Zacharia Isaay (Mbunge Mbulu): Serikali iache kigugumizi ieleze wazi kuhusu ugonjwa wa kupumua unaomaliza watu wa Mbulu

Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Isaay ametaka Serikali ya Tanzania kueleza wazi kuhusu alichokiita ugonjwa wa kupumua ambao anasema unamaliza watu wa Mbulu.

Isaay amezungumza kwa hisia kali bungeni leo Alhamisi Februari 11,2021 akisema hawezi kuzungumzia mpango badala yake anaona bora azungumzie hali ya wananchi wake ambao kila mara anakwenda kuzika.

"Serikali iache kigugumizi jimboni kwangu watu wanakwisha Spika,nimechoka kuzika hata leo wanazika mtoto wa diwani wakati mwingine nashindwa kukuaga Spika kwenda Mbulu naamua kutoroka,"amesema Isaay.

Mbunge huyo anasema wanaopoteza maisha jimboni kwake magonjwa yao yanafanana ambayo ni tatizo la kupumua akihofia kuwa msimu wa baridi jimboni kwake utaendelea kuwaumiza.

"Jana nilikwenda hospitali ya hapa Benjamin Mkapa (Dodoma) kwa ajili ya kufanya vipimo lakini wakaniambia mitungi ya gesi imejaa,watu ni wengi sasa nimesema kama watu watanichukia basi lakini nimesema," amesema Isaay.

Mbunge huyo ameomba Serikali kuangalia namna ya kuboresha dawa za miti shamba ambazo ameeleza kuwa zinasaidia kwa kiasi kikubwa lakini akabainisha kuwa zinapatikana kwa gharama kubwa.

-----
Maoni Yangu
Tukipata wabunge watano jasiri kama huyu, Tanzania tutapona.

Juxi katibu mkuu Afya kasema ametembelea hosipitali zote hali ni nzuri. Hebu ona mbunge kaenda hosipitali anasema hali ni mbaya.
Hawa wataalam wana takiwa kunyongwa.
Huyu mbunge aache wenge. Tanzania hakuna covid 19.
 
Watakuwa madaktari wamemwambia ukweli mana wanabebeshwa mzigo usiowahusu , hata kama hutaki kutangaza , tuone basi huduma zinaboreshwa kimya kimya ili tujue Tija ya kutotangazwa .....
 
Mbunge wa Mbulu Mjini (CCM), Zacharia Isaay ametaka Serikali ya Tanzania kueleza wazi kuhusu alichokiita ugonjwa wa kupumua ambao anasema unamaliza watu wa Mbulu.

Isaay amezungumza kwa hisia kali bungeni leo Alhamisi Februari 11,2021 akisema hawezi kuzungumzia mpango badala yake anaona bora azungumzie hali ya wananchi wake ambao kila mara anakwenda kuzika.

"Serikali iache kigugumizi jimboni kwangu watu wanakwisha Spika,nimechoka kuzika hata leo wanazika mtoto wa diwani wakati mwingine nashindwa kukuaga Spika kwenda Mbulu naamua kutoroka,"amesema Isaay.

Mbunge huyo anasema wanaopoteza maisha jimboni kwake magonjwa yao yanafanana ambayo ni tatizo la kupumua akihofia kuwa msimu wa baridi jimboni kwake utaendelea kuwaumiza.

"Jana nilikwenda hospitali ya hapa Benjamin Mkapa (Dodoma) kwa ajili ya kufanya vipimo lakini wakaniambia mitungi ya gesi imejaa,watu ni wengi sasa nimesema kama watu watanichukia basi lakini nimesema," amesema Isaay.

Mbunge huyo ameomba Serikali kuangalia namna ya kuboresha dawa za miti shamba ambazo ameeleza kuwa zinasaidia kwa kiasi kikubwa lakini akabainisha kuwa zinapatikana kwa gharama kubwa.

-----
Maoni Yangu
Tukipata wabunge watano jasiri kama huyu, Tanzania tutapona.

Juxi katibu mkuu Afya kasema ametembelea hosipitali zote hali ni nzuri. Hebu ona mbunge kaenda hosipitali anasema hali ni mbaya.
Hawa wataalam wana takiwa kunyongwa.
Angalau huyu ame risk maisha yake kwaajili ya wana mbulu

Tunataka viongozi kama hawa
 
Mbunge wa Mbulu anasema jimboi kwake amefriki watu wengi wenye waliokuwa na dalili za Corona kiasi kwamba kwa sasa amekuwa akipokea taarifa za misiba na kuzipotezea

Ameendelea kusema pia Serikali imeshauri watu kutumia dawa za miti shamba lakini watu wamkuwa wakinywa tu kama gongo sababu hakuna muongozo maalumu

Pia amesema ametembelea Hospitali ya BW Mkapa na kuambiwa mitungi yote ya Oksijeni imeisha na kutahadharisha kuwa watashindwa hata kuwalinda wataalamu wa afya na kumba Serikali kuongeza miungi hiyo.

Amejilipua
 
Back
Top Bottom