Zamani chombo au kifaa imara kiliitwa Madee

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,252
21,345
Mambo yanaenda kasi sana!

Miaka ya 1970- hadi 1980!, Chombo chochote imara waliita madee yaani (Made in China)

Wakati huo kulikuwa hakuna beseni Bali yalikuwepo makalai, wakati huo kulikuwa na ndoo za chuma ambayo ukiitua vibaya inakata vidole vya mguu!

Kipindi hiko wembe mmoja ulikuwa unaweza kunyolea hata watu 10 yaani nywele za familia nzima!

Kikombe cha mchina kipindi hiko kiliwekwa rasmi hadi mgeni wa heshima aje ndipo kitolewe! mfano mwalimu au padri akija utamsikia mama akisema!

Kalete kile kikombe cha MADEE! maanake (Made in China)

Kiufupi Made in China ilikuwa Original kupita maelezo!

Kipindi hicho kumkuta mtoto wa shule ya msingi kavaa viatu ilikuwa hamna, ni mwendo wa pekupeku hadi walimu!
Miaka ya 80 ndipo zikaletwa chachacha (Saa sita utanikoma)

Hiyo saa sita utanikoma ilikua balaa! Vile viatu wakati wa Jua viliunguza miguu hatari sana!
Wakati ule pia kina mama walipendelea kuvaa magauni ya madoadoa! Ndani walitanguliza sketi nyepesi iitwayo Anda!

Kipindi hicho mwanaume ukiona tu yale marinda ya Anda yamechomoza kwa chini! Aiseeeeh! Tena usiombe Anda yenyewe iwe nyeupe! Hakiyanani daah!

Kwanza mbali na kuchomoza, kipindi hicho ukiikuta Anda Imefuliwa na kuanikwa! Ubongo unavurugika!

Lakini sahivi mtu anavua dera, anabakisha taiti anaonekana wa kawaida, akitoa Tait ibaki chupi bado holaa, haya tufanye avae zile tandabui kama barakoa lakini napo holaaa! Yaani mpaka ajimanue hivi ndo watu waamka dah!

Ukitafakari; Sijui ni wapi tulipojikwaa hadi tumekuja kuangukia kwenye ufeki huu!

Sahivi ukisikia neno Mchina! Kuna mawili kama siyo makalio feki basi ni bidhaa feki!

Noma sana.
 
Kwenye michuano ya Netball makundi ya wanaume yalikua yanahudhuria viwanjani sio kuona mchezo bali kupiga "chabo" mini skirts za kina dada wanaocheza. Mapaja ya KE yalikua hayaonekani hovyo barabarani atii🤪
 
Kwenye michuano ya Netball makundi ya wanaume yalikua yanahudhuria viwanjani sio kuona mchezo bali kupiga "chabo" mini skirts za kina dada wanaocheza. Mapaja ya KE yalikua hayaonekani hovyo barabarani atii🤪
Weeeh noma Kabisaa!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom