Zanzibar: Eddy Riyami atangaza kujitoa CCM

Zanzibar: Eddy Riyami atangaza kujitoa CCM

Huu mkoa (Zanzibar) wa Tanganyika (Tanzania) una #makeke !!!!!!!!!!!! Si mchezo.
Tusipotoshe habari,Zanzibar ilikuwepo kama ilivyokuwepo Tanganyika,kabla ya uhuru na baada uhuru wa Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi za kuonekana kwa macho,na kiutawala, wala sio mambo ya kubuni.Hatuwezi kukwepa watu wenye mawazo huru katika mabadiliko au muundo wa Tanzania mpya 2015.Anaye sema ni gharama kuwa na serikali tatu anamapungufu ya kihisabati.Hakuna hata siku mmoja walipowahi kutoa ufafanuzi wa gharama za serikali tatu,tunachokisikia ni headline tu.Familia yeye watoto 3 haina maana familia inatumia gharama mara tatu ya familia ya mtoto 1.Iweje mnaongeza idadi ya mikoa na wilaya kila kukicha?labda hilo ndo tatizo.Rudi darasani.
 
akili za pruduct ya shule za kata yani chekechea kata, primari kata, sekondari kata, chuo udom kata.

Unaweza vipi kujitoa kwenye kitu ambacho hujaingia ?

usitutukane wana udom na shule za kata wapo maproccm pia wapo wanamageuz, be specific and not general. Tupo pa1.
 
Kwani kipi hakiwezekani; (1) Tanzania bila Zanzibar. (2) Tanzania bila Tanganyika.
 
maxresdefault.jpg


31/08/2013

Mwanaharakati Maarufu Bw Mohamed Riami (Eddy Riami) ametangaza kujiondoa katika Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza katika Kongamano lililotayarishwa na Kamati ya Maridhiano, hii ilikuwa strong speech iliyowahi kutolewa na Bw Eddy Riami amesema yeye sio mwanasiasa, akiwafananisha na Jusa na Mzee Moyo. Bali yeye ni raia kama walivyo raia wengine.

Amewataka Wazanzibar kujitolea kutafuta heshma zao na nchi yao.

Alisema kwamba ni wao ndio waliompigia kura Rais kwani Rais mwenyewe hakupiga kura katika uchaguzi uliopita. Hivyo anajuwa vipi Zanzibar itashinda kabla ya mwaka 2015. Alikuwa akikariri moja ya hotuba ya Mzee Karume alpokuwa anakadiria kuwa Zanzibar haihitaji uchaguzi
hadi baada ya miaka 50.

Ametaka suala la siasa litolewa katika katiba mpya. Vilevile amewataka viongozi wengine kuachana na siasa badala yake kupigania Zanzibar nje ya siasa. Kwani ni siasa ndio iliyoifikisha hapa Zanzibar.

Eddy Riyami who, What, how much? So what?
 
wapeni nchi yao wenyewe hataki tena watanganyika tumekuwa hatuna aibu utadhani nyani,hamna hata mzanzibar mmoja anae taka muungano kwa sasa wanao pigania muungano ni hao viongozi ambao wako serikalini na wanafanya hivyo sababu ya matumbo yao,kwanini isipigwe kura ya maoni zanzibar,serikali inajuwa kabisa kama itapigwa kura ya maoni zanzibar hawawezi hata kupata zaidi ya watu 100 wanao taka muungano kuwapo,waachieni nchi yao bhana

Hata mzee wa lambalamba Bakhresa na wenzake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Someni ALAMA za WAKATI - Muungano wa serikali mbili hauwezekani. Kwa kejeli za CCM, wataadhirika mwaka huu. Huku zanzibar, mambo yako wazi kabisa ndio maana CCM wanatumia vitisho. Lakini, ni vitisho vya nyau hivo. Wazanzibari wamekwisha fanya maamuzi. Kosa kubwa wanalolifanya CCM ni kujaribu kuzima sauti za wazanzibari. Kuwafunga viongozi wazanzibari na kuwaekea mashitaka ya kubuni wazanzbari wenye kuitetea nchi yao. Kwa ufupi, munashuhudia kifo cha chama kikuu Tanzania.
 
Kwa mwendo huu, CCM Zanzibar itabaki kwenye vitabu vya historia tu!
 
hivi mi nashangaa hawa viongozi,kwann wanawang'ang'ania lkn si wawaachie nchi yao jamani?
..tied of this
 
Aise, kweli nimekumbuka bwn, Shein ndiye rais pekee duniani ambaye hakujipigia Kura, kumbuka kituo chake kilikua Dar na sio Zanzibar and Dar kama sehemu ya Tanganyika, uchaguzi wa Zanzibar haukutuhus.

No wonder hawataki mambo yao yaamuriwe Dododma!!
 
wapeni nchi yao wenyewe hataki tena watanganyika tumekuwa hatuna aibu utadhani nyani,hamna hata mzanzibar mmoja anae taka muungano kwa sasa wanao pigania muungano ni hao viongozi ambao wako serikalini na wanafanya hivyo sababu ya matumbo yao,kwanini isipigwe kura ya maoni zanzibar,serikali inajuwa kabisa kama itapigwa kura ya maoni zanzibar hawawezi hata kupata zaidi ya watu 100 wanao taka muungano kuwapo,waachieni nchi yao bhana


wewe usiongee kitu ambacho hukijui,jaribu kuwauliza vizuri wazanzibari wote wanaoishi huku bara na kule kwao utapata jibu,mtu asie jua kitu wala haoni faida yake lakini wanaofahamu na kujua matumizi yake wanaona umuhimu wa muungano so usiropoke bila kufanya research.
 
Back
Top Bottom