Yule ambae humtaki ndio mumeo

Wadau wazima,

Kwa wadada unaweza kumkataa mwanaume kisa hana hela au ana hela ila roho haijaridhia basi unajiachia kwa vibwana ambavyo vinakuchezea tu mwishowe unatoa mimba unaachwa unasalitia mpaka unazeeka.

Tokea wimbo wa Vaileti mpaka Tetema hujaolewa hujui kwanini kwa maana yule unayemkata ndio kaja kwa wema ila wale unaowapapatikia ndio utaishilia ukitoa macho kama mjusi aliyabanwa na mlango.

Oh mara unasema huyu namchuna mpaka nini .
Mara nina wangu tuna miadi naye ya mbele we have future together mwenyewe hata home hajawahi kuja.

Anawatifuatifua marafiki zako kama nini halafu kutwa masaa ishirini nanne unakuwa unamsema unamuwaza unakuwa unamuota na unajiona kumbe ni mpita njia kazi yake ni kula na kusepa.

Sasa huyo uliyemkataa ataoa utabaki umekomaa hadi ukigongwa na pikipiki sio wewe unajeuriwa na pikipiki umeijeruhi.

Acha kuchagua utajikuta wewe ndio kila mtu anapita akichoka nyumbani kwake. Anajua unachopenda chakula vinywaji na pesa anakuja anakupa anaenda ila hata siku moja hutasikia ndoa.

Utavaa nguo zakila neno hadi ubadili uanze kuvaa vitengee. Utabakia ukiitwa majina kisa ni wewe ulitaka.

Kaa naanaye kupenda tatizo ni hili kumpenda asiyekupenda. Aliyekupenda tulia naye hata hela mkikaa pamoja mkawa serious mtazipata tu.

Au kama anazo basi jaribu kumuweka unavyotaka wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Very nice story

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshauri hata kwa mafumbo kaa kimya atakuletea wajomba nyumbani na utawatunza na kusomesha
mpaka mwisho maana baba zao hawaeleweki

Sent using Jamii Forums mobile app
Wee acha tu tatizo kanipita kiumri,wazee wameongea wamechoka,kuna kipindi alimkataa jamaa moja mchaga kisa meno yake ni yana rangi ya kama ya kahawia fulani,jamaa yupo vizuri ana biashara zake,nyumba ,usafiri.
 
Kaogopa meno duu kwani jamani atakuwa anakenua muda wote? Kuna umri ukifika atajutia ila kuna wengine wana bahati zao atampata amtakae, kuna dada naye anachagua anataka handsome sasa kuna mmoja alikuwa naye ila mme wa mtu alimwambia atamfukuza mkewe amuoe yeye miaka imepita hakuna kitu

Wee acha tumemwachia Mungu.
 
Ujue kapeace ishu iko hivi...we unayempenda yy hakupendi na anayekupenda kwa dhati we humpendi.....sijui why hii ishu asee

Sent using Jamii Forums mobile app

Huwa tunasingiziaga eti ni "Nature" Ukweli mapenzi mengi ya kibongo yamejaa unafiki na uwongo mwingi. Bahati mbaya wengi ni wavivu wa kufanya home work kabla ya kuukabidhi moyo kwa mwenza. Mara nyingi unakuja kujua ukweli wakati ushazama mzima mzima. Kinachofuatia nimateso mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom