kiswahili fasaha ungesema Zanzibar hainauwezo kuchangia sawa na TanganyikaZanzibar haina uwezo kuchangia sawa na Bara
Na Sharon Sauwa, Mwananchi
Posted Jumanne,Novemba12 2013 saa 24:0 AM
KWA UFUPI
Inadaiwa haina mapato kujiendesha na kuchangia Muungano kama Srikali tatu zitapitishwa Katiba Mpya
Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uchumi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Salimin Awadhi Salimin amesema Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kuchangia uendeshaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama muundo wake utakuwa wa Serikali Tatu.
Amesema Zanzibar haiwezi kuchangia hata kwa asilimia 10, hivyo kuukubali mfumo huo kunauweka Muungano katika hatihati ya kuvunjika. Katika utekelezaji wa utaratibu huo, Tanzania Bara na Zanzibar kila moja inatakiwa kuchangia asilimia 50 ya gharama za uendeshaji wa shughuli za Serikali ya Muungano.
Akizungumza katika semina ya Wabunge wa Muungano na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar mjini Dodoma jana, Salimin alisema hali hiyo inatokana na udogo wa uchumi wa Zanzibar na kusisitiza kuwa mfumo wa sasa wa serikali mbili ndiyo unafaa.
Rasimu ya kwanza iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Julai mwaka huu ilikuwa inapendekeza kuundwa kwa Serikali Tatu; za Muungano, Tanzania Bara na ile ya Zanzibar.
Alisema wakati wa kujadili mfumo huo ni lazima kuangalia suala la kiuchumi katika Serikali mbili zilizopo, iwapo zina uwezo wa kugharimia uendeshaji wa Serikali ya Muungano.
Tunapokuwa na Serikali ya Tanganyika, tunapokuwa na Serikali ya Zanzibar, tunapokuwa na Serikali ya Muungano kwa vyovyote vile matumizi yatakuwa makubwa mno, alisema Salimin katika semina hiyo iliyoandaliwa
na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), kujadili Rasimu ya Katibu Mpya.
Alisema Serikali ya Muungano itatakiwa kuhudumiwa kwa mapato yanayotoka katika Serikali mbili zinazounda Muungano, jambo ambalo Serikali ya Zanzibar haiwezi.
Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya Zanzibar, nauangalia uchumi wangu wa mapato ya kila mwaka. Je, tunaweza kuchangia hata asilimia 10? alihoji.
Alisema mapato ya Zanzibar kwa mwaka 2013/2014 ni Sh240 bilioni tu na kutoa mfano wa Wizara za Mambo ya Ndani na ile ya Ulinzi ambazo ziko chini ya Muungano kuwa bajeti yake ni kiasi cha Sh1.3 trilioni kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.
Alisema amepiga hesabu na kugundua kuwa gharama ya kuendesha wizara zote za Muungano inakadiriwa kuwa Sh3 trilioni.
Kama Sh3 trilioni zitahitajika katika kuendesha Serikali ya Muungano, sisi Zanzibar tukiambiwa tuchangie hata asilimia 10 tu ambayo ni sawa na Sh300 bilioni tutaweza? alihoji Salimin.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi
mwkilishi huyu ni mbumbumbu hakuna asiejua. kichaka chake ni CCM tu na ndio akawa mwenyekiti wa kamati. Yeye na Waziri wa Fedha Omar , tena mwenzake anajua nani zaidi mambo ya uchumi ?.Huyo mwenyekiti angemuulia Malim Seif, Mansour na Jussa, wanaweza kuwa na majibu kuhusu uwezo wa Zanzibar kuwa nchi kamili ndani ya Muungano wa 'Pasu kwa Pasu'.
Hatutaki muungani hata Jakaya anajua. kwenye kukusanya maoni juu ya uunwaji wa katiba mpya zaidi ya silimia sitini (60%) ya Wazanzibari wamesema wanataka muungano wa mkataba. hizi takwimu za ccm zilizojitokeza sasa tunajua ni janja ya Tanganyika kutaka kuendelea kutuuibia. Hatutaki Muungano na wachuna ngozi za wanadamuSasa wanataka muungano wa nini kama hawawezi kuchangia.... mbona kwenye mapato mnataka sawa.?
Hatutaki muungani hata Jakaya anajua. kwenye kukusanya maoni juu ya uunwaji wa katiba mpya zaidi ya silimia sitini (60%) ya Wazanzibari wamesema wanataka muungano wa mkataba. hizi takwimu za ccm zilizojitokeza sasa tunajua ni janja ya Tanganyika kutaka kuendelea kutuuibia. Hatutaki Muungano na wachuna ngozi za wanadamu
Copy Barubaru chama gombesugu THE BIG SHOW ...................
Ukweli umetimia sasa wanahangaika. Uongo wa kusema Tanagnyika inawanyonya sasa hadharani.Huyo mwenyekiti angemuuliza Malim Seif, Mansour na Jussa, wanaweza kuwa na majibu kuhusu uwezo wa Zanzibar kuwa nchi kamili ndani ya Muungano wa 'Pasu kwa Pasu'.
cc Nguruvi3
Ukweli umetimia sasa wanahangaika. Uongo wa kusema Tanagnyika inawanyonya sasa hadharani.
Kitu cha ajabu sana ni hao hao wanataka tume iwe asilimia 50, wanataka bunge la katiba liwe asilimia 50. Wanataka viongozi wa muungano na wafanyakazi wa serikali ya muungano wawe nusu kwa nusu.
Tumewahi kuwaeleza mara nyingi sana wazanzibar akiwemo Jusa na Ahmed Rajab kuwa Tanganyika haihitaji znz kwa lolote. Hatuhitaji znz ila znz inatuhitaji sana.period.
Ona sasa imefika wakati wa gharama wanajichafua nguo hovyo. Wale wanaosema Tanganyika inawanyonya znz wajiulize kama mwenyekiti wa kamati anasema hawana uwezo, Tanganyika inawanyonya wapi.
GHIBUU takashi Jusa Jasusi JokaKuu Kakke Jasusi Nonda gombesugu Zinedine FJM