Zainabu Kawawa

Zainabu Kawawa

Tunakuta akina nchemba wakijibu hoja kwa kejeli na kuwaaacha akina mzee wasira wajizolee umaarufu kwa kuingia ktk hoja zote kwa hekima na siasa ya juu sana.....tuzalishe wabunge watakaoikosoa serikali na kuisaidia serikali na siyo mabwana/mabibi wakubwa kisa eti watoto wa waasisi ...hii hapana

Mimi nimeipenda signature yako tu!:israel:
 
Ndiyo matatizo ya hivi viti maalum aka vya kizinzi, yaani hawa wote au haya yule chei chei shangazi Vailet mzindakaya kwanza hawana hata sifa za maadili za hata kuwa monita au mjumbe wa nyumba 2, mbunge mzima anageuzwa-geuzwa ktk magari, mara ktk vichochoro unadhani hata wanajua wanachokisema ? mwigulu anawatafutia vipoint uchwara ili mradi waonekane wanaongea...maana hiyo inaweza wapatia soko jipya..

Nilisikia zile points za yule kijeba, mbunge wa namtumbo Kawawa nikabaki hoi. Halaf nae eti yupo ktk ile kamati ya bunge ya Lowassa, mambo ya nje sijui na ulinzi na usalama.... yaani hii inji ya Dhaifu ina vituko kweli !
Sjui ni mimi peke yangu ninayepata shida na aina ya michango ya hawa watoto wa marehemu Mzee Kawawa. Wanaongea vitu vya hovyo sana. Week iliyopita kama mtu-Vita Kawawa alikuwa anasema hakuna shida na deni letu na kuna wakati akalinganisha na level ya madeni ya Marekani na Japan! Leo hii dada mtu anasema kitendo cha Tanzania kualikwa kwenye G8 ni heshma kubwa!

Ukiangalia nchi zinazounda G8 zote zina maslahi Tanzania. Kilichofanyika pale ni uchief-Mangungo na hawa watoto wangejishughulisha kusoma wangejua sio jambo la heshma kama ambavyo wanadai. Nchi kama Brazil, India, South Africa na China etc zimeunda umoja wao- BRICKS, wanaona kabisa G8 sio mahali pao. Kusema tushangilie kuitwa G8 ni sawa na kusema mama ntilie afurahie kuitwa kwenye kikao cha Bakheresa na Mengi! Ni dhahiri huyu mama ntilie atajikita zaidi kuomba na lazima a-trade off something. Sisi tume-trade off nini hawa big boys?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom