Yupi ni Mwanasoka Bora wa Wakati Wote Barani Afrika?

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,849
67,285
AFRIKA imezalisha Wachezaji wengi mahiri ambao wamekuwa na Vipaji maridhawa katika mchezo wa Soka.

Kutoka zama za akina Abedi Pele, Kalusha Bwalya hadi zama za akina George Opong Weah, Phil Masinga, Mustapha Hadji, Austin Jay Jay Okocha, Lucas Radebe na akina Nwanko Kanu.

Pia zikaja zama za akina Samuel Eto'o Fils, Didier Drogba, Yaya Toure, Mohamed Aboutrika.

Hao ni baadhiya wanasoka tu mahiri ambao wametoka katika bara hili na ambao hata baadhi yao wameacha kumbukumbu na rekodi kubwa kwenye vilabu vya Wazungu huko Ulaya.

Je kwa mtazamao wako, yupi ni mchezaji bora wa wakati wote kutoka katika bara hili adhimu la Afrika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom