais wa kwanza nyerer kazaliwa butiama ,mwinyi kazaliwa kivule mkoa wa pwani ,mkapa mtwara na JK msoga na kuna dalili rais wa tano kutoka bara kwani majina yanayotajwa ni ya wabara tu

Khaa!! Hapa ndiyo naona busara kubwa za Mh J Kikwete. Huwezi kuwatenganisha wapemba, waunguja na watanganyika aslan. Udugu wao niwa damu ni wa asili. Umethibitisha hivyo kwenye uzi huu wako
 
Miaka 50 ya muungano wa tanganyika na zanzibar ,zanzibar haijawahi kutoa rais wa muungano,rais wa kwanza nyerer kazaliwa butiama ,mwinyi kazaliwa kivule mkoa wa pwani ,mkapa mtwara na JK msoga na kuna dalili rais wa tano kutoka bara kwani majina yanayotajwa ni ya wabara tu

Hii nayo ni kero. Itaondoka tu mara tutakapokuwa na serikali tatu, Tanganyika, Zanzibar na JMT. Ikitokea sasa hivi itaonekana Mzanzibari (mgeni) anatawala watanganyika ambao hawana nchi mpaka sasa!
 
Mbona hata karume ni mbara? Si huyu alikuwa mvuvi wa kisukuma
 
Karume alikuja Zanzibar toka Malawi akiwa tayari na mvi kichwani. Pia Dr Bilal kaja kwa miguu yake toka Malawi.
 
Back
Top Bottom