Yusuf Manji: Nitamshitaki Makonda kwa kunichafulia jina

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Leo hii, muda mfupi ujao, Yusuf Manji ataongea na Wanahabari. Haijajulikana anataka kuongelea nini.
Nitatoa Updates hapa hapa JF.

Stay tuned.

=======


Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.

Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu Mzee Manji(Manji ni jina kubwa duniani) na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Club Kubwa Barani Afrika Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.


a2f05f99-ff53-4c1a-aac0-a83f597803fa.jpg


Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.

Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.

Manji: Na Katiba inasema kila mtu ana haki yake, ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.

Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.

Manji:
Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari. Ulitakiwa unifuate kisirisiri kuniuliza ili kunisaidie.

Manji:
Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.

Manji:
Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kifungu 32 pia. Vinanilinda. Kunitaja kwenye list ya wauza madawa ya kulevya wakati sihusiki ni kuvunjia haki zangu.


Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.

Manji:
Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.

Manji:
Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya Mkuu wa Mkoa ni kosa siwezi kukubali.

Manji:
Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.

Manji:
Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie? Manji ndo umeona wa kukusaidia?

Manji:
Hiwezi kuniita mimi kama Mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.

Manji:
Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania. Leo umenichafua, kesho tukienda Comoro tutaonekana watanzania ni wauza madawa.

Manji: Kama unataka msaada wa kukusaidia kukutajia majina ya wauza dawa za kulevya omba msaada sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Huyu si anataka nitoke Saa tano usiku? Sina kazi nyingine za kifanya?

Manji:
Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilingi moja. Unanihusisha mimi jina langu nililoachiwa na baba la Manji kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako?

Manji:
Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.

Manji:
Hivi ni vita na nawaunga mkono na wanahitaji msaada wa haraka na kama wana shutuma au ushahidi au wanataka huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri Ijumaa. Mimi naenda kesho.

Manji:
Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.

Manji:
Ambao hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa. "Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho namshitaki.

Manji:
Wakina Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi wangu kwenye radio, uwezo ninao lakini nitakiwa namvunjia heshima.

Manji:
Mimi nipo tayari kupimwa kama natumia madawa na kupekuliwa nyumbani kwangu na Makonda naye apimwe kama anatumia madawa na wampekue pia nyumbani kwake.

Manji:
Ninayo Mengi ya kusema, lakini sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Kesho au keshokutwa nitafanya mkutano na nitazungumzia kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya madawa.

Manji:
Huyu Mkuu wa Mkoa kwanza nilikuwa simjui, ila kunasehemu nimewahi gongana naye Oysterbay na siku nyingine nilienda kuonanana naye ofisini kwake kama Diwani wa Mbagala Kuu kumuomba afikishe ombi langu kwa rais ili Mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka Mbagala na kupelekwa nje ya mji (Ile kambi ambayo mabomu yalilipuka).

Kama Diwani siwezi kumuandikia rais.
 
Tunapenda vita hii iendelee maana inaangamiza nguvu kazi ya taifa lkn naona kama namna inavyoendeshwa haiko fair , kwakweli Makonda watu unaowataja kuhusika na madawa ya kulevya mahakama ikiwaona hawana hatia utakuwa na wakati mgumu sana.

Sisemi uache lkn nimekupa tahadhali,kumbuka cheo ni dhamana.
 
Back
Top Bottom