Z. Madabida na Upatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Z. Madabida na Upatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Babu Ubwete, Dec 15, 2008.

 1. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #1
  Dec 15, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu waungwana wana JF. Idumu JF, Tukumbukane wazee wa enzi za BCS Times. Ningependa kufahamu ile shutuma ya kutapeliwa wanawake matajiri wake za vigogo kupitia mchezo wa Upatu iliyomkabili huyu mama Zarina Madabida ilizimwa vipi kwani alikusanya mamilioni ya pesa na kutoweka nje ya nchi. Kweli wanaonusa pesa ndio wanaoingia kutuongoza ufisadi utaisha kweli.
   
 2. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Duh! Babu! Hii ishu imekuwa kama imefanywa siri lakini iliandikwa sana na kuwekwa katika vyombo vya habari! Wanawake wengi walichika na kupewa talaka, wengine walidundwa na waume zao, kisa walilaghaiwa! Hii kesi ilimhusisha mpaka Mama Warioba, Mama Rupia na wanawake wengi vigogo! Madabida alikuwa ni mwenyekiti wao! Aisee nilisahau kabisa hii kesi lakini waandishi inabidi wafukue.
   
 3. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #3
  Dec 15, 2008
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nafikiri huyu mama tayari ana doa na alitikiwa awe gerezani kwani Upatu kisheria huruhusiwi Tz ni aina fulani ya Money Laundering na huyu mama mpaka akina Maria Sarungi na Vipindi vyao vya Facets wali expose sana ubaya uliofanywa na mama huyu na kudai alikimbilia Ufaransa. Anajitahidi lakini tujue ameingia kuzichota za bure zisizo na auditing
   
 4. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  Duh! Hiyo ilinipita! Itabidi ikatafutwe archives zake alafu zionyeshwe live! Itakuwa ni kiboko!
  Nakumbuka nilisoma katika Guardian ambapo iliitwa Pyramid scheme tena ilikuwa ina jina fulani la kukomboa wanawake, waliahidiwa mamilioni, wamama walikopa na kuiba pesa maofisini na majumbani! Kumbe maskini wanaibiwa! Kweli huyu Madabida alitakiwa kufungwa!
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Babu,
  ni vizuri kukumbushana madhambi yaliyofanywa na hawa watu wanaotaka kila siku wao watuongoze.Kwa kuwa tayari ameshaukwaa uenyekiti wa UWT dsm hata tukimjadili hapa haitasaidia sana kwa kuwa tayari ameshakalia kiti.Na kwa jinsi ilivyokuwa skendo yenyewe iliwahusisha wake wa vigogo, mke wa warioba na rupia ni majina makubwa sana nchi hii.
  kwa mawazo yangu nadhani ingekuwa busara sana kama mjadala huu ungefanyika kabla hajaukwaa huo uenyekiti vinginevyo tutakuwa tunapoteza muda kumjadili hapa.
  ni mtazamo tu.
   
 6. Susuviri

  Susuviri JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2008
  Joined: Oct 6, 2007
  Messages: 3,713
  Likes Received: 224
  Trophy Points: 160
  You have a point there! Lakini tulipitiwa bana! Hii skendo ilikuwa muda kidogo! Lakini bado inawezekana siyo too late.
   
 7. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #7
  Dec 15, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Je ana uhusiano na Ramadahani Madabida wa Umoja trust Fund? naona Madabida mwenyewe amefanya kazi sana kwenye makampuni ya madawa na huyu bwana naye alishiriki sana kubinafsisha shirika la madawa.
   
 8. z

  zetiti2008 New Member

  #8
  Dec 15, 2008
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yaani hamkukosea. ndio mwenyewe haswa.pamoja na kuchelewa kuweka taarifa hizi kwenye blog lakini bado taarifa ziwekwe ili kuwafungua wa akina mama macho kwenye hicho chama chao. alitapeli na kupata mtaji mzuri tu wa kufanya biashara alizonazo wakati huo farmacy ikilegalega.
   
 9. h

  halikuniki Member

  #9
  Dec 15, 2008
  Joined: Aug 6, 2007
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kuona kuwa anashinda ktk chaguzi?
   
 10. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Babu Ubwete , si wake za vigogo u waliolizwa ni wengi zaidi, tungepata picha ya huyu mama Zarina Madabida kwenye JF ingetusaidia sana.
   
Loading...