Zanzibar haina uwezo kuchangia sawa na Bara’

Zanzibar haina uwezo kuchangia sawa na Bara’

Kashishi

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2010
Posts
1,147
Reaction score
641
Zanzibar haina uwezo kuchangia sawa na Bara’

Na Sharon Sauwa, Mwananchi

Posted Jumanne,Novemba12 2013 saa 24:0 AM

KWA UFUPI

Inadaiwa haina mapato kujiendesha na kuchangia Muungano kama Srikali tatu zitapitishwa Katiba Mpya

Dodoma.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Fedha na Uchumi ya Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Salimin Awadhi Salimin amesema Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kuchangia uendeshaji wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kama muundo wake utakuwa wa Serikali Tatu.

Amesema Zanzibar haiwezi kuchangia hata kwa asilimia 10, hivyo kuukubali mfumo huo kunauweka Muungano katika hatihati ya kuvunjika. Katika utekelezaji wa utaratibu huo, Tanzania Bara na Zanzibar kila moja inatakiwa kuchangia asilimia 50 ya gharama za uendeshaji wa shughuli za Serikali ya Muungano.

Akizungumza katika semina ya Wabunge wa Muungano na Wawakilishi wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar mjini Dodoma jana, Salimin alisema hali hiyo inatokana na udogo wa uchumi wa Zanzibar na kusisitiza kuwa mfumo wa sasa wa serikali mbili ndiyo unafaa.

Rasimu ya kwanza iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Julai mwaka huu ilikuwa inapendekeza kuundwa kwa Serikali Tatu; za Muungano, Tanzania Bara na ile ya Zanzibar.

Alisema wakati wa kujadili mfumo huo ni lazima kuangalia suala la kiuchumi katika Serikali mbili zilizopo, iwapo zina uwezo wa kugharimia uendeshaji wa Serikali ya Muungano.

“Tunapokuwa na Serikali ya Tanganyika, tunapokuwa na Serikali ya Zanzibar, tunapokuwa na Serikali ya Muungano kwa vyovyote vile matumizi yatakuwa makubwa mno,” alisema Salimin katika semina hiyo iliyoandaliwa

na Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), kujadili Rasimu ya Katibu Mpya.

Alisema Serikali ya Muungano itatakiwa kuhudumiwa kwa mapato yanayotoka katika Serikali mbili zinazounda Muungano, jambo ambalo Serikali ya Zanzibar haiwezi.

“Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Uchumi ya Zanzibar, nauangalia uchumi wangu wa mapato ya kila mwaka. Je, tunaweza kuchangia hata asilimia 10?” alihoji.

Alisema mapato ya Zanzibar kwa mwaka 2013/2014 ni Sh240 bilioni tu na kutoa mfano wa Wizara za Mambo ya Ndani na ile ya Ulinzi ambazo ziko chini ya Muungano kuwa bajeti yake ni kiasi cha Sh1.3 trilioni kwa mwaka wa fedha wa 2013/14.

Alisema amepiga hesabu na kugundua kuwa gharama ya kuendesha wizara zote za Muungano inakadiriwa kuwa Sh3 trilioni.

“Kama Sh3 trilioni zitahitajika katika kuendesha Serikali ya Muungano, sisi Zanzibar tukiambiwa tuchangie hata asilimia 10 tu ambayo ni sawa na Sh300 bilioni tutaweza?” alihoji Salimin.

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Huyo mwenyekiti angemuuliza Malim Seif, Mansour na Jussa, wanaweza kuwa na majibu kuhusu uwezo wa Zanzibar kuwa nchi kamili ndani ya Muungano wa 'Pasu kwa Pasu'.

cc Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:

kiswahili fasaha ungesema Zanzibar hainauwezo kuchangia sawa na Tanganyika
 
Hawa jamaa Wazenji bwana si mnaona wameshaanza kutoa nje? Si ndio walikuwa wanadai serikali tatu hawa kuwa kila watu we na yao wapate kupumua🙂

Unajua akina Mzee Warioba wamewapa serikali yao makusudi ili hii sinema wote tuione mwisho wake...lakini watapewa serikali yao na soon tutafika mahali watu wataulizwa mwataka serikali moja au kuendelea na tatu. Na sisi haturudi tena kwenye mbili...mana huko kwenye mbili tulisha shindwana na hawa jamaa. Itabidi wachague tatu au moja. Kwisha!

Mambo yenyewe wamdedai 'haki sawa kwa wote' kwenda mbele tumesema sawa. Wanataka Equal partnership...haya wee. 'Hakuna kumezana 'sawa wazee. Malipo ya serikali yetu muungano pia hatuna haja kuumizana. Unasikia watu wakidai hapo hatuko sawa...unajiuliza kivipi?

Akina Mzee Warioba na akina Kiwete wasoma alama za nyakati watu hawakukurupuka kumwaga hizi serikali tau kama wwenyewe walivyolilia. Wale waliokuwa hawaelewi fumbo la serikali tatu sasa watakuwa wamepata idea.
 
Hizi ndizo hoja zinazotakiwa kwenye Muungano. Kwa maana nyingine, serikali ya Zanzibar haitaki serikali tatu wakati pia wanadai serikali mbili zinawanyonya!. Hoja iliyojificha hapa ni kuwa, Wazanzibar hawataki muungano. Finito.

Siyo jambo la kushangaza kusikia hoja kama hii kisiasa kwa sababu serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaongozwa kwa kiasi kikubwa na sera za CCM ambapo serikali mbili ndiyo sera yake na pia Salimin Awadhi Salimin ni mwakilishi kupitia tiketi ya CCM.

Hakuna haja ya kuwa na muungano kama hakuna manufaa endelevu kwa wananchi wake. Swala la kuwa kwenye muungano ambapo msingi wake mkuu ni siasa halina mashiko hata kidogo katika dunia ya sasa inayonyambulishwa kiuchumi zaidi.

Bila kujali anachokisema ni sera ya CCM, fact always fact hasa katika uhalisia wa jambo ambalo linahusisha uchumi. Watanganyika lazima tuuangalie muungano kiuchumi zaidi na katika uchumi ndipo tunapata gharama za serikali tatu halafu vile vile kuna kuchangia gharama za EAC achilia mbali regional economic, political and security cooperation schemes with other nation. Hizi ni gharama kubwa sana na sidhani kama Watanzania wanapata value for their tax money. Gharama za Zanzibar inayochangia kwenye serikali mbili hazisemwi!.

Kwa nini tusiachane na Zanzibar na tukakutana nao katika SADC kama member nation kitu ambacho ni political and economic sense kuliko kung'ang'ania kuwa na nchi ambayo haiwezi hata kulipa 10% ya gharama za Muungano.

Kiuchumi Tanganyika itanufaika sana kuwa mwanachama wa SADC zaidi ya kuwa na muungano na Zanzibar na hasa iwapo watanzania watatumia ipasavyo nafasi hii kwa sababu ukiangalia total population and GDP kwa kila nchi inakupa wastani wa per capital $2,080.
 
Huyo mwenyekiti angemuulia Malim Seif, Mansour na Jussa, wanaweza kuwa na majibu kuhusu uwezo wa Zanzibar kuwa nchi kamili ndani ya Muungano wa 'Pasu kwa Pasu'.
mwkilishi huyu ni mbumbumbu hakuna asiejua. kichaka chake ni CCM tu na ndio akawa mwenyekiti wa kamati. Yeye na Waziri wa Fedha Omar , tena mwenzake anajua nani zaidi mambo ya uchumi ?.
 
weli hatutaki muungano na mafuta yetu hivi hamjui? au mnataka kuendelea kutunyonya? na kutuibia rasilmali zetu za mafutana bahari kuu?
 
Sasa wanataka muungano wa nini kama hawawezi kuchangia.... mbona kwenye mapato mnataka sawa.?
Hatutaki muungani hata Jakaya anajua. kwenye kukusanya maoni juu ya uunwaji wa katiba mpya zaidi ya silimia sitini (60%) ya Wazanzibari wamesema wanataka muungano wa mkataba. hizi takwimu za ccm zilizojitokeza sasa tunajua ni janja ya Tanganyika kutaka kuendelea kutuuibia. Hatutaki Muungano na wachuna ngozi za wanadamu
 
Sasa Baraqhas ... mnachotaka ni nini? Kwa nini uwe wa mkataba? Kwa nini msiseme hamtaki muungano kabisa tujuwe moja? Muungano wa mkataba ndio ukoje? Tafadhali fafanua
 
Zanzibar hata kulipa bill tu ya umeme imewashida, wataweza kweli kuchangia muungano ulio sawa. Ni bora kwao waukate na kuuvunja huu muungano.
 
Ngongo,

Sina hakika kwa undani zaidi na hayo matamshi ya huyo Bwana Kiongozi kama alivyonukuliwa na hilo jarida.

Insha Allah,tunafuatilia hizi khabar kwa utuvu...lakini nakhis yakuwa hayo ni mazungumzo tu ya kisiasa,kwa maana nyingine ni coded words za sisi kukwambiani nyinyi Watanganyika yakuwa huo Muungano hatuutaki tena,ushitushinda kwa mangi ya ulaghai na dhuluma!?

Hicho ni kipimo changu tu binafsi kiduchu kwa kuanzia,lakini tarejea tena hapa barzan kadri mnakasha utakavyoendelea.

Labda Mufti Barubaru,atakapopata fursa ya kujongelea hapa barzan yawezakuwa ana mangi ya kutujuza...maana yeye ni mbobefu wa mahisabu na takwimu hizo za fedha za kuendesha huo "Muungano".

Lakini pia tujikumbushe japo kiduchu,yakuwa kabla ya hizo Serikali tatu,italazim pia turejee nyuma kiduchu na kujikumbusha madeni ya Serikali ya Muungano/JMT,ambayo inadaiwa na Serikali ya Zanzibar!?

Sijawahi hata siku moja kuona member/s yeyote au hata thread yeyote humu JF,ikikumbushia zile "enzi za Mwalimu"; wakti Tanganyika na Serikali ya Muungano vikiwa taabani kiuchumi,na zikitegemea pita kiasi senti/akiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar-SMZ ili kujikimu na kujiendesha!?

Mnakumbuka yakuwa wakti ule wa ile vita ya Nyerere dhidi ya Uganda,SMZ iligharamia kwa kiasi kikubwa mno ile vita ambayo binafsi Wananachi wa Zanzibar wala Serikali yao haikushirikishwa kikamilifu kwenye yale maamuzi dhaifu ya Nyerere kungia vitani baada ya kumchokoza kwa makusudi yule mpuuzi Idd Amin kwa miaka kadhaa!?

Mnakumbuka pia,SMZ ililazimishwa na Nyerere kutumia akiba yake takriban yoote kugharamia yale yaliyoitwa ati "mapambano ya ukombozi wa nchi za Afrika"!?

Niwia radhi Mkuu,hapa silalamiki asilan,lakini ni muhimu pia kiduchu kujikumbusha fadhila,ihsan na madeni mangi mno dhidi ya hiyo Tanganyika aka JMT...ambayo(madeni dhidi ya JMT) mpaka kesho hayajawahi kuzungumziwa hata na Viongozi wowote wa ngazi za juu,na hatujui sababu ni ipi!?...labda woga,ubinafsi,uchu wa madaraka,vitisho au upumbavu wa fikra!?

Ahsanta.
 
Huyo mwenyekiti angemuuliza Malim Seif, Mansour na Jussa, wanaweza kuwa na majibu kuhusu uwezo wa Zanzibar kuwa nchi kamili ndani ya Muungano wa 'Pasu kwa Pasu'.

cc Nguruvi3
Ukweli umetimia sasa wanahangaika. Uongo wa kusema Tanagnyika inawanyonya sasa hadharani.

Kitu cha ajabu sana ni hao hao wanataka tume iwe asilimia 50, wanataka bunge la katiba liwe asilimia 50. Wanataka viongozi wa muungano na wafanyakazi wa serikali ya muungano wawe nusu kwa nusu.

Tumewahi kuwaeleza mara nyingi sana wazanzibar akiwemo Jusa na Ahmed Rajab kuwa Tanganyika haihitaji znz kwa lolote. Hatuhitaji znz ila znz inatuhitaji sana.period.

Ona sasa imefika wakati wa gharama wanajichafua nguo hovyo. Wale wanaosema Tanganyika inawanyonya znz wajiulize kama mwenyekiti wa kamati anasema hawana uwezo, Tanganyika inawanyonya wapi.

Hawa watu wamefundishwa ujinga wa kuamini maneno ya mitaani bila ushahidi wa kiuchumi.
Tunasema hivi serikali ni tatu na kila mmoja achangie sawa.
Muda wa kubeba watu migongoni wakitukana hovyo iumekwisha.

Hiki ni kijimkoa tu lakini kelele tu wamejaaliwa. Tutakomaa hadi mtaomba radhi kwa maneno yenu machafu.
Wananyanyua pua eti muungano ni nchi mbili wabia sawa. Thubutu, wabia sawa wakati wewe unachangia maneno na kelele ! usawa wa ubia upo wapi.

Wewe unavia kodi za Mtanganyika halafu unasema ubia sawa. Hawa watu waajabu sana.
Leo wanasema hawana uwezo na wakati wa kujadili muungano hali ya uchumi iangaliwe.
Ni hawa hawa walikomaa tume iwe na wajumbe sawa. By the way hawajui gharama za tume wala za bunge la katiba.Kelele zitawatokea puani this time

fungeni midomo na muwe na adabu. Shikeni adabu, muungano uchumi si mipasho na taarabu.
Leteni kitu mezani si kuvizia nafasi za urais wa zamu na uwaziri. Kupe wakubwa mninyi.

Mkome kusema mnanyonywa, nani anyoinye mnasikini wa mapato kama yenu.
Mkome kudai vyeo msivyojua gharama zake. Matabaki chini ya kivuli cha Tanganyika kwasababu hamna uwezo.period

GHIBUU takashi Jusa Jasusi JokaKuu Kakke Jasusi Nonda gombesugu Zinedine FJM
 
Ukweli umetimia sasa wanahangaika. Uongo wa kusema Tanagnyika inawanyonya sasa hadharani.

Kitu cha ajabu sana ni hao hao wanataka tume iwe asilimia 50, wanataka bunge la katiba liwe asilimia 50. Wanataka viongozi wa muungano na wafanyakazi wa serikali ya muungano wawe nusu kwa nusu.

Tumewahi kuwaeleza mara nyingi sana wazanzibar akiwemo Jusa na Ahmed Rajab kuwa Tanganyika haihitaji znz kwa lolote. Hatuhitaji znz ila znz inatuhitaji sana.period.

Ona sasa imefika wakati wa gharama wanajichafua nguo hovyo. Wale wanaosema Tanganyika inawanyonya znz wajiulize kama mwenyekiti wa kamati anasema hawana uwezo, Tanganyika inawanyonya wapi.
GHIBUU takashi Jusa Jasusi JokaKuu Kakke Jasusi Nonda gombesugu Zinedine FJM

Wataongea tu, hakuna namna.

Kwa sasa tuna serikali mbili, serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano -ambayo kimsingi inahusika na mambo ya Tanganyika na yale ya Muungano. Kama mwenyekiti anasema kuwa Zanzibar haina uwezo wa kuchangia Serikali ya Muungano endapo kutakuwa na serakali tatu, maana yake amekiri kuwa hata sasa hivi Tanganyika ndio inalipa 'bills' zote. Sasa huo unyonyaji aoimba Maalim Seif unatoka wapi?

Na siku zote tumekuwa tunasema hapa, madai ya pasu kwa pasu yasishie kwenye kuepeana nafasi za kazi peke yake, kila upande wa Muungano uwalipe watu wake.

Wasipokuwa makini hii inakula kwao, maana Tanganyika wamechoka kuitwa wakoloni, sasa watadai serikali moja au tatu.
 
Wacheni hivi mnapapasa au mnajua kilichopo ,hivi Mungano wa Ulaya una nchi ngapi ? Katika nchi hizo hakuna zilizo ndogo na ambazo nyingine bora Zanzibar kwa Utajiri ,Hapa kwenye huu Muungano tunaojing'ang'aniza wa EAC hivi nchi zote ni tajiri ?

Tatizo lipo wapi au kwa huyo memba wa Chama Cha Mashetani (CCM) ambae anajivutia huko upande wa pili yakhe kama tutakuwa hatuna uwezo hapana jipya eti ,si tutagawana mbao tu ! Aafu tutajiunga na Kenya na Uganda na Rwanda ,tutapeleka maombi huko ,ila kwenu kwa vile tutakuwa hatuna uwezo tutawasamehe ,halafu nyie wazito sana hamubebeki ,ndio maana akina Kenya wamewatenga kiaina ,mnaonekana mumo lakini hamumo ,kiukweli mpo outside mpo kama outsider tu.

Sina wakati mrefu kwa sababu nipo hapa Philipines tukitoa msaaada wa kibinadamu.
 
Back
Top Bottom