Zaidi ya watalii 1000 kutoka Israel kutembelea vivutio vya Utalii nchini

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1570784833888.png

Tanzania inatarajia kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka nchini Israel ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii mwezi huu wa Oktoba.

Kundi la kwanza lililokuwa na zaidi ya watalii 200 liliwasili nchini kuanzia tarehe 05 Oktoba na kundi la pili lenye zaidi ya watalii 520 linatarajiwa kuwasili nchini tarehe 12 na kundi la tatu lenye watalii zaidi ya 200 litawasili nchini tarehe 13 Oktoba kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Watalii wengine zaidi wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu baada ya Makampuni ya Uwakala wa Utalii kukamilisha taratibu za safari zao.

Watalii hao wanatarajiwa kutembelea Visiwa vya Zanzibar, Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuitangaza nchi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa kushirikiana na wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi.

Tanzania imejipanga kuwapokea na kuwatembeza watalii hao katika vivutio vya utalii vilivyoko nchini. Serikali inawakaribisha watalii hao kutembelea vivutio hivyo vya utalii ambavyo nchi imebarikiwa kuwa navyo ili wakawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania nchini kwao na kwingine watakakokwenda.
 
... hivi waarabu tofauti na races nyingine sio watu wa kupenda kutalii? Utasikia wachina, wajapan, wazungu, waisrael, n.k. lakini sio waarabu. Waafrika inaweza kueleweka ni maskini ila waarabu ni matajiri wa kutupwa. Bodi ya Utalii ikapige debe Riyadh, Dubai, Amman, Doha, Muscat huko waarabu walete dola nchini.
 
Kundi la kwanza lililokuwa na zaidi ya watalii 200 liliwasili nchini kuanzia tarehe 05 Oktoba na kundi la pili lenye zaidi ya watalii 520 linatarajiwa kuwasili nchini tarehe 12 na kundi la tatu lenye watalii zaidi ya 200 litawasili nchini tarehe 13 Oktoba kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)......

Kesho weka picha ya kundi la pili wakiwasili nnchini.... Itahamasisha watalii wengine pia itathibitisha hii taarifa..
 
... hivi waarabu tofauti na races nyingine sio watu wa kupenda kutalii? Utasikia wachina, wajapan, wazungu, waisrael, n.k. lakini sio waarabu. Waafrika inaweza kueleweka ni maskini ila waarabu ni matajiri wa kutupwa. Bodi ya Utalii ikapige debe Riyadh, Dubai, Amman, Doha, Muscat huko waarabu walete dola nchini.
So wamekodi hifadhi nzima wamejaa waarabu wa uae
 
Kuna watu wakisoma hii habari wanazima simu kwa hasira,wanatoa betri na laini wanatupa mbali.
Viva Tanzania
Viva JPM.
 
Watalii toka Israel 🇮🇱 walianza kuja Tanzania miaka ya 2000 tena wengi walipokelewa na kampuni ya Kibo guides . Ukisoma hii story utafikiri wameanza kuja mwaka huu
 
Watakuja kuangalia ndege za ATCL?! Nilisikia kwamba zile ndege ni zitaongeza watalii, au zinawafuata kutoka waliko?!
 
View attachment 1229573

Tanzania inatarajia kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka nchini Israel ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii mwezi huu wa Oktoba.

Kundi la kwanza lililokuwa na zaidi ya watalii 200 liliwasili nchini kuanzia tarehe 05 Oktoba na kundi la pili lenye zaidi ya watalii 520 linatarajiwa kuwasili nchini tarehe 12 na kundi la tatu lenye watalii zaidi ya 200 litawasili nchini tarehe 13 Oktoba kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Watalii wengine zaidi wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu baada ya Makampuni ya Uwakala wa Utalii kukamilisha taratibu za safari zao.

Watalii hao wanatarajiwa kutembelea Visiwa vya Zanzibar, Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuitangaza nchi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa kushirikiana na wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi.

Tanzania imejipanga kuwapokea na kuwatembeza watalii hao katika vivutio vya utalii vilivyoko nchini. Serikali inawakaribisha watalii hao kutembelea vivutio hivyo vya utalii ambavyo nchi imebarikiwa kuwa navyo ili wakawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania nchini kwao na kwingine watakakokwenda.

Meanwhile wafuga Majini na Mandevu wanatuletea tende na Siasa kali za utengano, Pumbafu
 
... hivi waarabu tofauti na races nyingine sio watu wa kupenda kutalii? Utasikia wachina, wajapan, wazungu, waisrael, n.k. lakini sio waarabu. Waafrika inaweza kueleweka ni maskini ila waarabu ni matajiri wa kutupwa. Bodi ya Utalii ikapige debe Riyadh, Dubai, Amman, Doha, Muscat huko waarabu walete dola nchini.
Hawa utalii wao mara nyingi ni uwindaji! Historia ya maeneo ambao walikaa hapa Tanganyika walikuwa wakiwinda sana na mengi ya maeneo hayo ni yenye tembo mfano Moro, Iringa, Manyoni-Itigi, Tabora na Shinyanga.
 
Ao watalii wote lazima wafike Zanzibar Kwanz den ndio mambo mengind Zanzibar ndio namba moja kwa utalii Tanzania
 
Watalii wanaongezeka bila hata ya Magufuli kutoka kwenda nje ya nchi kuwafuata, amewekeza ndani ya nchi hadi wanakuja wenyewe.
 
Back
Top Bottom