Zain africa challenge 2010 na vyuo vyetu TZ.


sijakuelwa?yaani wanashindwa kujibu kwa kuwa na tensio wanaonekana kwenye TV??mbona wanaweza kuongea kwa simu?SIJAKUELEWA
 
Bw/Bi. Pareto hoja zako ni maridhawa, ila nakataa hoja yako ya kuwatetea vijana kwa kisingizio cha kupata homa ya quiz. Homa hiyo kwanini waipate wao tu?

Nways, hoja yako kuhusu jamii kukosa mwamko wa elimu ni ya ukweli kabisa. Lakini hatua tuliyoifikia kama nchi ni kuvunjika kwa social and economical structures, hususan suala la kipato. Ktk hali kaa usitegemee chochote kitatengemaa mkuu.
 
Dahh nimekaa natazama kipindi cha Zain Africa challenge kati ya University of Ghana na University of Arusha,kwa kweli ni aibu vijana wetu hawana uelewa wa mambo kabisa yaani wanabaki kubun buni tu majibu...I felt very bad and disturbed

Hiyo ni picha ya elimu yetu Tanzania. Tunapiga soga sana na kupenda njia za mkato kwa kila kitu hata kuandika notisi za darasani na matokeo yake ndiyo hayo!
 
Mi niliswitch channel mara tu kilipoanza..nilijua kwamba kitatokea nini
 
Dahh nimekaa natazama kipindi cha Zain Africa challenge kati ya University of Ghana na University of Arusha,kwa kweli ni aibu vijana wetu hawana uelewa wa mambo kabisa yaani wanabaki kubun buni tu majibu...I felt very bad and disturbed
wajichagulie zawadi wenyewe hapa hao wanafunzi wa Arusha University
 
wote nimewasikia na what you've commented with the university students of tz.
bwana ukwweli ni kwamba elimu zetu za kibongo ni ile ya mtaala ulioachwa na waingereza... wa kumfanya mwanafunzi aje awe mtumikishwaji... na sio mtumiaji wa hiyo elimu aliyo pewa chuoni ( yaani kufanya vitu kwa kujitegemea na sio lazima aajiriwe. so kutokana na hiyo elimu ya kutegemea na kukariri vyuoni mwetu na ndo mana wanachemsha na huo ndo mwanzo lets chect it out.. ni vyuo vichache sana ambavyo kuna watu wenye ufahamu mkubwa na wanatumika sana..sasa ni wakati wizara ya elimu kuangalia na kutathmini nini mstakabali wa wanfunzi hao. si mnaona wa form four...
 
Wanaweza kuipata kama in their school life hawajawahi kusimama mbele ya darasa hata kupresent something. Vyuo vyingi huwa wanapresent final year project only....hasa hasa mainjinia na wanafunzi wa sayansi. Sina habari sana na wafunzi wa arts.....wengine wanaweza kutujuza.

 
Dahh nimekaa natazama kipindi cha Zain Africa challenge kati ya University of Ghana na University of Arusha,kwa kweli ni aibu vijana wetu hawana uelewa wa mambo kabisa yaani wanabaki kubun buni tu majibu...I felt very bad and disturbed
Mbona nimesikia kwenye muhutasari wa magazeti asubuhi kuwa University of Arusha imeingia nusu fainali au ilikuwa geresha? Na kama wameingia watakuwa wameingiaje kwa jinsi mnavyowakandia? Tatizo kubwa la vijana wa siku hizi ni tamthilia za kwenye TV k.v Second chance, Prison break and many others from southern America. Sisi tulikuwa na debate kwa sababu wakati wa jioni kabla ya prep ndo kilikuwa kiburidisho lakini sasa hivi ni TV. Tusiwalamu wao bali tujilaumu sisi wazazi na viongozi tunaowajengea hayo mazingira ya kukesha kwenye TV without even taking a look on his/ her exercise book.
 
Hivi serikali huwa inapitia mijadala Kama hii jaman hapa ndio tungeweza kupata pa kuanzia juu ya uchakavu wa mitaala yetu

Nje ya Mada sijui kigogo huyu n Yule wa kule twitter

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…