Yupo wapi Kheri James, Mwenyekiti UVCCM taifa

Elvis Legacy

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
3,388
4,717
Habari wapenzi na mashabiki wa jukwaa hili pendwa.

Naomba kuuliza alipo kijana Kheri James, moja ya vijana mahiri wenye ushawishi mkubwa wa siasa hapa Tanzania kwa mujibu wa jarida fulani.

Mara ya mwisho kumsikia huyu kada wa CCM ni alipoomba radhi kwa watanzania aliowakosea kwenye kutekeleza majukumu yake na kuomba kuanza ukurasa mpya wa mshikamano kwa watanzania.

Pia alikuwa mahiri kwenye kufanya ziara za hapa na pale. Nashangaa sijamuona kwenye harakati hasa kwenye chaguzi ndogo za majimbo mawili kule Kigoma.

Naomba tujuzane aliipo komredi Kheri James.
 
Yaani familia nzima ilichomekwa daaaa yule wa kawe naye amevunja rekodi kabisaa hajulikani akashinda kura zote hadi wakaona aibu....sasa Kheri James ambae sio jina lake pia ....ameomba msamaha kwa matusi na kejeli awamu 5 ya mjomba wake alitukana akasema anaebisha watampa mimba mke wake....jeuri kibri kilimzidi umri
 
Aliomba msamaha "kama amekosea" wakasusia, sasa hivi atakuwa anaishi mithili ya wanayama jamii ya swala, digidigi, pundamilia katika pori lenye chui,duma,simba, fisi na wanyama wengine wakali walao nyama kwa jina la kisayansi huitwa "kanivora'
 
Habari wapenzi na mashabiki wa jukwaa hili pendwa.

Naomba kuuliza alipo kijana Kheri James, moja ya vijana mahiri wenye ushawishi mkubwa wa siasa hapa Tanzania kwa mujibu wa jarida fulani.

Mara ya mwisho kumsikia huyu kada wa CCM ni alipoomba radhi kwa watanzania aliowakosea kwenye kutekeleza majukumu yake na kuomba kuanza ukurasa mpya wa mshikamano kwa watanzania.

Pia alikuwa mahiri kwenye kufanya ziara za hapa na pale. Nashangaa sijamuona kwenye harakati hasa kwenye chaguzi ndogo za majimbo mawili kule Kigoma.

Naomba tujuzane aliipo komredi Kheri James.
Inabidi akamatwe atwambie nani alimpiga Lisu risasi maana aliseam and I quote him "Safari hii tunammaliza na sindano, pyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu"
 
Heri James, Dotto James, Sabaya na Makonda walikuwa miungu watu enzi za mwendazake. Sasa wanaishi kama digidigi.
Ila wamepiga Sana kodi zetu sema tu Utawala wa kulindana kwa wenzetu ilifaa wawe ndani bila ushahidi kukamilika kwanza waonje kama walivyowatendea wenzao
 
Back
Top Bottom