Zantel waondoa huduma ya GPRS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zantel waondoa huduma ya GPRS

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Tumsifu Samwel, Dec 12, 2009.

 1. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #1
  Dec 12, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Zantel wameondoa huduma ya GPRS kuunganisha kwenye computer, ni wiki ya pili sasa najaribu kutumia simu yangu kuunganisha internet kwenye laptop yangu bila mafanikio yoyote.

  Kila nikiunganisha ina connect ikifika sehemu ya kuregister kwenye computer ina goma na kuniletea meseji "subscribe to packet data first" ingali configuration setting za zantel zipo na siku zote ndizo ninazo tumia kuunganisha huduma ya internet kwenye computer yangu. Leo nimewapigia simu zantel kitengo cha huduma ya Internet na kuwaambia tatizo langu wakanijibu kuwa "Zantel hiyo huduma ya kutumia simu kuunganisha na computer upate huduma ya internet tumeiondoa kwa sababu watu wengi wanatumia isivyo takiwa, hiyo huduma tuliitoa kwajili ya matumizi ya ndani ya simu tu na sio kuunganisha hiyo hudumu kwenye laptop or desktop, hivyo hutoweza kuunganisha tena hiyo huduma kwenye laptop yako zaidi utatumia ndani ya simu tu… kama unataka huduma ya Internet kwenye laptop yako njoo ofisini kwetu ununue modem"

  Hayo ndio majibu kutoka kwa custormer services wa zantel ambayo yameniacha hoi!

  Napenda kuwauliza wadau wengine je na nyie mmekumbana na tatizo kama hili?
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Dec 12, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Pole sana, mimi situmii huduma zozote za Zantel lakini sioni logic ya kusema kwamba watu wanatumia huduma hiyo isivyo! Huduma ya kutumia simu kama modem si wateja wanaitumia kulingana na maelekezo yao Zantel au mteja ana uwezo wa kufanya configuration atakavyo? Au wanataka kumaliza stock ya modems walizo nazo?
   
 3. Mutensa

  Mutensa JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2009
  Joined: Feb 20, 2009
  Messages: 426
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huo wanaofanya ni ushamba kama ni kweli. Wao kama wafanya biashara wanachotakiwa kujali ni Bytes downloaded/uploaded na sio kifaa ulichotumia kudownload. Isitoshe hamna tofauti kiufundi kuvuta data kwa simu au kwa modem.
   
 4. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Pesa ni ile ile na mb zilezile ni uhuni tuuuuu
   
 5. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Unajua matatizo mengine ni mpaka upeleke simu au moderm offisini kwao kule ndio kuna wataalam,

  mimi natumia modem ya Zantel wako vyema saana na haina matatizo yoyote kabisa.
  .
   
 6. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #6
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ThinkPad, na kubaliana na wewe kuwa Zantel ni wazuri kwenye huduma ya mtandao, custormer care aliye nipa hayo majibu ali lielewa tatizo langu vizuri ndio maana akanipa hayo majibu... Kama mdau alivyo sema hapo juu ni kwamba inaonekana wanataka kumaliza stock ya modem zao, maana hii huduma ya kutumia simu kama modem inatumika duniani kote cha kushangaza zantel wameindoa.
   
 7. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  ngoja nijarbu kuwacheki kesho ntakupa jibu kama wametoa au lah
   
 8. Inteligence

  Inteligence Member

  #8
  Dec 13, 2009
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani ni configuration tuu zimesumbua ktk laptop yako:

  Elewa Modem/data cards=phone ktk data/GPRS(General Packet Radio Servc for 2g,HSDPA-High Speed Downlink Packet Access for 3g.

  Hata ukiconnect modem yako kwenye laptop then ukipiga simu kwenye hiyo line ya kwenye modem itaita...vivyo ,hivyo kwenye sms.

  SOLUTION:Inalekea ports zina problem au some setting---FANYA system RESTORE mpka tarehe ambapo hiyo modem ilikuwa inafanya kazi then 100pcent itafanya kazi.

  Just go to Start--then Help and Support--click Undo changes to your computer by system restore.ikimaliza isipofanya kazi -----basi nipe jibu.

  Asante
   
 9. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #9
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Shukran mkuu...
   
 10. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #10
  Dec 13, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu Inteligence, Asante kwa maelezo yako mazuri,hizo option zote nimezifanya na hata kwenye simu nimefanya hivyo maana uwa kila mwezi nafanya backup kwenye simu yangu... Pia configuration setting hizo hizo za zantel nikiweka line yaTigo/voda na Zain zina fanya kazi bila tatizo lolote,tatizo lina kuja kwenye zantel kila niki-connect ina niletea hii message "subscribe to data packet first" ingali configuration setting za zantel zipo.
   
 11. Inteligence

  Inteligence Member

  #11
  Dec 13, 2009
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Itabidi wa inaelekea kuna problem kwenye Core Network yao(either SGSN-serving GPRS support node,GGSN,billing etc
   
Loading...