Zantel msitafute mchawi

Gudboy

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
867
77
Mimi ni mmoja wa mtumiaji wa huduma ya internet ya zantel (Zconnect) tangu walipoanza kuleta modem zao. Kubwa zaidi nilijiunga kuwa mteja wa high life. Hivyo nilikua najiunga na kifurushi cha wiki kwa sh. 10,000, hivyo kwa mwezi ni sh. 40,000. Hivyo nilikua na line ya zantel kwa ajili ya kusaidia huduma hii kama jinsi inavyotakiwa. Na line hiyo sikuwa naitumia kwa ajili ya kupiga simu bali kwa internet tu. Na sio mimi tu hata watu wengine ambao wanazo line hizo ni kwa ajili hiyo.

Sasa tatizo limeibuka juzi wakati nataka kujiunga na kifurushi cha wiki, ikaja meseji kuwa siwezi kujiunga mpaka line yangu iwe imetumia sh. 5,000/= kupiga simu ndani ya siku saba zilizopita. Nikatafuta line ya mtu mwingine naye ikaja na meseji hiyo hiyo. Na jamaa wengine pia wakalalamika juu ya suala hili.

Sasa napenda kuwaambia zantel kuwa biashara yao wanaiua wao wenyewe na walawasitafute mchawi, sasa kwa kunilazimisha kwa wiki nitumie 5000 kwa ajili ya kupiga simu ili nipate nafasi ya kujiunga na huduma ya internet hapo mmechemsha kabisa. Kwa mantiki hiyo mnanitaka kwa wiki nitumie 15,000 na mwezi ni 60,000? Mmenikosa kote kote sasa na pia sio mimi tu na wengine kibao watawakimbia. Maana huduma ya interent ni internet haihusiani na mimi kupiga simu.

Pia mnajua kabisa ya kuwa huku Tanzania bara walao mmeweza kupata wateja kwa ajili ya Internet, maana hakuna anayetumia zantel kwa ajili ya simu ni asilimia chahce sana, ukiondoa TIGO, AIRTEL na VODACOM ninyi hamna wateja wa kupiga simu. Sasa mnaamua kutulazimisha kwa kupitia internet. Sasa nakufahamisheni ya kuwa mmenikosa kabisa nitanunu merm nyingine tena ni bei nafuu kabisa.

Hiki ni kipindi cha ushindani wa biashara ndio maana huduma zinapungua, sasa ninyi badala ya kupunguza ndio mnaongeza ilhali mnaona makali ya maisha jinsi yanavyowaumiza watanzania tulo wengi, na ndio maana tunaangalia wapi kuna unafuu ndio tunakimbilia. Nina uhakika msipojirekebisah kwa hili wateja wengi watawakimbia. Nina jamaa zangu zaidi ya 10 waliopata tatizo hili na kuanzia sasa watawakimbia kabisa.

Ni hayo tu. Pia hapa JF kama kuna mtu anayetumia internet ya Zantel atoe maoni yake hapa kuhusu huku kulazimishwa kupiga simu
 
mkuu .. nenda kwenye jukwaa la business and economy utakuta hii thread ya zantel imepamba moto ..... wahi huko
 
pia wapaswa nunua line ya CDMA, hii ni kwa ajili ya internet tuu. ukitumia line ya GSM ndiyo matatito kama hayo yanatokea. wao zantel watakuchukulia ni mtumiaji wa simu na internet na ndiyo maana wamefanya hivyo. HUU NI MTAZAMO WANGU KUTOKANA NA UZOEFU NA HAWA ISP.
 
Back
Top Bottom