Zama hizi tunawahitaji Great Thinkers

Joshua justine

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
792
1,007
Wasalaam wadau,

Jamani tupo katika zama mbaya sana kisiasa katika taifa hili, imekuwa ni mabishano ya vurugu tupu bila hoja zenye misingi.

Huyu anasema hivi yule anasema hivi na hakuna anaekubali kwamba hoja ya mwenzake ina mashiko zaidi ya hoja yake, hii sio sifa ya great thinkers.

KWA UFUPI SANA HATUA ZA GREAT THINKERS

1. KUELEZEA TATIZO( Analysing an Issue)

Kama huna uwezo wa kuliona tatizo katika undani wake, na kulieleza vizuri kwa wenzako ambao hawajaliona bado ili nao wakubaliane na wewe kwamba hilo ni tatizo basi hapo haupo katika utaratibu na sifa za great thinkers.

(a) great thinker , kwenye forum kama hii anaweza akaleta jambo aliloliona na yeye mwenyewe pia akaja na ushauri namna ya kulishughulikia

(b) lakini pia, kwa jukwaa kama hili great thinker mara nyingine anaweza akaleta jambo na kuamua kuwapa uwanja wadau / great thinkers wengine walichambue na kulimalizia kwa hatua zinazofuata.

2. KUTAMBUA MISINGI YA HOJA ZAKO( Identifying your Premises)

Ni lazima ujue misingi ya hoja zako utakazozileta kama majawabu. Hii inakuwezesha kuzijenga hoja zako kwa kina na kieleweka hata na watu waliokuwa na mitazamo tofauti hapo awali, baada ya kukusikia wanaweza kubadili misimamo yao na mitazamo yao baada tu ya kukusikia.

3. KUJENGA HOJA ( Synthesizing your Premises)

Hatua hii ni ya kuelezea kwa kina hoja zako , moja ikifuatia nyingine , moja ikibeba nyingine mpaka utoe picha kamili ya kimtazamo kwa watu wanaokusikiliza na hakuna mtu atakaekubishia ukiwa umeenda vizuri kwa hoja za ukweli, ukweli haupingwi ila watu wanaweza kukataa tu kwa kiburi chao ila kuupinga hawataweza.

4. KUHITIMISHA HOJA ZAKO( Conclusion)

Katika kujenga hoja zako, hoja juu ya hoja, hatimae hoja zako zimebebana na kushirikiana kufikia wazo kuu moja lililokusudiwa awali

Kiufupi ulikuja na wazo kuu lakini ulipaswa ulijenge kwa hoja mpaka likubarike, liwe wazo litakaloitwa ukweli, kwa kutumia hoja zako. Hapo sasa unaruhusiwa kuliweka chini wazo hilo nalo likakubaliwa.

JE SIKU HIZI BADO JF TUNA MAGREAT THINKERS, AMA KILA MTU ANAAMUA TU KUWA ""SITAKI HOJA ZAKO"", HATA KAMA MOYONI ZINAMSUTA

TUKUMBUKE KUWA MTU ANAPOONGEA UKWELI NA KUUJENGEA HOJA , HUYO MTU YEYE SIO UKWELI ILA AMEFANIKIWA TU KUISHI NA UKWELI NDANI YAKE, UKIKATAA HOJA YA HUYO MTU HUMKATAI YEYE BALI UNAKATAA HUO UKWELI NA UKWELI UPO KILA SEHEMU NDANI YA VIUMBE HAI NA NJE YA VIUMBE HAI. UNAPOKATAA UKWELI UNAJITENGA WEWE KAMA WEWE NA UKWELI , NA USIJIDANGANYE KAMA UMEMSHINDA MTU FULANI, BALI UMEJITE GA WEWE NA SIFA INAYOUMBA VITU VYOTE HAI NA VISIVYOHAI , SIFA HIYO NI UKWELI.
HATUTAWEZA KUANDIKA KATIBA MPYA KABLA WATU HAWAJAJIFUNZA KUTAMBUA UKWELI NA KUJENGA HOJA SIO KUBISHANA TU KAMA WATOTO , HIYO KATIBA ITAJAA MABISHANO YA KITOTO YENYE MASLAHI BINAFSI NA SIO HOJA ZA UKWELI , UKWELI AMBAO UNAWEZA KUISHI MILELE HATA VIZAZI BINAVYOKUJA VIKAUHESHIMU NA KUUTUMIA.

Hakuna anayefanikiwa kwa kuupinga ukwwli, ," you cant live a lie" !!!
 
Tabia haijenhwi siku moja!!
Hata mlevi hakuanza siku moja, wala mzinzi wala mwizi ,
Sasa kwa nn tusianze moja leo kuamua tutafuata tafakuri za kina juu ya kweli sio wakati wa mizaha tunapotaka kuweka jambo zito na la muhimu kama katiba mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom