Yupi kati ya hawa?/ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yupi kati ya hawa?/

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by chriss brown, Dec 18, 2011.

 1. chriss brown

  chriss brown JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  NI siku nyingine tena tunakutana katika safu yetu bora ambayo inazungumzia mambo ya mapenzi. Inapanua uelewa na kujenga kujiamini zaidi katika uwanja wa mapenzi. Wengi wamenufaika kupitia hapa.

  Ndoa nyingi zilizopoteza muelekeo zimekaa sawa baada ya kusoma ukurasa huu. Kadhalika kuna vijana wengi ambao wamefanya maamuzi sahihi na kuoa/kuolewa na wenzi sahihi baada ya kupata muongozo hapa.

  Naam! Ni kisima cha ujuzi wa mambo ya mapenzi. Mada inayoendelea ni kama inavyosomeka hapo juu. Tupo katika juma la pili la kuangalia ni wapi hasa mwanamke bora anapopatikana.

  Wiki iliyopita tulianza kwa kuona faida na hasara za mwanamke wa kijijini. Pia tulianza kuona faida za mwanamke wa mjini. Leo tuanze na kuona hasara za mwanamke wa mjini kabla ya kusonga mbele zaidi.

  HASARA
  Inaelezwa kwamba wanawake wa mijini, hutumia vibaya utandawazi na hujikuta wameharibika na hivyo kuwa na tabia chafu. Mitandano ya simu za mikononi na intaneti zinatajwa kama vyombo vinavyotumiwa na baadhi ya wanawake hao kufanya ufuska.

  Ni wanawake wa gharama sana, wanapenda kutolewa ‘out’, disko na kumbi mbalimbali za burudani kila mwisho wa wiki. Kama akizoeshwa ndiyo huwa hatari zaidi, kwani siku asipotolewa, huwa ugomvi mkubwa, maana ameshachukulia kama sehemu ya maisha yao ya kimapenzi.

  Wakati mwingine ni wabishi, wanaweka fedha mbele, wakiamini fedha ni kila kitu katika mapenzi. Baadhi yao huwa na wanaume kwa ajili ya kujipatia fedha tu, na siyo ajabu siku fedha ikiisha ikawa ndiyo mwisho wa mapenzi.

  Mara nyingi wanawake hawa wamezoea maisha mepesi, siyo rahisi sana kukabiliana na mikikimikiki ya maisha. Kwa maneno mengine, huwa hawawezi kuishi katika mazingira ya shida au mabadiliko ya mazingira.

  Tatizo lingine kwa wanawake hawa ni mavazi yao, mara nyingi hayana staha na hata kama ukimweleza juu ya hilo, huwa mgumu sana kubadilika.

  Siyo werevu wa kukabiliana na vishawishi (hasa waliopo maofisini). Ni wepesi sana kushawishiwa kwa ahadi ndogo ndogo au mvuto wa kimahaba wa wanaume watanashati. Kama hutakuwa makini na mwanamke huyu, unaweza kuwa kwenye foleni ya mapenzi bila kujua.

  Ni mjanja sana wa kutengeneza mambo, anaweza kuwa amefanya kitu, lakini akakudanganya kwamba hajafanya, hata kama ni kwa kutoa machozi! Huyu ni mkali wa kufanya usanii na usishtukie kirahisi.

  Kwa uchache tu, hizo ndiyo hasara za kuwa na mwanamke huyu wa mjini. Hata hivyo, usisahau kwamba, siyo kila mwanamke anaweza kuwa na tabia nilizoanisha hapo juu. Wengine wana baadhi, zaidi au pungufu lakini kwa wastani wengi wana tabia hizo.

  Sina shaka sasa, umeanza kuelewa japo kidogo sana kuhusu wanawake hawa wanaoishi katika mazingira tofauti. Swali la msingi sasa ni je, nani kati ya hawa anaweza kuwa mke bora zaidi ya mwenzake?

  Je, kuna ukweli kwamba wanawake wa kijijini wakiolewa na wanaume wa mjini hubadilika? Je, mwanaume wa kijijini anaweza kuoa mjini na kumchukua mwanamke huyo kwenda kuishi naye kijijini? Tuendelee kuona.

  VIPI MAZINGIRA?
  Wengi wanaamini wanawake wa vijijini wana mapenzi ya kweli, wazuri, wakarimu na wenye sifa zote nzuri za kuwa wake bora, lakini wakiolewa na kupelekwa mjini hubadilika! Sababu ambazo zinatajwa kusababisha kubadilika huku ni pamoja na kuathiriwa na mazingira.

  Inaelezwa kuwa, msichana ambaye amekulia kijijini ambapo hakuna mambo mengi kama mjini, akifika mjini anabadilishwa na mazingira. Hili siyo la kweli. Sikatai kwamba hakuna wanawake ambao wakifika mjini wanabadilika, lakini nataka kukuambia kwamba,
  kinachombadilisha siyo mazingira bali tabia yake.

  Kama mwanamke ana tabia chafu, hata akiwa kijijini anaweza kuendelea na uchafu wake vizuri sana. Lakini tunapotizama suala la mazingira, siku hizi za Sayansi ya Teknolojia, kuna vitu vingi sana vipo vijijini.
  Nishati ya umeme, mawasiliano yameondoa matabaka yaliyokuwepo zamani, angalau kwa kiasi kidogo, hivyo mwanamke wa kijijini hatakuwa na mageni sana atakapoenda mjini.

  Kama umeamua kuoa kijijini na kumchukua mkeo huyo kwenda naye mjini, ni vizuri sana kumwangalia kwa karibu, mweleweshe mji ulivyo, mtahadharishe na walaghai, mwambie jinsi unavyompenda na ulivyomuona wa thamani.

  Mtake aithamini thamani hiyo kwa kumchagua yeye, mambo haya na mengine yanayofanana na hayo yanaweza kumbabadilisha mwanamke wako na kuwa mwenye heshima na asiyebabaishwa na mabadiliko hayo.

  Kubwa zaidi ni vyema kama utapata muda wa kuzungumza naye kabla ya kumpeleka mjini, yaani picha nzima ya maisha ya mjini awe nayo kabla ya kufika mjini, hii nayo inaweza kumsaidia na kumfanya aishi kwa umakini bila kushawishika.

  Kumbuka kwamba, makosa mengi yanayofanywa na wanawake ni kwa sababu ya kuhadaiwa, sasa kama utakuwa umeshamfumbua macho mapema, siyo rahisi kudanganyika!
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mapenzi,mapenzi, mapenzi yanarani dunia
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  No!Money does!
   
 4. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,457
  Likes Received: 2,504
  Trophy Points: 280
  Yana Run Dunia...
   
 5. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Haya mambo yanategemea mambo mengi sana hadi kutokea na huwa na sababu tofaut tofauti kati ya m2 na m2,
   
 6. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Kuna TETESI kwamba watu wanaoishi mijini kufatia huu UTANDAWAZI now days wanatumia sana vyakula vya viwandani (industrial products) Samaki wa kopo, nyanya za kopo, Juice, Soda e.t.c .
  Haishii hapo mbogamboga, Nyanya, Hoho, Bamia, Nyanyachungu, Bilinganya, vilivyopo masokoni mijini siku hizi si vile vya asili (source macho yenu na nafsi zenu) ni vile vinavyooteshwa kwa muda mfupi.
  Watu wa vijijini bado wanakula vyakula vyote vya asili.
  Kwa sababu hizo ndiyo kuna watafiti wameanza kuthibitisha kwamba wanawake na wanaume wa mjini taste zao katika tendo la ndoa zinapoteza ladha ya asili, yaani Mwanaume wa kijijini akiingiliana na Mwanamke kijijini Mwanaume wa mjini atafaidika zaidi ambapo Mwanamke wa kijijini hatofurahia!
  Hivyo kwakua tendo la ndoa ndiyo hubeba sehemu kubwa ya ndoa kwangu mimi Mwanamke wa kijijini ndiyo mambo yote.
  Kazi kwenu mnaoishi mjini.
   
 7. sister

  sister JF-Expert Member

  #7
  Dec 19, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,028
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  hahahhahah unatutishia cyo
   
 8. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #8
  Dec 19, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Binafsi naamini ktk tabia na makuzi aliyoyapa huyo mwanamke,
  Bila kujali ni wa kijini au mjin,
  Tabia na makuzi ya ndio humfanya either awe mke afaae au vinginevyo,
  Mambo mengine ya mazingira,utandawazi nk,yanaongozwa na tabia ya mtu,
  Ni kwa jinsi gani atapambana nayo na kuendana nayo.
   
Loading...