Zanzibar hadi lini?

mtwana

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
428
140
Hivi najiuliza hali hii ya Zanzibar hadi lini mbona sielewi, maana hakuna Rais wala waziri na wananchi wapo njia panda hadi hii leo hawajui kama utakuwepo uchaguzi au haupo..

Kama upo kwa sheria gani zinasema na kama haupo kipi kinachofata..

Nawasilisha kijihoja
 
Hivi najiuliza hali hii ya Zanzibar hadi lini mbona sielewi..
maana hakuna Raisi wala waziri na wananchi wapo njia panda hadi hii leo hawajui kama utakuwepo uchaguzi au haupo..
kama upo kwa sheria gani zinasema na kama haupo kipi kinachofata..

nawasilisha kijihoja

Mambo yanayoendelea Zanzibar yananikumbusha kitabu kimoja kinaitwa Kivuli Kinaishi.

Mambo ya Giningi, Bibi Kirembwe akina Mtolewa. Waliokisoma wamenielewa.
 
Hivi najiuliza hali hii ya Zanzibar hadi lini mbona sielewi..
maana hakuna Raisi wala waziri na wananchi wapo njia panda hadi hii leo hawajui kama utakuwepo uchaguzi au haupo..
kama upo kwa sheria gani zinasema na kama haupo kipi kinachofata..

nawasilisha kijihoja
Solution ya Zanzibar ni so simple.
Uchaguzi ulifanyika tarehe 25/10/2015 kwa amani na utulivu.
Waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi wakatoa taarifa zao za tathmini ya uchaguzi huo na kuuita kuwa ulikuwa huru na haki.
Mawakala wa vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo wakasaini fomu za matokeo hayo na hata washindi wa baraza la wawakilishi wamekabidhiwa vyeti vyao vya ushindi.
Mwenyekiti akaanza kutangaza matokeo ya Urais na baraza la wawakilishi kwenye majimbo mbalimbali hadi yakafikia 34 kati ya majimbo 51 ya Unguja na Pemba.
Ghafla siku ya 3 ya matangazo ya tarehe 28/10/2015 kwa mshangao mkubwa, ndipo tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha, linasomwa kupitia ZBC tena likiwa recorded, akieleza kuufuta uchaguzi huo kwa mamlaka aliyodai anayo, lakini bila kutaja kifungu chochote cha sheria kinachompa mamlaka hayo.
Ni dhahiri kwa mlolongo huo wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar ulivyokwenda, naweza kuthubutu kwa kusema kuwa tamko la Jecha ni batili na halina nguvu kisheria, unless serikali ya CCM itake tu kulazimisha na kuamua kulihalalisha tamko hilo la kibabe.
Kwa hiyo solution pekee kwa maslahi mapana ya Zanzibar na Taifa la Tanzania kwa ujumla wake, ni kwa Tume ya uchaguzi Zanzibar kumalizia 'kiporo' cha kutangaza matokeo ya majimbo 17 yaiyokuwa yamesalia na hatimaye kumtangaza mshindi aliyeshinda kiti cha Urais Zanzibar.
Njia nyingine zozote ambazo watawala watataka kuyakataa matakwa ya wananchi na badala yake kutaka wao ndiyo wang'ang'anie madarakani hata kwa kudiriki kuivunja Katiba ya nchi waliyoapa kuilinda, hakika uchu huo wa madaraka wa watawala wetu unaweza kulitumbukiza Taifa hili kwenye machafuko makubwa.
 
Sala na dua mbali mbali za kuomba amani na utulivu zinahitajika.Viongozi muogopeni ALLAH......hakuna wa kuishi milele hapa diniani.Bahati nzuri wote ni Islam na munaijuwa dini barabara.Sisi maamuma munatupeleka wapi....????
 
Unasema bahati nzuri wote ni ISLAM!!! Speak for yourself!!! Nyie wote na nani? Acha umburula wako wa udini hapa mambo ya Zanzibar ni ya HAKI ya Wazanzibari wote wa dini mbalimbali!!
 
Nakubaliana na nyinyi ila kiupande Mmoja sihisi ila ndio ukweli kua watawala hawaamini kua Nchi sio mali ya CCM na ndio mana inakua vigumu sana kuachia madaraka..
Lengo lao labda watu wafanye fujo than wapate sababu ya kusema kua wapinzani wanapenda fujo na ndio ilivotokea Zanzibar baada ya kuufuta uchaguzi na ndio maaskari wakawa wapiga watu ovyo na kupiga mabomu ya machozi bila sababu hali ya kuwa watu walitulia kabisa
Ila kwa dhulma hii hakika Mwenyezi Mungu hatokua nao pamoja In Sha Allah na uchaguzi hautorejewa na Mshindi halali atatangazwa bila kumwagika damu ya mtu mwengine yoyote
 
Zanzibar zanzibar utawala wa kiduni ndo unawapa adhabu hii wangekua wanafuta utaratibu wa tawala za kidini haya yote yasingewakuta hakuna ccm wala cuf wate wamatanguliza maslah ya dunia mbele
 
Nenda zako Syria kaka kama wewe napenda Islamic State. Dini ndani ya moyo yako kaka sio government Inchi ona Saudia Sharif Haramain nini nafanya kule Yemen? Queen of England is Defender of The Faith (Christianity) nini nafanya duniani? Hindu BJP Gujerat Province ya India nini memafanya, Budhist Myanmar nini mefanya ile Rohyngas kule.
 
Sala na dua mbali mbali za kuomba amani na utulivu zinahitajika.Viongozi muogopeni ALLAH......hakuna wa kuishi milele hapa diniani.Bahati nzuri wote ni Islam na munaijuwa dini barabara.Sisi maamuma munatupeleka wapi....????
Amani huletwa na haki! Sala na Dua hazina uhusiano wowote na AMANI.
 
Nenda zako Syria kaka kama wewe napenda Islamic State. Dini ndani ya moyo yako kaka sio government Inchi ona Saudia Sharif Haramain nini nafanya kule Yemen? Queen of England is Defender of The Faith (Christianity) nini nafanya duniani? Hindu BJP Gujerat Province ya India nini memafanya, Budhist Myanmar nini mefanya ile Rohyngas kule.

Punjab Singh you have made my day.
 
Back
Top Bottom