Zahanati wapewe Mamlaka kamili

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
2,360
2,000
Zahanati ni ngazi ya kwanza kabisa kukutana na Mgonjwa na Asilimia kubwa zikiongozwa na Matabibu/ Co japo hata Nurses pia wanaweza kuongoza, Zahanati kuna changamoto nyingi kama ni rufaa nyingi zinaanzia Huku awe na Mgonjwa wa kawaida au hata Mjamzito.

Ishu inakuja pale baadhi ya dawa kupigwa marufuku kuweko zahanati nikimaanisha kwamba kuna baadhi ya dawa hurusiwi kumwandikia mgonjwa kwa Ngazi ya Zahanati mfano baadhi ya dawa za Pressure/HTN baadhi ya Antibiotic..nk.Na unakuta hapo zahanati Kuna Tabibu ambaye dawa hizo hizo amezisoma akiwa Chuoni tena kwa undani zaidi lakin akifika zahanati anaambiwa haruhusiwi kumwandikia mgonjwa.

Hii Husababisha Clinicians wengi kuonekana wana uwezo mdogo wakati sio kweli,Na hapo hapo huyu Clinicians ikatokea kahamia kituo cha Afya au Hospitali anazikuta dawa hizo na kuruhusiwa kumwandikia Mgonjwa Elimu ya medicine bila kuifanya kwa vitendo unasahau haraka sana ndio unaenda Kituo cha Afya unasahau hata Mg ya Nifedipine unabaki kuandika 1*1*1/12 Sipendi hii napenda 20mg po od 1/12.

Ushauri:
Nafikiri Kuna haja ya Serikali kupitia Sera zake za Afya upya na kuzifanyia marekebisho na kushusha huduma Nyingi zaidi ngazi za chini ili kumwepushia mgonjwa usumbufu sio shida hata machine ya FBP kuwepo zahanati as Longer kuna mtaalamu mzuri wa maabara.
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
5,631
2,000
Kuna watu wana mioyo mizuri jamani! kama huyu mleta mada, yaani unaangaikia "waipiga kura" hadi basi au ndio umeajiriwa majuzi maana wengie waliaoanza kama wewe walikatishwa tamaa na "wanasiasa" hadi huruma ikafubaa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom