YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,994
Hekari 1000 za mpunga za wakulima wa kijiji cha mkangawalo tarafa ya Mngeta wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro zimeharibiwa vibaya na mwekezaji wa kampuni ya Kilombero Plantation Limited (KPL) inayohusika na shughuli za kilimo cha mpunga wakati akipulizia sumu ya kuua magugu shambani kwake kwa kutumia ndege na kusababisha hasara kubwa kwa wakulima 400 waliolima jirani na mwekezaji huyo.
ITV imeshuhudia mpunga huo ukiwa umenyauka shambani huku wakulima hao wakieleza kusikitishwa na kitendo hicho na kukosa ushirikiano kwa muwekezaji ambapo wamesema tarafa ya Mgeta ikohatarini kukumbwa na baa la nja kutokana na mpunga huo kuharibiwa na dawa hiyo ukiwa bado shambani.
Aidha wakulima hao pamoja na viongozi wa serikali ya kijiji cha Mkangawalo wameiomba serikali kuingilia kati tatizo hilo kwani mashamba yaliyoathiriwa ni mengi hivyo endapo serikali itashindwa kuwasaidia kutatua tatizo hilo ijiandae kutoa msaada wa chakula kwa wananchi wa tarafa hiyo.
Kwa upande wake meneja rasilimaliwatu na utawala wa kampuni ya KPL Bwana David Lukindo akijibu malalamiko ya wakulima hao amekiri kutumia ndege kupulizia sumu ya kuua magugu lakini amesema kampuni ilitumia utaratibu wa kitaalamu kuhakikisha sumu hiyo haiathiri mashamba yaliyo jirani.
Source: ITV
:: Zaidi Ya Hekari 1000 Za Wakulima Wa Mpunga Kilombero Zimeharibiwa Na Mwekezaji