Mimi siishi Tanzania, ila naishi hapa old Europe kwa miaka mingi sasa tayari nina wajukuu hapa ila napenda sana makala zako na post zako ningependa sana tuongee, sababu pia unaandika kiswahili cha misamiati mizuri, napenda watoto wangu na wajukuu zangu wajue kiswahili, bado nawafundisha kwa kutumia vitabu vya Bulicheka, kama wimbo wa kisichana chini ya mti alisuka kitunga, na Maganga hodari kavuka ziwa nyasa, lakini wewe nakuona upo vizuri sana kwenye kiswahili na misamiati yake.pia muda mwingine natumia vitabu vya mzee mmoja pale chuo kikuu yule mwingereza aliye amua kuwa mbongo makengeza jina kama hilo yupo kitivo cha lugha. ningeomba ni beep tuongee bado nitaweka jina lako anoniem.