Yusuf Manji: Nitamshitaki Makonda kwa kunichafulia jina

a5f4df8eee20c5464ac231dc633aa47c.jpg

Nimeipata hiyo katika baadhi ya nyuzi humu
duh! hiyo ni hatari
 
Swali moja! Hivi huwa watu hivi vifungu vya sheria wanavyovitaja mpaka na namba sijui 60 sijui kifungu no. 70 wanakuwa wanavijua kabla ya kuwa hatiani au baada? Maana watu huwa wanakuwa makini kushika hivi vifungu na nambari zake, baada ya 'kuguswa' na sheria! Nijuveni siri ya namba na hivi vifungu vyake....je nifanyeje ili niwe na uwezo wa kukariri hivi vifungu? Je ni kweli wanaohusika na sembe (sijataja mtu) wanao uwezo mkubwa wa kushika hivi vifungu? Au hata raia tu wakawaida kama mie
Inabidi usome sheria kwa kina aisee kwanza kifungu cha sheria kimoja kinaweza kubadilishwa na maana ya kifungu kingine haraka sasa wewe ukishikilia kakifungu fulani ulikokariri akija aliyebobea vingu vingi mbona utabaki unatoa macho tu, ndio maana wanakuambia Law is flexible.
 
Leo hii, muda mfupi ujao, Yusuf Manji ataongea na Wanahabari. Haijajulikana anataka kuongelea nini.
Nitatoa Updates hapa hapa JF.

Stay tuned.

=======


Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.

Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu Mzee Manji(Manji ni jina kubwa duniani) na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Club Kubwa Barani Afrika Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.


View attachment 468510

Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukuahukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.

Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.

Manji: Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.

Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.

Manji:
Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari. Ulitakiwa unifuate kisirisiri kuniuliza ili kunisaidie.

Manji:
Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.

Manji:
Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda. Kunitaja kwenye list ya wauza madawa ya kulevya wakati sihusiki ni kuvunjia haki zangu.


Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.

Manji:
Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.

Manji:
Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali.

Manji:
Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.

Manji:
Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie? Manji ndo umeona wa kukusaidia?

Manji:
Hiwezi kuniita mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.

Manji:
Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania. Leo umenichafua, kesho tukienda Komoro tutaonekana watanzania ni wauza madawa.

Manji: Kama unataka msaada wa kukusaidia kukutajia majina ya wauza dawa za kuleya omba msaada sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Huyu si anataka nitokeSaa tano usiku? Sina kazi nyingine za kifanya?

Manji:
Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shillingi moja. Unanihusisha mimi jina langu nloachiwa na baba la Manji kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako?

Manji:
Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.

Manji:
Hivi ni vita na nawaunga mkono na wanahitaji msaada wa haraka na kama wana shutuma au ushahidi au wanataka huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri ijumaa. Mimi naenda kesho.

Manji:
Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.

Manji:
Ambao hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa. "Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho namshitaki.

Manji:
Wakina Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi wangu kwenye radio, uwezo ninao lakini nitakiwa namvunjia heshima.

Manji:
Mimi nipo tayari kupimwa kama natumia madawa na kupekuliwa nyumbani kwangu na Makonda naye apimwe kama anatumia madawa na wampekue pia nyumbani kwake.

Manji:
Ninayo Mengi ya kusema, lakini sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Kesho au keshokutwa ntafanya mkutano na ntazungumzia kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya madawa.

Manji:
Huyu Mkuu wa mkoa kwanza nlikuwa simjui, ila kunasehemu nimewahi gongana naye oysterbay na siku nyingine nlienda kuonanana naye fisini kwake kama diwani wa mbagala kuu kumuomba afikishe ombi langu kwa rais ili mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka mbagala na kupelekwa nje ya mji(Ile kambi ambayo mabomu yalilipuka).

Kama diwani siwezi kumuandikia rais.

Mangi, kuna haja kweli ya makelele yote hayo! Mkuu wa mkoa wako amekutaja, we nenda tu kama upo safi hizi kelele zote za nini? Huoni unasababisha maswali mengi zaidi! Hutaonewa, wewe nenda kama uko safi hupaswi kuanza makelele yote haya. Kwenye list wapo wengi wametajwa na watahudhuria na kutoa ushirikiano kwa polisi! Kuwa m/kiti wa yanga hakumzuwii mtu kuuza madawa ya kulevya! Tena hii inaweza ikawa ni njia rahisi zaidi ya kujifichia! Usivute media ktk suala hili! Kama huusiki, utakuwa 'cleared'!
 
Atapona Makonda hana jeuri ya kumtaja
Kwenye ile listi ya majina yaliyoletwa na mfungwa wa madawa ya kulevya China hakutaja jina hata moja ni Hariri.
Mkuu riz one c mkaz wa Dar-es-salaam.
Makonda ama deal na wana dsm pekee...kama uko pwan baac ww umepona
 
Binafsi sipendi kuona biashara hii ikisikika inafanyika Nchini, Ila najua Mheshimiwa Makonda hajawahi kufanikiwa katika mambo mengi ambayo ameyaanzisha. Sasa ninauhakika hii shughuli imeshamshinda. Strategy anazozitumia ni za hovyo kabisa.... na ninaiona aibu itakayo kuwa kwake siku chache zijazo. Hata mashirika makubwa ya CIA na FBI ya nchini Marekani hayapambani na madawa kwa style hii!! Manji ameongea points kadhaa zenye uzito wa aina yake.
 
na Manji alivyo na mdomo usio na break tutegemee mazito zaidi.
Kiongozi hapo naona Boss Manji kweli kama ameteleza sehemu fulani, coz hata kama RC amekosea hawezi kujudge negative kwa kiongozi wa umma wakati RC alipomtaja sehemu fulani alisema wanao ushahidi wa kutosha, kwa pande zote tatu. Watumiaji,wauzaji na wenye taarifa za kusaidia khs upatikanaji wa madawa yenyewe. Kwahiyo me cdhani sana kama RC anaweza kutoka hadharani kuzungumzia jambo bila kuwa na chembe ya uhakika. Vita hii ni NGUMU mno. NO TRUST ANY ONE. Alamsiki
 
...safi sana Manji....jina la Freeman Aikael Mbowe halimo kwenye orodha ya makonda....hivyo Freeman haitaji kwenda polisi ijumaa....aliposema mbunge wa Hai hakusema ni mbunge wa sasa ama wa lini...na kama alimaanisha wa sasa basi jina lake halimo kwenye list...period.....inabidi wale wanaoonekana kutajwa kwa hila sasa wakomae na sheria tu...maana ni sheria peke ya ke itawapa haki na kuwasafisha....Manji analijua hili vema....na ameanza...
 
Kiongozi hapo naona Boss Manji kweli kama ameteleza sehemu fulani, coz hata kama RC amekosea hawezi kujudge negative kwa kiongozi wa umma wakati RC alipomtaja sehemu fulani alisema wanao ushahidi wa kutosha, kwa pande zote tatu. Watumiaji,wauzaji na wenye taarifa za kusaidia khs upatikanaji wa madawa yenyewe. Kwahiyo me cdhani sana kama RC anaweza kutoka hadharani kuzungumzia jambo bila kuwa na chembe ya uhakika. Vita hii ni NGUMU mno. NO TRUST ANY ONE. Alamsiki
alivyompiga warioba alikuwa na uhakika!!!!
 
Angalia sasa ulivyokuwa mzembe wa kufikiri unajua km huautendei haki ubongo wako wake up kijana, relax, changanua na pambanua mambo ndio ukoment siyo unapelekwapelekwa ovyo tu
Nikuulize wewe kibaraka wa manji kwani ni yeye peke yake katajwa? Mbona unashoboka sana? Mmezoea kuishi kwa kusifia fanya kazi ule kwa jasho boss wako Ndio hivyo tena ni muuza madawa lazma akanyee ndoo kama vipi nenda sentro kamsaidie lakini kumbuka serikali hii haijaribiwi
 
Hahaha magazeti ya kesho yatavyogeuzwa chezea pesa makonda ashtakiwa na manji kuharibu jina lake
 
Nikuulize wewe kibaraka wa manji kwani ni yeye peke yake katajwa? Mbona unashoboka sana? Mmezoea kuishi kwa kusifia fanya kazi ule kwa jasho boss wako Ndio hivyo tena ni muuza madawa lazma akanyee ndoo kama vipi nenda sentro kamsaidie lakini kumbuka serikali hii haijaribiwi

Kwaiyo umekaa mwnyw na ukatafakari ndio umekuja kuharisha hapa, wasalimie
 
Hahahhahahahahaa
Kuwa Mwenyekiti wa Yanga sio sababu ya kuzuia kuhojiwa Manji afadhali Manji angesema yeye Kama kiongozi Diwani. It's very shame kwa Manji kumhusisha Kardinali Pengo. Manji heshimu mamlaka iliyopo madarakani kwani kuitwa na kuhojiwa sio kuwa una kosa, unatakiwa uende ukasikie wito wa serikali. Kuhusu suala la kulipa kodi sio msaada ni wajibu wa kila mtu kulipa.
Mr Manji Look before you Leap.
 
Back
Top Bottom