Zain yawapiga nzito fitna TTCL! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zain yawapiga nzito fitna TTCL!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MziziMkavu, Jun 6, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Kampuni la simu za viganjani la Zain inaipiga vita Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) katika mpango wake wa kupanua huduma za simu za mkononi. Tayari makao makuu ya Zain imeiandikia barua Serikali ya Bongo ikiitaka iachane na mipango ya kuisaidia mijihela TTCL ili kuboresha huduma zake, ikiwamo hiyo ya simu za mkononi. heheeee fitnaaaa

  TTCL ni kampuni inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania ambayo imeingia ubia na kundi la kampuni za Zain ambapo Serikali inamiliki asilimia 65 wakati Zain ambayo awali ilikuwa Celtel inamiliki asilimia 35.

  Kwenye barua hiyo , ilielezwa kuwa Zain hawafurahishwi na hatua ya TTCL ya kuwa na huduma ya simu za mkononi na inatamka wazi kuwa haiungi mkono upanuzi wa simu za mkononi za TTCL kutokana na mgongano wa maslahi uliopo kutokana na Zain kufanya biashara kama hiyo.

  Ilifafanua kuwa nia hiyo ya Serikali inaifanya Zain ikose namna nyingine ya kuachana na kujihusisha na TTCL hasa kwenye mpango wa kupanua huduma za simu za mkononi za TTCL. Kwa barua hiyo ya Zain ni wazi kuwa wabia hao hawataki TTCL iendeshe biashara ya simu za mkononi; badala yake wanataka iendelee na biashara ya simu za mezani.

  Katibu Mkuu Hazina, Ramadhan Kijjah, alikiri kupokea barua ya Zain ikiitaka Serikali ijiondoe katika kuiunga mkono TTCL ili ijitanue kwenye mtandao wa simu za mkononi.

  “Ni kweli hiyo barua nimeipata, lakini ninachoweza kukwambia ni kwamba sisi wizara hatuwezi kuchukua uamuzi wa kujiondoa hadi tutakapopata ushauri wa kitaalamu kutoka Wizara ya Miundombinu,” alisema Kijjah.

  Aliongeza kuwa wizara ya Miundombinu ndiyo yenye jukumu la kusimamia mambo ya kiufundi ya kampuni ya simu wakati Wizara ya Fedha ilishughulika na mambo ya fedha. Alipoulizwa sababu ya Zain kupinga Serikali kuiunga mkono TTCL huku wote wakiwa na hisa, Katibu Mkuu huyo alijibu: “Hayo masuala yatajibiwa vizuri pale tutakapopata ushauri wa wenzetu wa Miundombinu.”
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hili swala ni gumu kidogo, maana kutumia kodi ya wananchi kuisupport kampuni ambayo inashindana na kampuni zengine kunakuwa kunaharibu ushindani.
  Yaani TTCL inaweza ikashindana hata kwa hasara kwa sababu hawategemei faida ya biashara, bali wanapata msaada wa kodi.
   
 3. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2009
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Yaani BEPARI NI BEPARI TU....! mnashindwa kufurahia TTCL kupewa sapoti na serikali ambayo maana yake itakuwa inawajali watu wa chini wasio na kitu bali mnajipigia debe ninyi mlio nacho....?
  NASHINDWA KUWATOFAUTISHA NA WABUNGE WANAOOMBA NYONGEZA YA MISHAHARA HUKU HALI ZA M-TZ WA KAWAIDA NI CHINI......!
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Jun 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Tulio nacho akina nani?? Hii nchi si inafuata mfumo wa capitalism au nimekosea? Sasa serikali ikianza kuharibu free market mambo yataendaje? Tena hii ni sekta yenye ushindani mkubwa teyari hakuna haja ya serikali kuleta ushindani artificial.

  Kweli TTCl inabidi waweke mkazo kwenye landlines, maana bei yake imekuwa juu sana, nchi za watu unapiga unlimited local/long distance calls na pia waweke mkazo kwenye Broadband internet kwa bei inayoeleweka kama wanataka kutusaidia watanzania.
   
 5. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Yes, TTCL wasiwe wavivu wa kufikiri na kuamua kurukia mobile telephony ati kwa kuwa wameona Vodacom, Zain na tiGO wanakula bingo.

  Binafsi nawakubali sana Vodacom maana walionesha u-visionary na ujasiriamali wa hali ya juu kuja kuwapiga kikumbo wababaishaji wa TTCL, Mobitel na TriTel enzi hizo na kuliteka soko.

  TTCL walikuwepo siku zote lakini hawakuwa na vision zaidi ya kuendekeza urasimu wa "subiri wahandisi waje kufanya survey" ... "na vifaa hakuna" ... mtu unangojea simu miezi kama unapewa bure vile.

  Kama ndio wanaamka sasa hivi opportunity bomba ya kukazania ni fibre optic cable ya broad band internet.

  Waendelee na strategy yao ya kujenga backbone ambayo itakuwa leased kwa internet service providers wengine kuanzia makampuni ya simu za mkononi mpaka makampuni mengine ambayo yako strictly kwenye internet business.

  Tumeshafanya makosa kwa kuruhusu kila kampuni ya simu za mikononi ijenge minara yake ... matokeo yake miji imejaa minara kila kona ... wakati minara hii ingeweza kuwa consolidated under 3P onwership na makampuni yakalease.

  TTCL wakijikita kwa fibre optic licha ya kula pesa kiulaini tutaondoa pia adha ya kila kampuni kujenga fibre optic line zake na hivyo kuchimba chimba barabara kila saa.

  Kama kuna sekta ambapo ushindani wa kisoko huria kweli unafanya kazi basi ni sekta ya simu za mikononi.

  TTCL kung'ang'ania kuingia huko ni kukosa vision tena ... vision yao inaonekana ni ile ya bahati ya mwenzio ILALIE mlango wazi.
   
 6. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #6
  Jun 6, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Kwa hilo hata mimi nakuunga mkono.

  Tatizo kubwa ya makampuni ya hapa kwetu bongo, serikali ikishakuwa na mkono wake kunakua na uzorotaji katika kila kona, ukianzina huduma mpaka vision ya kampuni.

  Mfano mwingine wa kampuni kama TTCL ambalo haliendi ingawa serikali ina mkono wake ni bank ya NMB.

  Ukweli ni kwamba, ndani ya TTCL kuna ufisadi mwingi sana. Nina wasiwasi hata kama wakipewa huo msaada na serikali hizo hela zitaliwa na wakubwa huko ndani na kamwe TTCL haita weza kuleta ushindani kwenye soko la simu za kiganjani ikiwa bado serikali inamiliki 65%.

  SEACOM wameshaleta fiber optic cable yenye uwezo wa communicate 1.28Tera bits/second. Swali ni - Tumefanya maandalizi gani kupokea hii fiber? Kwa mtazamo wangu nadhani TTCL badala ya kujikita kwenye simu za mkononi, waelekeze nguvu zao kutengeneza backbone ya fiber ndani ya nchi zitakazo tumiwa na makampuni ya telecommunication na ISPs kuboresha na kupunguza gharama za mawasiliano.
   
 7. B

  Binti Sayuni JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 357
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Acheni hizo,Zain (celtel) ndiyo imeifikisha TTCL katika hal hii ngumu sasa. Zain imeitumia TTCL kujiimarisha kimtandao na kifedha, kama walivyobebwa wao waache TTCL wabebwe pia ni zamu yao.
   
Loading...