VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Zamu ya kuahidi halafu kupoteza ushahidi.Kuahidi kupambana na rushwa ndani ya CCM yetu halafu kuishia kupongeza wagombea watakaopita kwa rushwa. Zamu ya kuwainua mikono juu wagombea watakaopenya kwa mlungula huku wakipigiwa chapuo ya kushika nyadhifa tamutamu nchini.
Imefika zamu yake. Zamu rasmi ya Comrade Phillip Mangula, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Taifa. Mangula ameahidi rasmi kuwa atakula sahani moja na watoa na wapokea rushwa ndani ya CCM hasa wakati wa kura za maoni. Kura za maoni ya Urais, Ubunge na Udiwani. Ni hapo mwakani. Mwaka wa uchaguzi mkuu nchini.
Wagombea watarajiwa wameshajindaa. Wamekusanya mamilioni yao kwenye sandarusi kuingia kwenye mchakato wa kura za maoni na uchaguzi mkuu wenyewe. Wako tayari kuuza nyumba, magari, mashamba na rasilimali zao nyingine kupata mamilioni ya uchaguzi. Tayari kushindana na kushinda.Tayari kufa au kupona.
Comrade Mangula ametangaza wakati mzuri. Wakati ambao maandalizi yanafikia ukingoni ili mechi ianze. Wakati ambao mbinu mbivu na mbovu zitatumika kupatikana kwa ushindi chamani na uchaguzini. Waliomtangulia Mangula katika kauli kama yake walishindwa kuisimamia na kupata ushindi kwa kauli na matendo yao.Kuvua gamba kukapotelea gizani.
Comrade Mangula ataweza kukomesha rushwa ndani ya CCM uchaguzini? Tusubiri tuone na kusikia!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam