Zaidi ya watu milioni 2 wafa kwa COVID-19

Zaidi ya watu milioni 2 wafa kwa COVID-19

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Zaidi ya watu milioni mbili duniani wamekufa kwa ugonjwa wa COVID-19. Takwimu hizo ni kulingana na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins. Vifo hivyo vimetokea wakati ambapo chanjo zinaendelewa kutolewa duniani ikiwa ni kampeni ya kuumaliza ugonjwa huo

Huku takwimu hizo zikiwa zimetolewa na mashirika ya serikali duniani, idadi kamili inaaminikwa kuwa ya juu zaidi kwa sababu ya upimaji duni na rekodi isiyo sahihi ya vifo, hasa wakati wa miezi ya kwanza baada ya kuzuka kwa virusi vya corona.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema idadi ya vifo imekuwa kubwa kutokana na kukosekana kwa juhudi za uratibu ulimwenguni. Guterres amesema sayansi imefanikiwa, lakini mshikamano umeshindikana. Idadi ya vifo hivyo ni sawa na idadi ya watu wa Brussels, Vienna au Mecca
 
kabla ya covid idadi hiyo ya watu walikua wanakufa kwa ugonjwa gani?? vp hayo magonjwa nayo pia wanayatangaza hivyohivyo?? sijui propaganda zitakwisha lini
 
Watuambie, kabla ya Covid, magonjwa yahusuyo mfumo wa upumuaji specifically mafua, yaliua watu wangapi katika kipindi hicho hicho
 
Back
Top Bottom