Yuko wapi Roho Saba?

Jamaa alikuwa vizuri sana. Ila unajua enzi zile kila msanii alikuwa na specific producer wake ambae anamuelewa. So ilikuwa ikitokea producer akapotea, basi mara nyingi na msanii anapotea.

Mfano, Juma Nature alikuwa partner sana na Majani, combination yao ilikuwa perfect. Angalia kifo cha Roy yule wa G record ambavyo kiliyumbisha wasanii wengi sana waliokuwa chini yake.

Tukirudi kwa Roho 7, naweza sema kupotea kwake kumechangiwa na kupotea kwa Amba. Amba alikuwa producer flan hivi ambae alikuwa anawapatia sana kina Roho 7, Yaki (alitamba sana na ile ngoma ya tonight). Kitendo cha Amba kuachana na game ya mziki, naweza sema ndio kilisababisha kina Roho 7 na Yaki wajikite katika career zingine.

Maana hawa wote walijaribu kutoa ngoma nje ya Amba, ila hazikufanya vizuri.

Sikiliza ile Waite Polisi na Nakupenda Hip hop za Roho 7 au ile Tonight ya Yaki jinsi ambavyo combination ya Producer Amba na hawa jamaa ilivyokuwa perfect.
 
Mnamuongelea Major wa Jesh!!!! Mwenye Roho ya kipekee!!!

Mpole!!! Asieacha tamadun za ki"hiphop hata akiwa amevaa gwanda!!!

Nadhan Hatakua Ngome hapo dom!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom