livewise1
JF-Expert Member
- May 25, 2019
- 837
- 968
Wakuu habari za asubuhi!
Nina rafiki amejikuta yupo njia panda, baada ya kujua ukweli na maamuzi yalishatoka kitambo.
*jamaa alimsomesha binti o'level mpaka certificate (mambo ya health).
*lengo lake na walivokubaliana ni kumuoa. Na kweli alimuowa baada ya shule.
*akamtaftia ajira mshahara laki na 20 lakini matumizi yote jamaa anatoa mpaka nauli mkewe kwenda kazini. (Mshahara wake aliutumia anavojua yeye)
*mama mkwe wa jamaa alikuwa kijijini na hali yake sio nzuri kiuchumi ( ni mjane ndio maana hakuwa hata na uwezo wa kusomesha mwanae)
*jamaa akanwambia mkewe wamchukue mama aje kuishi nao, kweli akaletwa maisha yakaendelea.
*baada ya muda kuna jamaa mpangaji mwenzao (mtu mzima) akamuuliza jamaa "kijana unaishi kwa amani na mkeo na mamake?" Jamaa akasema ndio....yule mtu mzima akakazia, "una uhakika?" Ndio nina uhakika, kwani vipi! ? Jamaa akasema ok sawa kama hakuna shida, ila kama patakuwa na shida usisite kuniambia.
*jamaa akafikiria weee....akaona ngoja achunguze kuna nini?
*siku moja akiwa anarejea kutoka kazini usiku akawakuta mkewe na mamake wanamjadili namna ya kumuweka kiganjani asisaidie ndugu zake ila awe anasaidia ukweni tu na wajipange wampige pesa kidogo dogo wajenge na kufungua duka kwao na kununua mashamba.
*jamaa akaingia ndani hawakujua kama kasikia kitu....usiku huo akamwambia mkewe ana malengo ya kumfungulia pharmacy ila mbona ameanza kuonesha dharau tatizo nini!?
*mke akasema hiyo pesa nipe mi najua ntaenda maduka ya dawa bei nafuu ... ila akakwepa kueleza kwa nini dharau zimeanza. Jamaa akasema zipo benki
*dharau zikazidi na fujo mpaka jamaa akatoa talaka na kuhama hapo akawaacha. Alikuwa taabani kwa mawazo maana alimpenda sana mkewe...kwa hasira akaowa mtu mwengine baada ya miezi kadhaa.
*mkewe aliemuacha akaanza kutaabika na mamake akarudi kijijini...kodi na chakula mshahara hautoshi akawa anamtafuta mtalaka wake ili amsaidie.
*baadae jamaa akaanza kumhudumia kodi na kula maana jamaa nae kakwama (bado anampenda binti japo hakuzaa nae) na ameoa mke ambae anajua ndoa ni nini...yaani hata kosa la kumsingizia halioni.
*mtalaka wake anaomba msamaha na kusema mama ndio kampoteza ila anampenda sana jamaa...anaomba jamaa arudishe moyo hata waowane tena.
*hapo ndio mziki sasa kwa jamaa...huyu mke wa saivi ni wife material yaani...halafu jamaa bado anampenda wa zamani na ashajua kirusi alikuwa ni mkwewe yaani.
*kumuacha huyu hawezi na kuowa wawili uwezo hana japo anahudumia mpaka leo ila ndio anavyodai kuowa wawili hawezi.
*yupo dilemma hajui afanye maamuzi gani!!
NB: aliniomba ushauri nikamwambia asee mi sina la kukwambia maana ulishaamua na hukunieleza yote haya tangu mwanzo. ..lakini pia angalia usije fanya kosa tena.
Wakuu hali hii ungekuwa wewe ungefanyeje?
Sent using Jamii Forums mobile app

mtu na mama ake awa wezi kukosana kisa ka mtu kamoja .......akirudi tu lig inaendelea