KELVIN GASPER
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 1,066
- 454
baada kuzimiwa mic akanongona dakika kumi hazitoshi.
hango wa mbunge waAnapanua mapafu kupigia kelele kilimo lakini hajui ABC za kilimo! bila zana(machinery) mfumo wa umwagiliaji(irrigation systems) mbegu bora ( improved seeds) pembejeo ( mbolea, madawa) watalaamu na utafiti na huduma za ugani processing industries, masoko access to credit systems n.k kilimo kitabakia kuongelewa kama agenda ya kisiasa kila mwaka, hakuna mtu mwenye nia ya dhati ya kuimarisha kilimo! ukizungumzia kilimo zungumzia kwanza wizara imetengewa kiasi gani na mchanganuo upoje lakini kupanua mapafu tuu wala haina tija, huyu mama angekuwa ni mdau kweli wa kilimo kwenye bajeti kuu angepinga hadi kilimo kitengewe pesa ya kutosha! she is a mediocre!!
mbona hoja zake na kimo chake vinaendana.mie nadhani ni wakati muafaka kwa wabunge wa mikoa ya kusini kuchangia kwa kuibana serikali kupeleka maendeleo kusini kuliko kupoteza kwa kusifia jk kualikwa G8.
kweli huyu jamaa amegusa pale penyewe nilimsikia na nampongeza sana maana amezungumzia hata Benki ya Kilimo inayoanzishwa! wakulima wameandaliwaje kukopesheka? taratibu za mikopo zimeandaliwa? benki itakuwa wapi? darau kwenye mikoa au vijijini walipo wakulima haya ndio mambo ya kuzungumzia unapotaka kunuia wakulima na kilimo!hango wa mbunge wa
mkuu nimeupenda sana mchango wa mbunge wa Gairo Mh Shabib kuhusu economics za ku own mchinery na hususan tractor - huwezi ukau categorise mkopo wa tractor katika very short run to short run unless kama utauza "unga" ndo upate hela ya kurejesha mkopo katika kipindi hicho. ni kama unamkopesha mtu apande kahawa ambayo inakuja anza kuzaa miaka minne na unamwambia arudishe mkopo wote mwaka wa pili. Pia kazungumzia pembejeo ambazo ugawaji wake umejaa mizengwe sana. Mbunge huyu anapozungumza unaona kabisa anaishi na kuwafahamu wakulima kwa kina sana. tatizo inaelekea wengi wanatoka kwenye rami na kuingia bungeni - type ya kina mh dr Mzindakaya inaendelea kupotea bungeni.
Sjui ni mimi peke yangu ninayepata shida na aina ya michango ya hawa watoto wa marehemu Mzee Kawawa. Wanaongea vitu vya hovyo sana. Week iliyopita kama mtu-Vita Kawawa alikuwa anasema hakuna shida na deni letu na kuna wakati akalinganisha na level ya madeni ya Marekani na Japan! Leo hii dada mtu anasema kitendo cha Tanzania kualikwa kwenye G8 ni heshma kubwa!
Ukiangalia nchi zinazounda G8 zote zina maslahi Tanzania. Kilichofanyika pale ni uchief-Mangungo na hawa watoto wangejishughulisha kusoma wangejua sio jambo la heshma kama ambavyo wanadai. Nchi kama Brazil, India, South Africa na China etc zimeunda umoja wao- BRICKS, wanaona kabisa G8 sio mahali pao. Kusema tushangilie kuitwa G8 ni sawa na kusema mama ntilie afurahie kuitwa kwenye kikao cha Bakheresa na Mengi! Ni dhahiri huyu mama ntilie atajikita zaidi kuomba na lazima a-trade off something. Sisi tume-trade off nini hawa big boys?
Hilo ni gamba lingine limejipenyeza ndani ya JF.Mawazo mgando ndio unao wewe na chama chako na mumeshaligharimuhayo ni maono yako! ulipaswa kuyatoa kwa lengo la kujenga na si kulihusisha na chama, pili nakubali kuwa watu wenye fikra mgando kama wenye mawazo yako mpo wengi na wakati mwingine mnaweza hata kuligharimu taifa?
Maskini kawawa alikuwa ni mwadilifu asiye na makuu katuachia mitoto zuzu yasiyokuwa na msimamo mitoto inatembelea NYOTA ya baba yao lakini bado haibebeki jina la MZEE KAWAWA linaweza kufutika nakudharaulika sababu ya hii MITOTO VILAZA.
Mkuu hapo unagusa interest za watu bana! hao vitu maalumu za Chama Cha Mapenzi vipo kwa kazi maalumu!