Zahoro Pazzi "aliuzwa" FC Lupopo kabla hajaenda Congo, fedha zikatafunwa TFF

Jeff Gemo

Member
Jul 11, 2015
34
95
1482691074504.jpg

Tanzania kuna mazingaombwe mengi sana katika tasnia ya mpira wa miguu, unaweza usiamini kwamba mchezaji anauzwa na kila document yake ikaenda kwenye timu mpya bila hata yeye kufika wala kuambiwa kama ameuzwa. Ndicho alichofanyiwa Zahoro Pazzi na viongozi wa TFF.. aibu kubwa mtu kama Boniface Wambura kuwa dalali na kujipa uwakala wa mchezaji na kumuuza kinyemela, Wambura akala pesa ya watu ambayo bado wanaidai mpaka leo, Jamal Malinzi lazima anajua na sitashangaa kabisa nikiambiwa na yeye anahusika.

Zahoro anafika Congo anakuta kuna ITC yake, release letter kutoka Simba Sports Club, na kesho yake usiku akakutana na bosi wa timu wajadili suala la mshahara, dogo akashangaa inawezekanaje aongelee mshahara kabla ya kusaini mkataba? Na kwanini waongee mshahara wakati hata hawajaona uwezo wake uwanjani wala hawajamjaribu kwa vipimo wala chochote? Kijana wetu akaingiwa na mashaka makubwa, alienda kwa ndege lakini kurudi alipanda basi la Taqwa.

Zahoro anaeleza kwamba hata alipoamua kuondoka zake baada ya hayo mazingaombwe, viongozi wa FC Lupopo walimfuata Stand na kumpokonya begi lake wanadai anatoroka wakati ni mchezaji wao, wakaleta mpaka askari polisi wa Congo wamkamate Zahoro, kijana akawaambia “kama mnasema mimi ni mchezaji wenu nionesheni mkataba niliosaini nanyi name nitashuka kwenye gari”, hapo sasa wale makondakta na madereva watanzania wakapata nguvu na hivyo wakasema wapo tayari kuchelewa kuondoka Congo mpaka waulete huo mkataba lakini wasimuache Zahoro mikononi mwa wakongomani.

Baada ya kuvutana kwa muda mrefu jamaa wakashindwa kuonesha mkataba, watanzania wakashinda wale wacongoman wakarudisha mabegi za Zahoro na kijana wetu akaanza safari ya kurudi Tanzania akiwa katika hali ya kustaajabu sana kuona ITC yake kule na release letter ya Simba SC ambayo yeye hakuwapa, ni wazi kwamba vilipatikana TFF na Wambura ndiyo aliyocheza huo mchezo “mchafu”, na wale FC Lupopo wanasema wazi kwamba wanataka Wambura arudishe fedha zao hawasemi TFF, hii ina maana kwamba Wambura alifanya kama meneja au sijui baba yake na Zahoro, anajua mwenyewe na shetani wake.

Baada ya Zahoro kurejea akapata timu ya Polisi Morogoro akaingia nao mkataba akidhani yeye ni mchezaji huru, kumbe FC Lupopo na Wambura walighushi mpaka mkataba na unaonekana ni wa miaka mitatu, imagine that! Polisi Morogoro wakaomba ITC wakaambiwa waongee na FC Lupopo, wakatajiwa kulipa kama Dola 5000 za kimarekani ambayo ni ziaidi ya milioni 10 za madafu. Polisi wakashindwa wakainua mikono juu, dogo akarudi mtaani.

Katika andiko lililotangulia tuliona kwamba ITC haina uhusiano wa aina yeyote na malipo wala kizuizi cha muda, yaani FC Lupopo hawana haki ya kuzuia ITC ya Zahoro kwa sababu ya kurejeshewa fedha, Wambura “aliwatapeli” na kuwaaminisha kwamba kila kitu kitakuwa sawa. Walitakiwa kuwa na mkataba ambao ndio wangeutumia kumuuza Zahoro, lakini kwa vile wanajua mkataba ni “Magumashi” ndio maana Wambura na wenzie wakaegemea kwenye ITC kwa makusudi na kukiuka sheria za FIFA, katika hili TFF, Association Ya Congo na FC Lupopo wana kesi ya kujibu FIFA.

Zahoro anasema akaanza kulifuatilia suala hili TFF na Wambura akamuonesha zile documents, eti Wambura ana documents za FC Lupopo, eeh Yesu wangu!! Sasa Wambura yeye ni kama nani? Watu wanatakiwa kujiuliza hapa, na Zahoro akaambiwa amesaini mkataba kule akashangaa na kulalamika sana, anajiuliza amewakosea nini?

Na mimi najiuliza, Zahoro amemkosea nini Boniface Wambura mpaka amtendendee unyama huu? Kumzuia kutopata riziki yake kwa miaka miwili na huu unaenda wa tatu? Wambura ana nufaika nini na mateso ya Zahoro ya Pazzi? Mpira ni kipaji anachotakiwa kukitumia kwa wakati maalumu sio wakati wote, na huu ndio muda wa kucheza mpira kwanini hachezi? Maisha ya Zahoro ni kama wachezaji wengine yameegemea kwenye kipaji chake, kwanini anaumizwa namna hii? Aliwakosea nini huyu mtoto jamani? Muambieni ajue atawalilia na kuwaomba msamaha lakini msikatishe ndoto zake.

Au labda kina Wambura wana “bifu” na Iddi Pazzi Kwahiyo wanamuadhibu mtoto wake? Kama ndivyo kwanini msimwambie Mzee Iddi Pazzi awaombe msamaha ili mwanae acheze mpira na kuendesha maisha yake? Ni mzazi gani anafurahia mateso ya mwanae? Ni katili gani anaweza kumtesa mtoto badala ya baba? Familia ya Pazzi imewakosea wapi hawa viongozi wa TFF?

Au labda ni tamaa ya pesa? Kweli tama ya pesa inaweza kufikia kiwango cha kuondoa utu na kumtesa mtoto mdogo ambae bado anatafuta maisha? Tena unamnyonga katika egemeo lake la muda wote la kujikwamua na umasikini? Zahoro anafanya biashara gani nyingine zaidi ya kutegemea kudra za Mwenyezi Mungu arejee uwanjani na aanze maisha upya? Unawezaje kuwa na roho ngumu ya kumkandamiza mtoto ambae Taifa linaweza kujivunia baadae kwa mpira wake? Unawezaje kusema unaongoza taasisi inayosimamaia ukuaji na uendelezaji wa vipaji ikiwa upo mstari wa mbele kuua na kuangamiza vipaji hivyo?? TFF mjipime sana katika hili.

Ok, tunaendelea.. Zahoro akaenda Mbeya City ambapo mpaka sasa ndio anahangaika nao kupata hii ITC, tatizo ni kwamba uongozi mzima wa Mbeya City sio watu wa mpira kabisa, nina mashaka makubwa na uelewa wao juu ya sheria hizi za usajili, hadhi na uhamisho wa wachezaji. FIFA wameeleza wazi kabisa tena wametamka mpaka muda wa masuala haya kuchukuliwa hatua, ina maana Mbeya City ni klabu ya mpira na hawajui sheria na kanuni hizi? Kwanini wanaruhusu kuchezewa akili na TFF? Kwanini wajishushe sehemu wanayotakiwa kupanda na kudai haki?

Mbeya City kama mlikuwa hamjui ni kwamba, Zahoro Pazzi ni mchezaji huru hana mkataba na FC Lupopo wala jina lake halipo katika orodha ya wachezaji wa Lupopo na halijawahi kuwemo, hawana sababu za kuzuia ITC ya kijana, wao na Wambura wanatakiwa watafute namna ya kuachana kama walivyotafutana wakati wanakutana, madai ya FC Lupopo kwa Zahoro katika lugha ya kisheria tunasema ni “Null and Void” yaani Kiswahili kisicho rasmi ina maana ya “Batili”, na TFF hawana ubavu wa kuzuia hili unless wanajitafutia matatizo na FIFA.

Sijajua ni lini Zahoro amesaini Mbeya City, lakini kwa mujibu wa sheria za FIFA chini ya siku 30 alitakiwa kuwa kiwanjani anacheza ligi kuu Tanzania bara, iwe wametaka au hawajataka, sheria haipindishwi na sheria haina busara wala subira, hakuna sababu ya kusumbuana na TFF ambao ndio wanyanyasaji wakubwa.. hivi wewe inakungila akilini kwamba ni Wambura peke yake yupo nyuma ya hili? Sasa kama unaamini vile ninavyoamini kwanini uendelee kuomba msaada kwa Malinzi?

Jambo la ajabu kabisa ni kwamba, viongozi wale wa FC Lupopo waliopiga “dili” na Boniface Wambura eti hawapo tena madarakani, wamekuja viongozi wapya na hawajui kabisa kuhusu huu mkataba wa Zahoro na timu yao, na kuna barua nakumbuka niliiona imeandikwa kwa kifaransa ikitamka kwamba Zahoro sio mali ya FC Lupopo na hawadaiani nae, kwahiyo inawezekanaje sasa tuseme FC Lupopo wamezuia ITC ya Zahoro wakati tayari wao wamesema hawamtambui? Ni nani anashikilia hii kitu ikiwa hata chama cha Congo hakina jina la Zahoro kama mchezaji wa FC Lupopo?? Kuna masuala kwakweli yanahitaji msaada wa Mungu kuyaelewa, vinginevyo mnaweza kupandishiana na watu ikabaki lawama. Maana ni full mvuruganyiko.. au ITC ipo pale pale TFF aisee?

Sasa tunarudi kwenye sheria za FIFA, kama kawida nitaandika bila kuzitafsiri nisije nikapotosha maana, hii ni REGULATIONSon the Status and Transfer of Players, na juu kabisa wameandika “These regulations were approved by the FIFA Executive Committee on 17 March 2016 and come into force on 1 June 2016”, kule Zurich, Uswisi ni zile latest kabisa. tuanze nah ii hapa:-

“1 SCOPE
1.
These regulations lay down global and binding rules concerning the status of players, their eligibility to participate in organised football, and their transfer between clubs belonging to different associations.”

Kwahiyo hapo TFF wanamezwa na hizi sheria, na hawana ujanja wa aina yeyote, wala kiburi. Ok, inafuta hii hapa..
“4 TERMINATION OF ACTIVITY
1.
Professionals who end their careers upon expiry of their contracts and amateurs who terminate their activity shall remain registered at the association of their last club for a period of 30 months.

2.
This period begins on the day the player made his last appearance for the club in an official match”

Zahoro Pazzi hajawahi kucheza FC Lupopo mchezo wowote, hana mkataba na Lupopo na hivyo kumbe hajasajiliwa na chama cha Mpira nchini Congo, sasa ITC yake itatolewa na nani? Kumbe wala hakuna ITC halali ya huyu mtoto. Na hata kama ipo, hiyo miezi 30 ni bure kwasababu hajawahi kuvaa jezi yao. Mkataba wake “feki” ni wa miaka mitatu, lakini jina lake halipo katika orodha ya kikosi cha Lupopo, ahsante sana.
Tuje na hapa:-

“5 REGISTRATION
1.
A player must be registered at an association to play for a club as either a professional or an amateur in accordance with the provisions of article 2. Only registered players are eligible to participate in organised football. By the act of registering, a player agrees to abide by the statutes and regulations of FIFA, the confederations and the associations.

2.
A player may only be registered with one club at a time”
Zahoro hayuko registered na Klabu yeyote duniani zaidi ya Mbeya City, hilo lieleweke wazi. Tuzidi kusonga mbele..
“8 APPLICATION FOR REGISTRATION

The application for registration of a professional must be submitted together with a copy of the player’s contract. The relevant decision-making body has discretion to take account of any contractual amendments or additional agreements that have not been duly submitted to it.”

Hapo sasa ni kwamba Zahoro anaweza kurekebishiwa mkataba wake kwa mujibu wa sheria hii, na ndipo inapoweza kugundulika “ Du Contractel Null and Void” yaani mkataba batili. Tunaendelea…

“9 INTERNATIONAL TRANSFER CERTIFICATE
1. (Skipped)
2. Associations are forbidden from requesting the issue of an ITC in order to allow a player to participate in trial matches.”

Zahoro aliambiwa anaenda kufanya majaribio tu FC Lupopo, na alikaa kwa siku nne nchini mule.. sasa hiyo ITC Chama Cha Congo kiliomba ya kazi gani? Na TFF ilikuwaje wakakubali kuitoa kabla hata Zahoro hajaenda? Neno “forbidden” tunaweza kusema ni “marufuku”, sasa inakuaje TFF na Chama cha Congo wakakiuka katazo hili la FIFA? Ni nani atapeleke taarifa FIFA za “Uhuni” kama huu? Katazo hili ni kwa Chama cha Congo, lakini TFF wanajua ilikuwaje mkataba na release letter ya Simba vikaenda FC Lupopo bila ya Zahoro kujua, na mkataba ukasainiwa kwa kuighushi sahihi ya Zahoro. Tubaendelea…

“13 RESPECT OF CONTRACT
A contract between a professional and a club may only be terminated upon expiry of the term of the contract or by mutual agreement.”

Mbeya City, Zahoro na hao FC Lupopo kwa mujibu wa kanuni hii, ndio wanatakiwa kuvunja mkataba “by mutual agreement” ili kama wana madai ya msingi basi Mbeya City watalipa, lakini sio kuzuia ITC hawana mamlaka hayo, ni chama cha Congo pekee ndio kina uwezo wa kutoa ITC na sio kuzuia. Tunaendelea..

“14 TERMINATING A CONTRACT WITH JUST CAUSE
A contract may be terminated by either party without consequences of any kind (either payment of compensation or imposition of sporting sanctions) where there is just cause.

15 TERMINATING A CONTRACT WITH SPORTING JUST CAUSE
An established professional who has, in the course of the season, appeared in fewer than ten per cent of the official matches in which his club has been involved may terminate his contract prematurely on the ground of sporting just cause. Due consideration shall be given to the player’s circumstances in the appraisal of such cases. The existence of sporting just cause shall be established on a case-by-case basis. In such a case, sporting sanctions shall not be imposed, though compensation may be payable. A professional may only terminate his contract on this basis in the 15 days following the last official match of the season of the club with which he is registered.”

Hapo sitii neno kabisaaa, lakini mazingira ya kuvunja mkataba yapo wazi na yanataka Zahoro awe amesajiliwa, sasa unavunjaje mkataba ambao haupo?? Sijui mnaelewa namna Zahoro anaonewa bila kosa jamani?? Hata sheria za FIFA haziwaungi mkono TFF, Lupopo, na Chama cha Congo, zoote zinaonesha ushindi mkubwa kwa Zahoro, sijui watu wanashindwa wapi jamani!
“17 CONSEQUENCES OF TERMINATING A CONTRACT WITHOUT JUST CAUSE
5.
Any person subject to the FIFA Statutes and regulations who acts in a manner designed to induce a breach of contract between a professional and a club in order to facilitate the transfer of the player shall be sanctioned.”

Hii ni kwa ajili ya Boniface Wambura, tena anatakiwa kufungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya michezo, Istanbul!!!! Bado tunaendelea…

“VIII. Jurisdiction

22 COMPETENCE OF FIFA
Without prejudice to the right of any player or club to seek redress before a civil court for employment-related disputes, FIFA is competent to hear:
a) disputes between clubs and players in relation to the maintenance of contractual stability (articles 13-18) where there has been an ITC request and a claim from an interested party in relation to said ITC request, in particular regarding the issue of the ITC, sporting sanctions or compensation for breach of contract;”

Haya na hapo tena mnataka kuniambia Mbeya City walikuwa hawajui? Meneja wa Zahoro alikuwa hajui? Ni uoga au ni kutokujua? Maana kuna watu wakiona viongozi wanatetemeka mno, yaani hawawezi kusimamia haki eti kwakuwa tu wapo wakubwa pale, kupishana na TFF wanaona kama ni kushushwa daraja au labda kujitafutia matatizo, come on guys for how long will you be slaves of your own fear? Don’t be so coward boys. Twendeni kazi..

MUHIMU ZAIDI NI HILI HAPA.

“Annexe 3
2 SYSTEM

1.
TMS provides associations and clubs with a web-based data information system designed to administer and monitor international transfers.

2.
Depending on the type of instruction, a variety of information must be entered.

3.
In case of an international transfer where no transfer agreement exists, the new club must submit specific information and upload certain documents relating to the transfer into TMS. The process is then moved to the associations for electronic ITC handling (cf. section 8 below).

4.
In case of an international transfer where a transfer agreement exists, both clubs involved must, independently of each other, submit information and, where applicable, upload certain documents relating to the transfer into TMS as soon as the agreement has been formed.

5.
In the case referred to in the preceding paragraph of this article, the process is only moved to the associations for electronic ITC handling (cf. section 8 below) once club-level agreement has been reached.”

Namba 3 hapo naona inahusika kabisa, kazi ipo kwa Mbeya City tu. Ngoja tu nihitimishe hapa..

“8.2 CREATING AN ITC FOR A PROFESSIONAL PLAYER

4.
Within seven days of the date of the ITC request, the former association shall, by using the appropriate selection in TMS, either:
a) deliver the ITC in favour of the new association and enter the deregistration date of the player; or
b) reject the ITC request and indicate in TMS the reason for rejection, which may be either that the contract between the former club and the professional player has not expired or that there has been no mutual agreement regarding its early termination.

5. (Skipped)

6
If the new association does not receive a response to the ITC request within
15 days of the ITC request being made, it shall immediately register the professional player with the new club on a provisional basis (“provisional registration”). The new association shall complete the relevant player registration information in TMS (cf. Annexe 3, article 5.2 paragraph 6). A provisional registration shall become permanent one year after the ITC request. The Players’ Status Committee may withdraw a provisional registration, if, during this one-year period, the former association presents valid reasons explaining why it did not respond to the ITC request.

7.
The former association shall not deliver an ITC if a contractual dispute on grounds of the circumstances stipulated in Annexe 3, article 8.2 paragraph 4 b) has arisen between the former club and the professional player. In such a case, upon request of the new association, FIFA may take provisional measures in exceptional circumstances. If the competent body authorises the provisional registration (cf. article 23 paragraph 3), the new association shall complete the relevant player registration information in TMS (cf. Annexe 3, article 5.2 paragraph 6). Furthermore, the professional player, the former club and/or the new club are entitled to lodge a claim with FIFA in accordance with article 22. FIFA shall then decide on the issue of the ITC and on sporting sanctions within 60 days. In any case, the decision on sporting sanctions shall be taken before the delivery of the ITC. The delivery of the ITC shall be without prejudice to compensation for breach of contract.”

Hapo sitii neno nisije kuonekana mchawi bure.. lakini mambo yapo uchi na hadharani, FIFA wenyewe wanaweza kuja kushughulikia hili suala ndani ya siku sitini tu. Hivi tangu Zahoro atoke Congo na alipojiunga na Polisi ina maana siku sitini hazijafika? Kwanini mtoto huyu bado anateseka?

Wambura anajua alichokifanya, na kitamtokea puani kama asipotoa ITC ya huyu mtoto, hili limekaa muda mrefu sana na sisi wapenda amani na wapenda mafanikio ya mpira hatuwezi kulivumilia tena, tutaongea na wote wenye mamlaka ikiwemo FIFA wenyewe ili kunusuru kipaji cha Zahoro Pazzi, huu “ushenzi” ni lazima ukomeshwe na iwe fundisho kwa wote wenye tabia na nia ya kutenda jambo kama hili.

Ikiwa na wewe ni mpenda amani na mpenda michezo, hata kama hujui utaratibu na hujui ni wapi uanzie, wewe tuma barua au piga simu FIFA, waeleze jambo lolote bovu linalofanywa na TFF kinyume na kanuni za FIFA. Wanasikiliza vizuri na utapewa muongozo wa namna ya kufanya, ni bora tufungiwe sisi kama Tanzania kwa muda au wafungiwe hawa viongozi “wadhalimu” kuliko kuendelea kushuhudia haki za wanyongwe zikipokonywa kwa uroho wa fedha na tamaa.

ANWANI YA FIFA

Fédération Internationale de Football Association (FIFA)
President: Gianni Infantino
Acting Secretary General: Markus Kattner
Address: FIFA
FIFA-Strasse 20
P.O. Box
8044 Zurich
Switzerland
Telephone: +41 (0)43 222 7777
Fax: +41 (0)43 222 7878
Internet: FIFA.com

Ifike mahali sasa hawa miungu watu wajue tumechoka, na tunajua cha kufanya, kuwakalia kimya ni kuchukuliana tu "Kibongobongo" lakini wao wanatuona sisi ni mafala na malofa.. watu wanaumia lakini wanakaa pembeni kwa kuogopa kuharibu mahusiano na hawa watu, huko kuwastahi lakini mimi natafsiri kama unafiki.

Sasa wenye uwezo wa kusema wasiposema ni nani atasema? wenye ujuzi na sheria na wapenda michezo msipoenda mstari wa mbele ni nani ataenda? watu hawajui sheria ndio maana wanaogopa, sasa hata nyie jamani? mawakili kabisa na tunawaamini... hebu acheni hizo bana tusaidieni seriously.. nyie mnaweza kusimama kizimbani kwa kesi kubwa za maana itakuja kuwa hizi kesi za "kitoto" kabisa ambazo hata mimi darasa la saba naziona kabisa ni za "kijinga"?

Mtoto huyu anahitaji msaada, wadau tumeshindwa kumsaidia kwasababu TFF ni wababe kupindukia, hawasikii la muadhini wala la mnadi swala! nitarudi baadae.

Jeff Gemo Mnyama Machine,
The One Man Army,
Affirmative Gemo The Great

[HASHTAG]#SeriesFreeLife[/HASHTAG]
Season Two | Episode 8
Zahoro Pazzi Free Edition.

Volume II.
 

rubaman

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
4,959
2,000
Sheria ingekuwa ni msumeno Wambura angefungwa miaka mingi jela na kufungiwa kujihusisha na business ya soka. Fraud kama hii ( kama ni kweli usemavyo) isingetokea nchi za watu wajuao biashara ya soka.
 

Wanu

JF-Expert Member
Sep 26, 2013
352
250
Sheria ingekuwa ni msumeno Wambura angefungwa miaka mingi jela na kufungiwa kujihusisha na business ya soka. Fraud kama hii ( kama ni kweli usemavyo) isingetokea nchi za watu wajuao biashara ya soka.
Sasa kwanini zahoro asiende mahakaman au sheria haimruhusu kufanya hivyo?
 

mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,285
2,000
Sasa kwanini zahoro asiende mahakaman au sheria haimruhusu kufanya hivyo?
Nilitarajia mtoa mada angetuelezea pia majibu/madai ya upande unaolalamikiwa ili atuwachie tupime uzito wa hoja za pande zote na hatimaye tuje na maoni yetu binafsi kwenye jambo hili zito. Ametunyima haki yetu hiyo ya msingi kama wapashwa habari. Na bila ya maelezo hayo ya upande wa pili, habari hii nzito inabaki kuwa ni 'ubuyu' tu, ingawa uliokolea viungo -ikitiliwa maanani kwamba muda wote huo TFF imekuwa kimya kuhusu majaaliwa ya Zahor.
 

Belo

JF-Expert Member
Jun 11, 2007
12,571
2,000
Nilitarajia mtoa mada angetuelezea pia majibu/madai ya upande unaolalamikiwa ili atuwachie tupime uzito wa hoja za pande zote na hatimaye tuje na maoni yetu binafsi kwenye jambo hili zito. Ametunyima haki yetu hiyo ya msingi kama wapashwa habari. Na bila ya maelezo hayo ya upande wa pili, habari hii nzito inabaki kuwa ni 'ubuyu' tu, ingawa uliokolea viungo -ikitiliwa maanani kwamba muda wote huo TFF imekuwa kimya kuhusu majaaliwa ya Zahor.
Malinzi alikuwa member hapa kabla hajachaguliwa angesaidia kutoa ufafanuzi mambo kama haya,baada ya kushinda amekimbia
 

nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
3,956
2,000
nimesoma baadhi ya maelezo lakini kuna kitu nyuma ya pazia zahoro pazi hataki kusema ukweli!

FC LUPOPO ni timu kubwa barani Afrika kwanini aliikimbia aje ajiunge na timu za hovyo habar tz kama polisi morogoro, stand utd, mbeya city ama simba??, ukiilinganisha kiuwezo au kihadhi fc lupopo hamna wakuilinganisha hpa tz???

kwani kujadili mshahara na bosi kabla ya mkataba kulikuwa na tatizo gani???
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom