Lionel Messi ni wakati wa kupewa jina analostahili

Nihzrath

Member
Jan 15, 2013
51
116
NA

NIHZRATH NTANI

WAKATI mwili wake utakapokuwa ukishushwa katika ardhi ya mji wa Rosario.Ni kilomita 300 kutoka mji mkuu wa Buenos Aires nchini Argentina.

Ni ardhi ile ile iliyowameza wachezaji maarufu na mashujaa wetu hata wapendwa wetu.

Ardhi isiyo na huruma hata kidogo. Ni katika mji huo wa Rosario; ndipo walipotokea watu maarufu sana duniani kama vile mwanamapinduzi Che Guevara.

Wachezaji maarufu kama Angel Di Maria, Maximilian Rodriguez, hata makocha stadi kama Gerardo ‘Tata’ Martino, Marcelo Bielsa bila kumsahau gwiji la uchekeshaji, Alberto Olmedo .Wote hawa wametokea mji mmoja na staa wa soka duniani, Lionel Messi.

Fahari iliyoje? Labda kipindi ambacho baadhi yetu hatutakuwepo Duniani.

Ni kipindi hicho ambacho vyombo vyote vya habari vitakuwa vikiripoti habari zake kila baada ya sekunde kupita, huku televisheni zetu zitakuwa zikirejea na kuonesha uwezo na umahiri wake angali akiwa mchezaji.

Mabao yake ya kusisimua na uwezo wake wa ajabu utakuwa unatukumbusha kile ambacho miongoni mwetu tulikuwa tukikibeza, nyakati zitaturuhusu kutukumbusha.

Ndipo ,kila mmoja wetu atakuja kukiri hakika Messi alikuwa na kipaji cha kipekee kuwahi kutokea Duniani.

Ilikuwa zawadi kubwa ambayo Mungu alitupatia. Wakati kizazi hiki kikiendelea kushangaa na kujiuliza sifa anazopewa Edson Nascrimento “Pele” wa Brazil kuwa alikuwa mchezaji mahiri zaidi kutokea Duniani.

Bado wengi wetu, tunaweza kubisha hili lakini ukweli Pele alicheza katika zama ambazo soka haukuwa mchezo maarufu sana.

Hata rekodi zake bado wachambuzi wengi wa soka na waliomshuhudia wanatia shaka.

Wakati ambao tumekuwa tukibishana nani bora kati ya Diego Armando Maradona na Pele, ndipo ambapo tunapata jina moja tu likijitokeza katikati yao na anaweza kuwa bora zaidi, naye ni Lionel Messi.

Miguu yake imetuonesha na inaendelea kutuonesha kile ambacho hatukuweza kukishuhudia kwa wachezaji wengine wanaosemekana kuwa mahiri kama vile Alfredo Di Stefano, Michael Platin, Johan Cruyff, Farenc Puskas na wengineo.

Pengine tutakuwa tumekaa kwenye runinga zetu nyakati hizo. Runinga zitakapokuwa zikitukumbusha kwa kuonesha ufundi wake, mabao na umahiri wake enzi ya uhai wake.

Miongoni mwetu tutakuwa tumechelewa mno kumpa sifa alizostahili wakati angali anacheza ,badala yake tutaanza kumsifia na kumtaja kuwa ndiye mchezaji bora zaidi kutokea Duniani. Huku baadhi wa watu wakienda mbali zaidi na kumtaja mchezaji bora zaidi wa muda wote.

Hata hivyo, hulka ya binadamu itakuwa inatimizwa. Kumsifu mtu akiwa hayupo machoni petu na hatuwezi kumuona tena.Unafiki ulioje!!

Mtu ambaye hataweza kusema asante na kujumuika nasi kusheherekea, ndipo tutakapotengeneza hulka ya kujipendekeza.

Alafu tutamuenzi kwa maneno, kisha tutamsahau. Lakini macho na akili zetu zitatukumbusha wakati huo utakapowadia.

Nyakati zitatuumbua hasa kwa watu ambao hatuwezi kukubali uwezo wake kwa sasa kwa kile anachotuonesha uwanjani. Bila shaka tutakuwa tumechelewa mno kumuita mfalme wa soka Duniani, kwanini tusimuite hivi leo?

Wakati mjadala wa yupi mfalme wa soka Duniani kati ya Pele na Maradona ukiwa kama unaelekea ukingoni katika kizazi hiki ambacho hakikupata nafasi ya kuwashuhudia wanaume hao wakicheza enzi za nyakati zao kwa kila mmoja, Lionel Messi anatupa jibu na kumaliza mjadala huo kwa kile anachotuonesha dimbani kila kukicha.

Wakati mashabiki wa sasa wakiendelea kuhoji ubora aliokuwa nao Edson Nascrimento ‘Pele’ enzi hizo ,ndipo ambapo wanaanza kufungua vitabu vingi vya kumbukumbu.

Pele hakuwahi kucheza nje ya Brazil akiwa katika ubora wake. Tunaweza kuendelea kusema alitamba katika ligi dhaifu iliyokuwa ikiwajumuisha Wabrazil pekee.

Pele ametwaa mataji mawili ya Copa Libertadores, michuano yenye hadhi sawa na ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, wakati Lionel Messi amefanya hivyo mara nne huku akiibeba Barcelona mikononi mwake.

Pele alitwaa mataji sita akiwa na Santos katika ligi ya Brazil lakini Messi amefanya hivyo mara tisa . Kitu pekee ambacho Pele anaweza kutamba ni kuweza kutwaa mataji matatu ya Kombe la Dunia akiwa na Taifa lake.

Lakini hoja hii inaweza kuwa haina nguvu sana kuisimamia, kwa sababu kuna wachezaji wasio na uwezo mkubwa na wamewahi kutwaa taji hili lakini hatuwezi kuwaweka katika daraja moja la wanasoka mahiri zaidi kutokea kwa kigezo cha kutwaa Kombe la Dunia.

Ametwaa tuzo ya Mwanasoka bora wa Dunia mara tano na hakuna mchezaji aliyewahi kufanya hivyo kabla yake. Tumpe sifa yake anayostahili sasa.

Utakuwa ni uwendawazimu hivi leo kumfananisha Lionel Messi na mchezaji mwingine. Ndio ,kwa kile anachotuonesha uwanjani ni uwendawazimu kumfananisha na mchezaji mwingine. Labda tu tuseme anamkaribia Lionel Messi. Jisifu tu kuwa wewe una bahati kubwa kuzaliwa katika kizazi cha Lionel Messi na kuweza kumshuhudia akicheza maana kuna wengine miaka mingi ijayo watakuwa wakisoma na kutazama santuri zake tu. Bahati kubwa hii, tujivunie sasa!

Wakati mmoja, Mhariri wa gazeti la ‘The Guardian’ la Uingereza, Sid Lowe, aliwahi kusema: “Kumfananisha Lionel Messi na yeyote sio haki hata kidogo.

Messi si binadamu wa kawaida,” kauli hii ikaungwa mkono na Ander Herrera wakati huo akiwa Athletic Bilbao alisema: “Sina hakika kama Messi ni binadamu.” Kufuru kubwa hii! Lakini anachotuonesha Lionel Messi ni maajabu machoni pa mwanadamu.

Umahiri na ubora wake huu ulikwishatabiriwa tangu akiwa na miaka 16 wakati huo, kiungo na staa wa Barcelona kipindi hicho, Ronaldihno Gaucho, alisema hili siku ya kwanza tu kumuona Messi akifanya mazoezi na timu ya wakubwa. Inasemekana Ronadihno aliwaambia wachezaji wenzake mtoto huyu mwenye miaka 16 angekuja kuwa mchezaji mahiri zaidi duniani kuliko hata yeye.

Ronaldihno haraka akajenga urafiki na Messi, ni Messi ndio alikuja kuwa sababu kuu ya kuuzwa kwa Ronadihno Gaucho kutoka klabuni Barcelona kwenda AC Milan. Utabiri uliokuja kutimia miaka michache baadaye.

Juni 24 mwakani, Messi atakuwa anatimiza miaka 32, kwa wachezaji wengi kutoka barani Ulaya utakuwa umri wa kuwa kileleni mwa soka lao.

Bahati mbaya Messi anatokea bara la Amerika ya Kusini ambako wachezaji wengi kutoka bara hilo wamekuwa wakifikisha umri huo miguu yao inatupa kile ambacho si ubora wake na kufikia mwisho wa umahiri wao.

Adriano de Leite mchezaji wa zamani wa InterMilan, Kaka, Ronadihno, Robihno, Tevez, Saviola, Redondo wanaweza kutukumbusha hayo.

Ila sitegemei kuliona hili kwa Lionel Messi, bado tuna miaka michache ya kuendelea kufaidi kuuona umahiri wake akiwa uwanjani.

Siku zote mpira unamtii Lionel Messi, macho yake yako makini zaidi kulijua goli kuliko hata anaposoma kitabu kitakatifu. Hakika tukubali tu na tumpe sasa sifa anazostahili, tusisubiri kumpa sifa zake pale tu atakapoondoka duniani.
 
Asante sana mkuu,,umeeleweka vizuri sanaa.huo ndo ukweli halisi kwa mfalme Messi.
 
Nimekuwa mshabiki wa damu wa CR7 ila Messi ni mtu mwingine. Sitaki kumpa sifa zake kwa sababu ya chuki tu ila jamaa anajua sana mpira.

Asingekuwa Cr7 ningempa sifa zake zote ila nakubali ni mmoja ya wachezaji wazuri kupata kuwaona.
 
Dah, wewe ndiye shabiki wa mpira haswaa. Big up sana!
Huwa nakuwa mgumu wa kuukana ukweli mtu akifanya jambo zuri huwa namsifia hata kama siko upande wake.

Mfano: Naipenda sana Simba ila kwa sasa Manula hawezi kuwa bora zaidi ya Kakolanya.

Kakolanya ni kipa mzuri sana kwa hapa nchini ni vile hajapata nafasi za kucheza ili vipofu wamjue vizuri.
 
Sure mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom