Zanzibar: Eddy Riyami atangaza kujitoa CCM

Zanzibar: Eddy Riyami atangaza kujitoa CCM

Kakke

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2010
Posts
1,883
Reaction score
1,482
maxresdefault.jpg


31/08/2013

Mwanaharakati Maarufu Bw Mohamed Riami (Eddy Riami) ametangaza kujiondoa katika Chama Cha Mapinduzi.

Akizungumza katika Kongamano lililotayarishwa na Kamati ya Maridhiano, hii ilikuwa strong speech iliyowahi kutolewa na Bw Eddy Riami amesema yeye sio mwanasiasa, akiwafananisha na Jusa na Mzee Moyo. Bali yeye ni raia kama walivyo raia wengine.

Amewataka Wazanzibar kujitolea kutafuta heshma zao na nchi yao.

Alisema kwamba ni wao ndio waliompigia kura Rais kwani Rais mwenyewe hakupiga kura katika uchaguzi uliopita. Hivyo anajuwa vipi Zanzibar itashinda kabla ya mwaka 2015. Alikuwa akikariri moja ya hotuba ya Mzee Karume alpokuwa anakadiria kuwa Zanzibar haihitaji uchaguzi
hadi baada ya miaka 50.

Ametaka suala la siasa litolewa katika katiba mpya. Vilevile amewataka viongozi wengine kuachana na siasa badala yake kupigania Zanzibar nje ya siasa. Kwani ni siasa ndio iliyoifikisha hapa Zanzibar.
 
Ccm Zanzibaw watashiwa akina Bilali na Shein , Mansuri ana kundi lake akina Amani karume na wenzake.
 
Nape wanalo hilo! CCM ina meguka kila uchwao. Tunasubiria Bukoba kesho!
 
Siasa za waswahili bana ni taaabu kwelikweli ati huyu tapeli naye wanamshangilia,alikula sana utawala wa Karume. Sasa atueleze ile sinema aliyocheza na Msabaha ya kumteka.
Ccm Zanzibaw watashiwa akina
Bilali na Shein , Mansuri ana kundi lake akina Amani karume na
wenzake.
 
huyu ndie Edi Riyammi, kama mnamkumbuka Salim Msabah yule muwakilishi wa mwanzao kujiuzulu CUF na ikawa sakata kua ametekwa inasemekana huyu jamaa alihusika kwa maslahi ya CCM.
Edi Riyyami.jpg
 
Mansoor , Mzee Moyo, Jussa na kundi lao, lina nguvu sana na linakubalika na wanzanzibar wengi. Hao jamaa ni vichwa na wanauchungu na nchi yao, kama CCM haitatumia Green guards kuua watu, 2015 nje
 
haka kawilaya ka Tanzania kana makeke sana
 
huyu ndie Edi Riyammi, kama mnamkumbuka Salim Msabah yule muwakilishi wa mwanzao kujiuzulu CUF na ikawa sakata kua ametekwa inasemekana huyu jamaa alihusika kwa maslahi ya CCM.
Kwahiyo ndiokusema alimpotosha mwenzake yaani Msabaha alafu yeye anarudi alikokuwa Msabaha?Hapo Msabaha atajisikiaje?
 
Huo ni msumari kwa CCM na wasipokaa sawa huo ndo mwisho. Hali inayojitokeza ndani ya CCm ndiyo dira ya 2015, nasi tunaendelea kuiombeaMIZIMU yao iendelee kuwavuruga na mwisho wa siku kitaeleweka.
 
wapeni nchi yao wenyewe hataki tena watanganyika tumekuwa hatuna aibu utadhani nyani,hamna hata mzanzibar mmoja anae taka muungano kwa sasa wanao pigania muungano ni hao viongozi ambao wako serikalini na wanafanya hivyo sababu ya matumbo yao,kwanini isipigwe kura ya maoni zanzibar,serikali inajuwa kabisa kama itapigwa kura ya maoni zanzibar hawawezi hata kupata zaidi ya watu 100 wanao taka muungano kuwapo,waachieni nchi yao bhana
 
Hivi aliyetulazimisha kuungana ni nani?

"Nchi ngumu hii"
 
Aise, kweli nimekumbuka bwn, Shein ndiye rais pekee duniani ambaye hakujipigia Kura, kumbuka kituo chake kilikua Dar na sio Zanzibar and Dar kama sehemu ya Tanganyika, uchaguzi wa Zanzibar haukutuhus.
 
Back
Top Bottom